b..

B1

Wynem

animation

Saturday, June 30, 2012

PICHA ZA MATUKIO YA MKUTANO WA WADAU NA WAFANYABIASHARA WADOWADOGO(MACHINGA) @ MACHINGA COMPLEX

Mmoja kati ya watoa mada wakiatoa mada kwa wadau waliohudhuria.
Viongozi wa meza kuu wakijadili jambo.
Baadhi wa wadau waliohudhuria katika mkutano huo.

Mwisho waandaaji walitoa shukrani kwa wadau
Habari, tunashukuru sana kwa wale mliopata muda na kujitokeza leo katika mkutano huu uliofanyika kwa mafanikio na kuudhuriwa na takribani watu 3000 pale machinga complex, na hata wale ambao hamkufanikiwa kupata nafasi iyo tuko pamoja na matumaini yangu mlikuwa katika shughuli za ujenzi wa taifa.

GARI LA HARUSI LAPATA AJALI, LABURUZWA NA LORI.


Friday, June 29, 2012

RAY AZINDUA FILAMU YA SOBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS

Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre   kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.Picha na Mpiga picha Wetu
Msanii wa Filamu Nchini Visent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps.Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya lei kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre vilivyotolewa na Kampuni ya Steps wakati wa Uzinduzi wa filamu yao Mpya ya Sobing Sound.Picha na Mpiga Picha Wetu
Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre   kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.Picha na Mpiga picha Wetu

Na Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu nchini  Visent Kigos 'Ray'  amezindua filam yake  mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.Filam hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filam hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5  kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaamAkizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba  watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha uku wengine wakiendelea kutahabika kitendo ambacho si kizuri.Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atakuwa kila filamu anayotoa atakikisha japo kidogo kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima kwana awajapenda.Alisema msaada uliotolewa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza amesema kampuni ya  Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kutushawishi tuwe tunawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingila magomu.Nae mmoja wa wakilishi wa Kampuni ya Steps Ignatus Kambarage amesema swala la watoto yatima ni letu sote na wala alichagui kwa kuwa tunawajibu na angalau kidogo tunachokipata kupitia filamu zetu tunarudisha kwa kutoa shukrani zetu.

DEIDRE LORENZ KAINGIA KWENYE MAPENZI NA TANZANIA

Deidre Lorenz akimkabidhi picha ya Ground Zero (New York) Rais wa Mt. Kili Marathon 1991 Onesmo Ngowi baada ya kukimbia mbio hizo

Na Mwandishi Wetu
Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.
Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana Tanzania.
“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote”aliendelea kusema Deidre Lorenz.
Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana.
Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental Races.
Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
Kwa kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.
“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.
Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.
Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.

Wednesday, June 27, 2012

SUPER D AITWA KUTOA UJUZI WA MASUMBWI IFAKALA, KILOMBERO

KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila
'Super D' amepata mwaliko wa kwenda kufundisha  pamoja na kuwapati ujuzi aliokuwa nao katika mchezo wa masumbwi mwaliko huo alioupata kutoka mkoa wa Ifakala mjini Kilombero kutoka kwa klabu ya Kilombero Boxing Klabu  ambaye mwenyekiti wake ni Hiyari Bohari na katibu wa Klabu Hiyo ni Ramadhani Mindu wamempatia mwaliko wa siku mbili
Kocha huyo kwa ajili ya kuwanoa Makocha na kuwapatia ujuzi wa ziada mabondia chipukizi mwaliko huo unaomtaka kwenda kutoa ujuzi wa mchezo wa masumbwi kwa kushirikiana na kocha kutoka mkoa wa Morogoro Boma Kirangi mafunzo hayo yanayotakiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agost yanaonekana kuwa na umuhimu kwa kuwa vijana wengi wamejitokeza kuwa na mwamko wa mchezo wa masumbwi nchini
Hata hivyo Super D 'alisema kuwa amepokea mwaliko kwa furaha na yupo tayali kutoa ujuzi wake alioupata wakati wa mafunzo ya kimataifa kwa vijana watakaojitokeza' Super D aliongeza kwa kusema mchezo wa maumbwi nchini unapendwa na wengi ila unakosa wafadhili kwa ajili ya kutoa sapoti mbali mbali Super D ametoa wito kwa makampuni mbalimbali  pamoja na wadau wa michezo kujitokeza kusaidia kwa namna moja au nyingine hususani mafunzo anayotaka kuyatoa akiwa mkoa wa Kilombero
Ambapo vijana wengi wanapenda kufahamu zaidi mchezo huo kwani kuna vijana zaidi walioamasika kucheza mchezo huo kwa kuwa na nia moja ya kuhakikisha mchezo wa masumbwi  unawafikisha mbali ya kuwa ni mchezo pia utawapatia ajira 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali

Tuesday, June 26, 2012

NAPE KATIKA MAHAFALI YA WANA-CCM TAWI LA CHUO KIKUU CHA TEKU, MBEYA

 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na viongozi wa  CCM mkoa wa Mbeya baada ya kuwasili leo asubuhi kwa ajili ya ziara ya siku mbili mkoani humo.

Nape akiongozwa na vijana wa Chipukizi wa CCM, baada ya kuwasili mjini Mbeya kuanza ziara hiyo.
Nape akiwasalimia baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya alipokwenda hoteli ya Paradise kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya wana-CCM hao
Nape akishiriki kucheza muziki wa kwaito na wana-CCM tawi hilo la TEKU

Wana-CCM wakila kiapo pamoja na wanachama wapya kwenye mahafali hayo

Nape akizungumza na wahitimu na wanachama hao. 
Hivi ndivyo walifanya kabla ya kumkabidhi picha hiyo.
 
Nape akaiangalia picha hiyo kwa makini 
Nape akiibusu picha yake baada ya kuzawadiwa na wana-CCM tawi la TEKU

Nape akimkabidhi kadi ya CCM, mmoja wa wanachama wapya waliopewa kadi wakati wa mahafali hayo

Monday, June 25, 2012

BONANZA LA NANE NANE KURINDIMA KAWE

Salum Suleiman 'Sule Junior'

Mwandishi Wetu
Bonanza kubwa la mchezo wa mpira wa miguu linaloitwa 'Nane nane soccer bonanza' linatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es Salaam siku ya kilele cha sherehe za nane nane.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kampuni ya SULE'S INC. & ENTERTAINMENT, Salum Suleiman ambao ndiyo wadhamini wa Bonanza hilo timu mbalimbali kutoka katika maeneo ya wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam zitashiriki. 
"Maandalizi ya bonanza hili yameshafikia katika hatua nzuri kabisa, Kamati imefanya kazi nzuri mpaka kufikia hapa na tunategemea bonanza hili litafanyika kwa mafanikio makubwa,"alisema Suleiman.
Akizungumzia timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo, Suleiman alisema,"tunatarajia kuwa na timu nane ambazo zitachuana katika kuwania kombe siku hiyo na mashindano yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano."
Alisema wameamua kuliendesha bonanza hilo kwa mtindo wa mtoano ili timu ziweze kutoa ushindani wa kutosha na kuburudisha watu watakaojitokeza katika bonanza hilo.
"Washindi watapata zawadi, kwa sababu mshindi wa kwanza atatwaa kombe, mshindi wa pili pia atapata zawadi, mchezaji bora, mfungaji bora, kipa bora na mchezaji mwenye nidhamu wote hao watapata zawadi."
Sherehe za nane hufanyika kila mwaka sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni siku ya kuadhimisha siku ya wakulima.

Sunday, June 24, 2012

NGOMA MPYA KUTOKA KWA NOCOZ ft BOU NAKO - KAZI.

Nocoz are back again this time wakimshirikisha BouNako toka N2N,hapa sasa NOcoz na NAkoz ndani ya pini moja ndani ya beat ya mtumzima Samtimber na vocals/mixing ikiwa ni pande za noizmekah.com chini ya defxtro.Support kwa hiphop chipukizi ndio mpango na pini linakwenda kwa jina la KAZI..ikiwa ni kazi kweli ya hardcore hiphop inayodokeza ugumu wa maisha na vikwazo vya kizembe vinavopelekea machizi kufilisika, kulosti maisha.Skiliza pini na support hiphop music from tanzania,One
BOFYA HAPA KWA KUUSIKILIZA NA KUUDOUNLOAD 4 PROMO ONLY.

WAZAZI WA CHEKA NA KASEBA WATAMBIANA

Baba Mzazi wa bondia Fransic Cheka , Bonifasi Cheka kulia akiwa amemkunja baba mzazi wa Japhert Kaseba, Josepher Kaseba wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuzungumzia mpambanbo wa watoto wao utakaofanyika siku ya sabasaba katika uwanja mpya wa Taifa. 
Baba wa bondia Japhert Kaseba, Josepher Kaseba kushoto akipeana mkono na Baba Mzazi wa bondia Fransic Cheka , Bonifasi Cheka wakati walipokuwa wakizungumza na waandishi wa Habari Dar es salaam leo kwa ajili ya kutangaza mpambano wa watoto waoi utakaofanyika siku ya Saba saba.


Baba Mzazi wa bondia Fransic Cheka , Bonifasi Cheka kushoto akizungumzxa na waandishi wa habari Dar es salaam lkeo kuusu mpambano wa mwanae utakaofanyika siku ya sabasaba kulia ni Baba wa bondia Japhert Kaseba, Josepher Kaseba wa pili kushoto ni meneja matukio wa Dar Live na Promota wa Mpambano huo Kaike Silaju.

Saturday, June 23, 2012

MAMA WEMA AJIFICHA CHUMBANI KUKIMBIA WAANDISHI WA HABARI

Na Waandishi Wetu

Takribani saa 18 tangu alipotamba runingani akimnadi mwanaye kuwa mambo safi, mama mzazi wa Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu amejificha chumbani baada ya waandishi ‘vichwa ngumu’ kutinga nyumbani kwake wakitaka kufanya naye mahojiano, Risasi Jumamosi lilishuhudia tukio la ajabu.
NI SINZA-MORI, DAR 
Tukio hilo lililokuwa kama filamu ya kivita lilijiri nyumbani kwa mzazi huyo wa Wema, maeneo ya Sinza-Mori, Dar es Salaam Juni 20, mwaka huu, mchana kweupe wakati kukiwa na marudio ya kipindi alichotumia kumnadi mwanaye na kuwananga marafiki zake.

Baada ya kugonga geti na kukaribishwa ndani na binti waliyemkuta, mapaparazi hao wawili walisimama kwenye mlango wa nyumba kusubiri binti huyo akamuite mama Wema ambaye wakati huo alisikika kupitia dirishani akimsimulia mtu kwenye simu yaliyojiri baada ya kubwatuka runingani siku moja iliyopita (jana yake).
“Eee! Nakwambiajee, nimewachamba ile mbaya kwenye televisheni na nimewaambia wasikanyage nyumbani kwangu,” alisikika mama Wema wakati binti aliyekwenda kumwita akisubiri amalize kuzungumza na simu amwambie kuna wageni wake (waandishi wawili).
‘MUVI’ LA KIVITA LAANZA
Sekunde kadhaa baada ya kukata simu, yule binti alisikika akimpasha habari kwamba kuna wageni wake, ndipo alipochungulia dirishani na kugundua kama aliokuwa akiwazungumzia muda mfupi ndiyo wameingia baada ya kuwaona wakiwa na vitendea kazi kama kamera, notebook, vinasa sauti na kalamu.
Kwa macho ya kawaida aligundua anaowaona mbele yake ni waandishi lakini kwa mwendo wa kubwatuka kwa sauti, alianza kwa kuuliza pasipo kutoa nafasi ya kupewa majibu.
“Ninyi ni waandishi, si ndiyo eeh. Nauliza ninyi ni waandishi? Nimesema sitaki kuona mwandishi anakuja nyumbani kwangu. “Eeeh… Hamnijui eeeh, hamjui mashetani yangu, eeeeeeeeh… nyie ni…(akaporomosha matusi mfulululizo). Ama kweli nyie vichwa ngumu! Pamoja na kuchimba mkwara mmekuja!” alisikika mama Wema.
BINTI AWATIMUA WAANDISHI
Mama Wema alipogundua kwamba waandishi wako ‘fulu’ na vifaa vya kazi, ilibidi ‘amualati’ binti huyo awapopoe kwa mawe na kisha kuwasakizia mbwa ambaye alionekana si wa ulinzi (ni yule Fiona wa Wema).
MAHOJIANO KUPITIA DIRISHANI
Wakati akiendelea ‘kuwaka’ na kusababisha mtaa mzima kurindima, waandishi waliendelea kufanya naye mahojiano kupitia dirishani wakitaka majibu ya maswali yao yaliyohusiana na utajiri wa ghafla wa Wema lakini majibu yakawa ni kelele za mayowe kutoka kwa mzazi huyo.
Timu ya waandishi ilipojiridhisha kwa picha za kumwaga, iliondoka na kumwacha mama Wema akiendelea kuporomosha matusi akiwa chumbani.
Imeandikwa na Richard Bukos, Erick Evarist na Issa Mnally.Chanzo:www.globalpublishers.info

FRANCIS MIYEYUSHO AMTWANGA BONDIA JON MASAMBA KUTOKA MALAWI.

Bondia John Masamba kutoka Malawi akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi naFrancis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana. 
Bondia Obote ameme akioneshana kazi na Cosimasi Cheka
Bondia Francis Miyeyusho akimshambulia bondia kutoka Malawi John Masamba wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Miyayusho alishinda kwa K.O Raundi ya 5.
Bondia Miyayusho akisikiliza wimbo wa taifa wakati wa kuimba nyimbo za matasifa mawili

Thursday, June 21, 2012

DEIDRE LORENZ ATUA MJINI MOSHI NA SHAUKU YA KUUNA MLIMA KILIMANJARO

Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA Bara la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi.
Na Mwandishi Wetu
Mcheza sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka.
 Ujio wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake.
 Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea kurudi kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.
 “Sasa nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya” alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York City linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial Capital) la kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya Uhuru Park.
 Mji wa Moshi na viunga vyake vinarindima kwa ujio wa watalii wengi kutoka Marekani ambao wamekuja kushiriki kwenye mbio hizi zilizojijengea umaarufu mkubwa kwa kuitangaza Tanzania nchini Marekani. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamania wa Tanzania nchini Misri.
Mbio hizi zimejijengea umaarufu mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo nyingi baadhi zikiwa zimetolewa na Wonders of the World Magazine lenye wasomaji zaidi ya milioni 5 likiwa limezipa nafasi ya 2 kama mbio zenye hadhi ya kukimbiwa duniani wakati jarida la Forbes la Marekani  lenye wasomaji wengi duniani limeipa nafasi ya kwanza. Ndio maana Manispaa ya Moshi itampa barabara na kuiita “Marie Frances Boulevard”mwaka 2009.
 Mbio hizi hukimbiwa na watalii wa Warekani wanaokuja Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro Marathon zinajulikana kama 7 continental races zikiwa zinakimbiwa katika mabara 7 ya dunia.
 Ratiba ya Deidre Lorenz inaonyesha kuwa kesho ijumaa atakitemnbelea kituo cha watoto yatima cha Upendo kinachoendeshwa na watawa wa Precious Blood. Lorenz atakaa na watoto hao na kuwasomea hadithi mbalimbali za watoto zilizoandikwa na Waltz Disney mwandishi maarufu wa karne ya ishirini wa Marekani.
 Siku ya jumamosi atatembelea hospitali ya KCMC ambapo atakutana na manesi ili kuwapa shavu kwa kazi yao nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya jumamosi atahudhuria Pasta Party ambapo atapata nafasi ya kukutana na wakimbiaji wengine na kuchagua namba ya kukimbia kesho yake siku ya jumapili tarehe 24 juni.

KICHUPA CHA SAIDAWG - GETHOKING

KAMATI YA MISS TANZANIA YAWAPA SOMO WASIRIKI WA MISS DAR INTERCOLLEGE.

KAMATI ya Miss TAnzania jana imetembelea kambi ya Miss Dar Intercollege iliyopo kwenye hoteli ya The Grand Villa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwafunda.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika ijumaa ya kesho katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na chuo cha Usmiamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza na warembo hao, mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye aliwataka warembo hao kufuata miongozi na kanuni za shindano hilo ikiwemo kuwa na nidhamu.
Alisema urembo si sura na umbo zuri bali unahusisha pia nidhamu katika jamii hivyo amewataka warembo hao kuzingatia hayo.
"Nafahamu ninyi ni wasomi wazuri hivyo mmeyapokea vema mafunzo tuliyowapa...hatutarajii kusikia mmoja wenu anachafua hali ya hewa katika siku za usoni na mambo ya skendo skendo,"Alisema Makoye.
Dina alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa uziki wa kizazi kipya nchini Nasib Addul ‘Diamond’ sambamba na bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

DRESS CODE @WEMA SEPETU'S GLITTERED NIGHT

 MAHALI::HYATT KILIMANJARO......Kempsyk
TAREHE::23 JUNE ...Jumamosi hii
BURUDANI:: Mwasiti, Linah, Shaa, Rachel......
SPECIAL APPEARANCE:OMOTOLA JALADE (From Nigeria)
DRESS CODE :: RED CARPET SWAGG...ntakuonesha hapahapa 360 % lile lakuzunguka mbele na nyuma kote panoge 

Tuesday, June 19, 2012

JACKLIN WOLPER FUNGUKA KUHUSU UVUMI WA KUNYANYANG'ANYWA GARI.

Katika stori za town sasa hivi ni kwamba Mwigizaji Jackline Wolper amenyanga’nywa gari ambalo ameonekana nalo kwenye misele mbalimbali Dar es salaam.
Kupitia blog yake J ameamua kujibu hizo stori ambazo zinadai kanyanga’nywa gari na mwanaume aliempatia.Kasema “Uvumi unaonea kwenye mitandao kuwa nimenyang’annywa gari sio kweli. wakati naendesha Noah watu kimya, Lexus hakuna aliyesema nimenyang’anywa, inakuaje X6? Kuna ajabu gani mimi kuendesha X6? Wanawake tusijishushe kuonekana vitu fulani hatuwezi kumiliki”“Nasikitika sana kusikia watu wanavumisha maneno kama hayo. Hivi inakuaje mtu unanyang’anywa gari yako mwenyewe? Nina kila uthibitisho wa kuonesha hii X6 ni yangu na hakuna atakayeweza kuninyang’anya” – J Wolper

TWANGA KUSUGUA KISIGINO NA WAREMBO MISS DAR INTERCOLLEGE, CLUB BILICANAS KESHO

Na Mwandishi Wetu
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss dar Intercollege 2012 jumatano ya keshjo wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo msanii wa bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "twanga Pepeta' kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila jumatano katika klabu hiyo.
Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao.
"Warembo wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga Pepeta hutumbhuiza kila Jumatano kupitia usiku wa Mwafrika, hivyo tunaoomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashuhudia kabla ya kuja tena Ijumaa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,"Alisema
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaoshiriki  wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Dinaismail(zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

MNYIKA ATIMULIWA BUNGENI LEO.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mhe. John Mnyika ametolewa nje ya bunge leo asubuhi na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake aliyosema kuwa Rais Kikwete ni dhaifu wakati alipotakiwa kufanya hivyo.
Mnyika alisema "Tumefika hapa kwa udhaifu wa raisi Kikwete, tumefika hapa kwa uzembe wa wabunge na upuuzi wa serikali ya CCM!!"
Mnyika ametolewa nje ya bunge wakati wabunge wakichangia mjadala wa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni. Mnyika atarudi bungeni kesho saa tatu asubuhi.

Monday, June 18, 2012

CHRIS WILDER KUIPA ZAWADI TANZANIA

Mmarekani Chris Wilder ataipa Tanzania zawadi ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika atakapokimbia kilometa 1 kwa kila mwaka wa uhusru wa Tanganyika/Tanzania. Hii ina maana atakimbia kilometa 50 kusheherekea uhuru wa Tanganyika uliotokean mwaka 1961. 
Chris wilder ni Physician Assistant kutoka Annapolis, Maryland Marekani na yuko hapa mjini Moshi kukimbia mbio za 22 za Mt. Kilimanjaro Marathon tarehe 24 Juni. Mbio hizi zitaanzia Moshi Klabu mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu. Kutakuwa na mbio za kilometa 42, Kilometa 21, Kilometa 10 na Kilometa 5.
 Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na mama Marie Frances anayetoka katika mji wa Bethesda Marekani mwaka 1991 katika mji wa Moshi baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za Marathon ili kuitangaza Tanzania. Kila mwaka jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita mbio za Mount Kilimanjaro marathon zimekuwa zinafanyika. 
Kwa kutambua mchango wake katika kuutangaza mji wa Moshi tangu mwaka 1991, Manispaa ya Moshi ilimzawadia Marie Frances barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard. Aidha Frances alipewa funguo za Manispaa na kufanywa mkazi wa kudumu wa Manispaa ya Moshi katika shereke zilizofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Moshi mwaka 2009.
Mbio za mwaka huu za Mt. Kilimanjaro marathon zitapambwa na mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz anayewasili mjini Moshi tarehe 21 mwezi huu tayari kushiriki kwenye mbio hizi maarufu. Miss Lorenz ameshiriki kwenye sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight na nyingine nyingi.
Chris Wilde ni mkimbiaji wa mbio za marathon za Ultra Marathon na mwaka jana alikimbia kilometa 100. Kwa kukimbia kwake kilometa 50 na kuizawadia Tanzania Wilde ataweka historia ya mtu aliyekuja kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia kilometa 50 kama zawadi ya nchi hii tukufu.

Saturday, June 16, 2012

WAREMBO MISS DAR INTER COLLEGE WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

Warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la MIss Dar Intercollege 2012 wakiangalia magari aliyowahi kutumia  baba wa Taifa Hayati Julius K.Nyerere tangu zamani mpaka kufariki kwake ambapo magari hayo yapo katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.Ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo yao kabla ya shindano hilo litakalofanyika JUNI 22 katika ukumbi huo.
Warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la MIss Dar Intercollege 2012 wakiangalia samaki aina ya Silikanti "KISUKUKU' ambaye mara ya mwishop kuonekana ilikuwa  mwaka 1965 kabla ya kuonekana tena mwaka 2003 katika kisiwa kimoja huko KILWA, .Ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo yao kabla ya shindano hilo litakalofanyika JUNI 22 katika ukumbi huo.
Warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la MIss Dar Intercollege 2012 wakiangalia simba ambaye alionekana miaka ya nyuma .Ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo yao kabla ya shindano hilo litakalofanyika JUNI 22 katika ukumbi huo.

Warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la MIss Dar Intercollege 2012 wakiangalia banda la wanyama katika makumbusho ya Taifa KILWA, .Ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo yao kabla ya shindano hilo litakalofanyika JUNI 22 katika ukumbi huo.