b..

B1

Wynem

animation

Monday, June 18, 2012

CHRIS WILDER KUIPA ZAWADI TANZANIA

Mmarekani Chris Wilder ataipa Tanzania zawadi ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika atakapokimbia kilometa 1 kwa kila mwaka wa uhusru wa Tanganyika/Tanzania. Hii ina maana atakimbia kilometa 50 kusheherekea uhuru wa Tanganyika uliotokean mwaka 1961. 
Chris wilder ni Physician Assistant kutoka Annapolis, Maryland Marekani na yuko hapa mjini Moshi kukimbia mbio za 22 za Mt. Kilimanjaro Marathon tarehe 24 Juni. Mbio hizi zitaanzia Moshi Klabu mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu. Kutakuwa na mbio za kilometa 42, Kilometa 21, Kilometa 10 na Kilometa 5.
 Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na mama Marie Frances anayetoka katika mji wa Bethesda Marekani mwaka 1991 katika mji wa Moshi baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za Marathon ili kuitangaza Tanzania. Kila mwaka jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita mbio za Mount Kilimanjaro marathon zimekuwa zinafanyika. 
Kwa kutambua mchango wake katika kuutangaza mji wa Moshi tangu mwaka 1991, Manispaa ya Moshi ilimzawadia Marie Frances barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard. Aidha Frances alipewa funguo za Manispaa na kufanywa mkazi wa kudumu wa Manispaa ya Moshi katika shereke zilizofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Moshi mwaka 2009.
Mbio za mwaka huu za Mt. Kilimanjaro marathon zitapambwa na mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz anayewasili mjini Moshi tarehe 21 mwezi huu tayari kushiriki kwenye mbio hizi maarufu. Miss Lorenz ameshiriki kwenye sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight na nyingine nyingi.
Chris Wilde ni mkimbiaji wa mbio za marathon za Ultra Marathon na mwaka jana alikimbia kilometa 100. Kwa kukimbia kwake kilometa 50 na kuizawadia Tanzania Wilde ataweka historia ya mtu aliyekuja kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia kilometa 50 kama zawadi ya nchi hii tukufu.

No comments:

Post a Comment