Tuesday, August 11, 2015

WASANII WATAKIWA KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kushoto) akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa na watoto wanaondaliwa na Baraza hilo kupitia programu ya ‘Sanaa kwa Watoto’ wakati wakitumbuiza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanatoka shule ya Msingi ya Msimbazi iliyoko Ilala jijini Dar es Salaam. Katikati ni Msanii wa filamu Honeymoon Mohamed na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Stadi za wasanii Bi. Vick Temu.  

Sehemu ya watoto wanaoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia programu yake ya Sanaa kwa Watoto wakicheza igizo kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanaosoma Shule ya Msingi Msimbazi walikuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa Sanaa. 

Wasanii kutoka Kundi la Ngoma za Asili na Maigizo la Jivunie lenye  makazi yake eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakionesha ufundi wao katika kuchenza ngoma za asili kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu.Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wametakiwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida wanayoipata kupitia kazi zao za Sanaa kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalum ili kujijengea mtandao wa kudumu wa masoko, uhalali na taswira nzuri kwa jamii.
Wito huo umetolewa mapema wiki hii na mtengeneza filamu wa Tanzania mwenye makazi yake nchini Marekani Bi. Honeymoon Mohamed wakati akiwasilisha mada kuhusu Filamu za Kitanzania na Masoko kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
“Wasanii wanaitegemea jamii kama chanzo cha mapato yao hivyo ni lazima wajenge utamaduni wa kurejesha kile kidogo wanachokivuna kutoka kwa jamii kupitia kusaidia watu wenye uhitaji maalum” alisema Honeymoon ambaye filamu yake ya Daddy’s Wedding  imeshinda tuzo kwenye tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF) lililomalizika hivi karibuni eneo la Ngome Kongwe, Zanzibar. 
Aliongeza kwamba watoto wenye uhitaji maalum wanapata faraja na kuhisi kupendwa na jamii pale wanapotembelewa mara kwa mara na watu mbalimbali wenye umaarufu na nafasi kubwa katika jamii hivyo wasanii wetu hawana budi kuwa sehemu ya kujenga faraja hii kwa watoto hawa.
Kwa mujibu wa Honeymoon wasanii wa Tanzania wako nyuma katika kuikumbuka jamii hususani kutembelea makazi ya watoto wenye uhitaji maalumu na kuchangia huduma mbalimbali zinazokuwa zinahitajika.
“Watoto wenye utindio wa ubongo wako wengi, kuna wale wenye ulemavu wa ngozi na wengine wanaishi wakiwa yatima kwenye vituo mbalimbali lakini wasanii wetu wamekuwa wazito kuwakumbuka. Wasanii hawana budi kuyakumbuka makundi haya maana wako kwa ajili ya jamii” alisisitiza.
Awali kabla ya uwasilishaji wa mada hiyo, watoto wanaoandaliwa kupitia programu ya BASATA ya ‘Sanaa kwa Watoto’ kutoka Shule ya Msingi wa Msimbazi iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam walitoa burudani mbalimbali za Sanaa wakisaidiana na Kikundi cha Sanaa cha Jivunie chenye maskani yake neo la Mbagala Manispaa ya Temeke.

Sunday, August 9, 2015

MISS KILIMANJARO AMBASSADOR 2015 YOLANDA SHAYO AINGIZWA MITINI NA MUANDAJI

Mshindi wa Miss Kilimanjaro 2015, Yolanda shayo


Na Mwandishi Wetu
Muandaji wa shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015, Jackline Chuwa adaiwa kuingia mitini na fedha za zawadi za warembo na malipo kwa watu aliofanya nao kazi kufanikisha shindano hilo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya familia ya mshindi wa shindano hilo zinasema kuwa vikao vya mara kwa mara hufanyika kupanga mkakati wa kuvamia ofisi za BASATA kujua hatma ya binti yao Yolanda shayo.

ILIKUAJE:
Wakati wa kutangaza matokeo ya ushindi siku ya fainali za mashindano hayo usiku wa julai 24,mshindi alikabidhiwa Televisheni kama zawadi na kiasi cha pesa kilichoadiwa kutolewa na mdhamini mkuu ambae ni Coca cola.
Cha kustaajabisha muandaji huyo alienda ofisi za kampuni hiyo na kuchukua kiasi hiko cha fedha ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza lakini mpaka leo mrembo huyo anahaha kupata zawadi yake.
Yolanda aliamua kufunga safari mpaka ofisi za Bonite Bottles na kuwauliza wahusika kuhusu zawadi yake na alijibiwa kuwa muandaji huyo alishakabidhiwa fedha hizo siku nyingi.
Mrembo huyo alichukua hatua nyingine ya kumpigia simu Jackline na kumuulizia kuhusu zawadi yake ya fedha taslimu alioadiwa jukwaani na wadhamini wakuu,chakushangaza muandaaji huyo alitoa kauli ya kumvunja moyo kwa maana hatoipata kabisa kwa kisingizio eti hakupata faida.

FAMILIA YA YOLANDA:
Familia ya mrembo huyo imechukizwa na kitendo cha muandaaji huyo kwa kuingia mitini na zawadi ya binti yao na bila kumkabidhi mikononi mwa kampuni hiyo ambapo ilitoka ahadi kuwa atakuwa balozi wa kampuni hiyo kufanya kazi mbalimbali kama balozi wa kinywaji hiko mkoani humo.
Wazazi wa mrembo huyo wamedhamilia kutinga ofisi za BASATA kufatilia mkataba wa bitni yao kutokana hali ya sintofahamu kuendela toka binti yao atawazwe kuwa mshindi mnamo julai 24.
Pia wanafamilia wametoa shutuma nzito kwa shindano hilo wakihoji ni kwanini  msanii wa bongo flava anapewa milioni 25 kutumbuiza wakati binti yao ambae ndiye mshindi anambulia zawadi ya televisheni pekee.

WASHIRIKI WENGINE:
Hali ni tata pia kwa washiriki wa walioingia tano bora hasa namba nne ambae alizawadiwa laki nne na mapazia kutoka kampuni ya Mapazia house lakini chakushangaza muandaji huyo aliingia mitini na fedha hizo na kumuacha mrembo akirudi nyumbani na mapazia tu.
Mrembo huyo Willice Donard amelalamikia kitendo cha muandaji huyo kumjibu majibu ya dharau pale alipompigia simu kuulizia zawadi yake.
Habari zinasema kuwa mrembo alieshika namba tano,Femy Lema alipokonywa nusu ya kiasi cha fedha alichokabidhiwa jukwaani ikiwa ni zawadi ya kuingia tano bora.

KAMATI YA MAANDALIZI:
Hali si shwali kwa upande wa kamati,habari za uhakika toka  kwa watu walioshiriki kumpa sapoti muandaaji huyo zikizadai kuwa amewaingiza chaka na kuwazulumu haki yao ya malipo,mpaka sasa hawajui fedha zao watazipataje.
 
KAULI ZA MUANDAAJI:
Kauli za muandaji zilizojaa dharau na kejeli kwa watu wanaodai haki zao ndizo zilizowapandisha hasira na kufanya baadhi ya watu kutoboa ukweli huu kwani amekuwa akiwaambia anaenidai aende mahakamani huko ndiko haki ya mtu hupatikana kwa kisingizio eti amesomea sheria.
 
KUMBUKUMBU ZAKE:
Kumbukumbu za muandaaji huyu zinaonesha ni mtu ambae anapenda mambo ya ujanja-ujanja na kujipatia faida kubwa kupitia majina ya watu kama alivyotaka kumtumia Zari Hassan kuvuta watu wengi kuingia katika tamasha lake na angali hakuwa na mkataba wowote na Zari.
Kitendo hiko kilimfanya Diamond Platnumz kutaka kususia na kuandika maneno makali katika ukurasa wake wa instagram,kitu kilichompelekea kutozwa faini na uongozi wa Zari.

BASATA:
Wito umetolewa kwa baraza la sanaa kuwa makini kwa kutoa vibali kwa waandaji wasio na uhakika na shughuli wanazofanya kama ilivyotokea kwenye hili shindano la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015.
Tunaamini dhamira ya shindano hili ni nzuri na lina manufaa kwa jamii kuhusiana na utalii,utamaduni na kazi za kijamii,shindano hili lina faida ila tatizo liko kwa muandaaji mwenyewe kana kwamba hana malengo na shindano hilo.
Lawama za pekee ziende kwa Basata kwani shindano hili lilipelekwa kienyeji bila usimamizi wowote kama ilivyo kwa mashindano mengine makubwa,isitoshe kanuni na taratibu hazikufuatwa mwanzo mwisho ndiyo maana leo tunapata malalamiko ya mshindi Yolanda shayo kuingizwa mitini zawadi na mkataba wake.


TANZIA: MBUNGE WA VITI MAALUMU (CUF) - MASASI AFARIKI KWA AJALI YA GARI

Monday, August 3, 2015

YOLANDA SHAYO BALOZI WA MKOA WA KILIMANJARO ATEMBELEA VITUO VYA WATOTOTO YATIMA

 Yolanda Shayo akisaidia kugawa chakula kwa watoto na viongozi wa vituo hivyo,ambapo alishiriki kwa pamoja nao katika chakula cha mchana.

Mrembo aliebuka kidedea kwenye shindano la kumsaka barozi wa mkoa wa Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ametembelea vituo vya watoto yatima katika eneo la mamba Malangu moshi vijijini.
 
Shughuli hiyo ilifanyika mapema jana ambapo mrembo huyo alitembelea vituo vinee ambavyo ni Msoroe,Mrieni,Kikoro na kotela kwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto na kula nao chakula cha pamoja kilichoandaa kwaajili ya watoto hao.
 
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na mrembo huyo ni kalamu,madaftari,rula na sabuni za kufulia na kuogea,Yolanda alipata fulsa ya kuongea na viongozi wa vituo hivyo ambapo alibaini changamoto balimbali zinazokabili vituo hivyo.

Yolanda ambae ni Miss Kilimanjaro Ambassador wa mara ya kwanza ameonesha jitihada zake za kuanza kazi ya urembo kwa kuitumikia  jamii yake ambapo alikuwa ana wito huo tangu akiwa mtoto.
Kwa nafasi aliyoipata mrembo huyo ameaidi kuwa kinara kuutangaza utamaduni wa mkoa wa kilimanjaro na kuvitangaza kitaifa na kimataifa vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya mkoa huo.

"mbali ya kuwa mrembo na balozi wa mkoa wa kilimnjaro nitahakikisha natumia fulsa hii kupeleka ujumbe mbalimbali kwa jamii yangu ikiwemo kuwahimiza vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba" aliongea Yolanda.