Monday, February 16, 2015

'NEW AUDIO' DAKEE FT SHEB Q - REST IN PEACE

Kwa kupakua wimbo mpya wa Dake Ft Sheb Q - Rest In Peace Bofya Link hapo chini

FILAMU YA C.P.U KUINGIA SOKONI LEO


Na Mwandishi Wetu
FILAMU kubwa ya C.P.U Kitengo cha kutetea Watoto imeingia leo sokoni kwa njia ya mtandao, lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi Ulimwenguni, hivyo kwa utaratibu wa kampuni ya usambazaji ya Proin Promotions ni kuuza katika mtandao baadae katika Dvd na njia nyingine.
Leo Jumatatu tarehe 16.February. 2015 inapatikana mtandaoni unaweza kununua filamu hiyo kwa kutembeleawww.proinpromotions.co.tz na kununua filamu ya C.P.U na filamu zingine za Proin Promotions utanunua na kuangalia full HD.
Sinema ya C.P.U imeshirikisha wasanii zaidi ya 230 huku wasanii wakongwe wenye majina kama Kulwa Kikumba ‘Dude’ Dotnata, Richard Mshanga ‘Mzee Masinde’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Sauda Simba, Subira Wahure, steve Sandhu, Nkwabi Juma, Mohamed Funga funga ‘Mzee Jengua’ Mobby Mpambala wakiwa vinara wa sinema hiyo.
C.P.U sinema ya kimataifa wiki ya pili itapatikana katika Dvd na kupatikana nchi nzima kutokana na mfumo mpya wa Proin Promotions kuuza kwa njia ya mtandao na wiki inayofuata utaweza kununua katika Dvd, NUNUA NAKALA YAKO HALALI YA C.P.U SASA!
Monday, February 9, 2015

SHYROSE BHANJI MGENI RASMI USIKU WA LADY IN RED 2015..Kufanyika Nyumbani Lounge  Ijumaa Februari 13

Na Andrew Chale
MBUNGE  wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh. Shy rose Bhanji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye usiku maalum wa Lady In Red 2015, Ijumaa ya Februari 13, kwenye ukumbi wa M.O.G Bar (Zamani Nyumbani Lounge) huku mitindo ya nguo nyekundu zitauzwa kwa ajili ya siku ya wapendanao ‘Valentine day’.
Mwaka huu ni wa 11, tokea kuanzishwa kwa  Lady in red, ambapo itajumuisha wanamitindo mbalimbali pamoja na wabunifu tofauti katika redcapert iliyotayarishwa maalum kwa ajili ya usiku huo.
Kwa mujibu wa wandaaji wa Usiku huo wa Lady in red 2015, Asia Idarous Khamsin ‘Mama wa Mitindo’  akishirikiana na Fashionnews  Tanzania, alieleza kuwa usiku huo utapambwa na Gusa Gusa Min Band,  kundil la Ngoma za asili na wengineo.
“Ijumaa  ya Februari 13 ni siku maalum ya usiku wa Lady in red. Kwa kiingilio cha sh 10,000 kawaida na sh. 20,000 kwa upande wa V.I.P. Nguo nyekundu za Valentine day zitauzwa sambamba na kufurahia   burudani mbalimbali” alisema Asia Idarous na kuongeza kuwa vazi maalum la usiku huo ni rangi nyekundu na tiketi za usiku zinapatikana Fabak fashions, Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere na Kobaz shop, Nyumbani Lounge.
Aidha, usiku huo wa Lady in red  2015, mdhamini mkuu ni Maji Poa, wengine ni Darling hair, , Vayle Spring,  Eventlite, michuzi media group, chaneli ten, magic fm, sibuka tv, profile and style, Jambo Leo, mashughuli  blog, vijimambo blog, Voice of America, Mo blog, Supernewstz blog na wengine wengi.


Sunday, February 1, 2015

ALI KIBA AAHIDI MAKUBWA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA Februari 12


Msanii wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba akiimba akapela moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano huo na wandishi wa habari (Hawapo pichani), katika mkutano huo juu ya ushiriki wake kwenye tamasha hilo linalotarajia kufanyika Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzibar. kushoto kwake, ni 
Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, Simai Mohammed.

Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, wandaaji wa tamasha la Sauti za Busara, Simai Mohammed (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wanahabari Jijini Dar es Salaam, juu ya tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika, Februari 12 hadi 15, mwaka huu, Ngome Kongwe, Zanzibar. Wengine (kushoto) ni Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani. na upande wa kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na msanii wa bongo fleva nchini, Ali Kiba (kulia).
Simai, Dj Yusuf na Kiba wakiwa wameunganisha mikono kwa kusalimiana ikiwa ni ishara ya Umoja na Amani, kama Kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo inavyohimiza amani.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Andrew Chale

Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga nyoyo watu mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzubar.
Ali Kiba alieleza hayo leo Alhamisi, Januari 29. wakati wa mkutano wa ulioandaliwa na Busara Promotions, wandaaji wa tamasha hilo kubwa la Kimataifa linalofanya muziki wa 'Live',  ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanamuziki na vikundi 37, watatoa burudani kwenye tamasha hilo kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari, Ali Kiba alisema kwa sasa amejiandaa kutoa burudani ya aina na ambayo itakonga nyoyo kwa watu wote watakaojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
"Hii itakuwa ni zawadi kwa watanzania wote kunishuhudia nikiimba 'live' bila kutumia 'cd' kama wafanyavyo wengine. Mimi ni mwanamuziki na nimesoma muziki hivyo nitapiga muziki wa nguvu jukwaani" alisema Ali Kiba.
Na kuongeza kuwa, kwa sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa kujifua na bendi maalum  kwa ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye ni msanii kwani muziki aliusomea na kujifunza huko nyuma alipokuwa  katika Nyumba ya kuibua vipaji THT, ambapo alijifunza vitu vingi ikiwemo kuimba muziki wa bendi na 'live'.
Aidha, aliwaomba wapenzi na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingi 
kushuhudia tamasha hilo kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje watatoa burudani ya kipekee.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Busara Promotion, wandaaji wa tamasha hilo, Simai Mohammed, alisema tamasha limeweza kuongeza ajira na uchumi wa Zanzibar kwani pia limeongeza fursa za utalii.
Kwa upande wake, Meneja wa tamasha  hilo, Journey Ramadhani, alisema tamasha hilo limeweza kuongeza fursa kila mwaka ikiwemo kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania kwa asilimia 90, ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na watendaji kazi na wa kujitolewa watakolipwa katika kusaidia tamasha hilo, zaidi ya watu 150.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf' alisema tamasha hilo limeweza kuibua wasanii mbalimbali ikiwemo kujitangaza kimataifa.
Aidha, Dj Yusuf alieleza kuwa, tamasha la mwaka huu litaendana na kauli mbiu ya kuimiza Amani, pia wameandaa tuzo maalum na zawadi maalum kwa wasanii wa Tanzania watakaoshinda katika kutunga nyimbo za amani.
Mbali na Ali Kiba, Wasanii wengine Isabel Novella kutoka  Msumbiji, Ihhashi Elimhlophe (Afrika Kusini),   Tcheka (Cape Verde),   Diabel Cissokho (Senegal),  Culture Musical Club (Zanzibar),  Msafiri Zawose (Tanzania),   Aline Frazão (Angola),   Tsiliva (Madagascar),   Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band (Tanzania),   Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar),   Thaïs Diarra (Senegal / Mali / Uswisi),   Liza Kamikazi and band (Rwanda),   Erik Aliana (Cameroon),  Mpamanga (Madagascar),   Mgodro Group (Zanzibar),   Rico Single & Swahili Vibes (Zanzibar),   Zee Town Sojaz (Zanzibar),   Ifa Band (Tanzania) na wengine wengi. Maelezo zaidi yanapatikana katika www.busaramusic.org