Tuesday, May 31, 2011

BRASIL FILM FESTIVAL BADO INAENDELEA LEO PALE GOLDEN TULIP


Ndugu Waandishi wa Habari, Wanamziki na Marafiki wote,

          Tunayo heshima kubwa kuwaalika kwenye Onyesho la pili la Tanz Cine Brazil Festival-Brazilian Film Festival Tanzania, siku ya jumanne May, 31st Golden Tulip Hotel, saa 11.00 jioni hadi saa 07.00 usiku.
          Tanz Cine Brazil Festival- kwa mara ya pili itaonyesha Sinema nzuri za Brazili hapa Tanzania, pamoja na kufanya majadiliano na kubadilishana utaalam mbalimbali na Wanasanaa wa hapa nchini.Mwezi huu vilevile kutakuwa na majadiliano na Film Directing, itakayo ongozwa na Monoca Monteiro,  Chuo kikuu cha Dra es Salaam.
        Ufunguzi wa hii sherehe ya wazi ni June, 3rd  Makutano, ambapokutakuwa na Bralian band Pandero Repique Duo na muziki wa Tnzania Mulfred. June 4th kutakuwa na onyesho la picha kwenye TV ya nje, Makutano kuanzia 07 jioni., na 8th Nafasi Art Space sinema maarufu ya Brazil; City of God, Usikose. 
Pia utaweza kuonana na Producer kutoka Brazili Pandeiro Repique Duo na utweza kuuliza maswali ya matembezi yao.

No comments:

Post a Comment