b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, May 10, 2011

ASHANTI BOXI KUONESHANA UMWAMBA WA KUTUPA MASUMBWI NA MATIBWA BOXING TABATA SEGEREA.

LIGI ya kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa mkoa wa Ilala inatarajia kufanyika tena Mei 14 kati ya mabondia wa Ashanti boxing na Matibwa ambapo ianatarajia kutimua vumbi, Tabata Segerea Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha mkuu wa timu ya Ashanti, Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni mratibu wa ligi hizo mkoa wa Ilala alisema ligi hiyo itakuwa ikifanyika maeneo tofauti ya mkoa huo ili kuweza kuhakikisha inawafikia wakazi wote wa Ilala.
Alisema, lengo hasa likiwa ni kutaka kuwavuta vijana wengi kujiunga na mchezo huo na kuepuka kukaa vijiweni huku wakiwa na kipaji cha kucheza mchezo huo ambapo mapambano ya ligi hiyo yatakuwa katika raundi nne katika uzito tofauti.
Alisema, katika mchezo huo wa hivi karibuni kwa upande wa klabu ya Ashanti mabondia watakaoenda kuchuana na mabondia hao wa Tabata ni Ibrahim clas atakae chuana katika uzito wa kg 60, Uwesu Manyota 58, Ramadhani kimangala kg 56, Rashid Mhamila kg 54, Mack Edison kg 52 na Musa Mohamed kg 49.
Alisema, kwa upande wa Ashanti wamejiandaa vizuri kiushindani kwani mabondia hao wote wapo katika kiwango cha juu hivyo wanaimani kuwaangusha mabondia wa klabu hiyo ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo.
Alisema Super D mbali ya kuamasisha mchezo wa ngumi pia kutakua na DVD zilizoandaliwa na kocha uyo kwa ajili ya kujifunza sheria za mchezo pamoja na jinsi ya kufanya mazoezi ambazo kuna mabingwa wa Dunia akiwemo manny Paquao, Floyd Maywether, Oscar Dela Hoya, Mohamedi Ally na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment