Saturday, June 9, 2012

DULLY AMTULIZA MWANA FA.

Mwana FA
Na Herieth Makwetta
BAADA ya kufanya kazi katika studio mbalimbali kubwa hapa nchini na kutengeneza kazi zake nyingi zilizompa umaarufu, hatimaye Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ametua Dhahabu Records.
FA amesema sasa yupo tayari kurudi kwa mara nyingine akiwa ameongozana na swahiba na mkongwe mwenzake Ambwene Yesaya AY huku Dully Sykes naye akitia mkono wake katika wimbo huo.
Ikiwa ni mara nyingine kwa wawili hao kukutana tangu mwaka 2008 walipotoa albamu ya pamoja Habari Ndio Hiyo, FA ambaye alikuwa chimbo akiandaa kazi yake mpya itakayoitwa 'Ameen' ambayo inafanyika chini ya   studio ya Dhahabu Records, inayomilikiwa na Mr Misifa.
"Mashabiki wananijua nini nafanya nikiingia studio, hivyo wakae mkao wa kula tu kusubiri nini nitawaangushi, desturi yangu huwa sikisii nimeshamaliza kurekodi na siku yoyote wategemee kuwa naangusha mzigo redioni kwanza kabla ya kufanya video yake,
"Wimbo huu wa Ameen, nimemshirikisha Dully Sykes na AY, kwenye chorus wamesikika Dully akiimba Ameen Ameen halafu AY anamalizia Mungu Niongezee halafu anamalizia na kusema Nishike mkono niongezee kisha mimi nakamalizia verse zote mbili ambapo wimbo una Dakika 4:19" alisema. Hiyo ni nyingine tena!!!!
Bofya hapa chini kwa kuusikilizana kudownload wimbo huo 4 promo only.

No comments:

Post a Comment