Saturday, July 30, 2011

NANDERA: NAKUJA KUTAKE OVER

Yeeeeeeha! kama kawa kama dawa mtoto wakitaa, Benjamini wa mambojambo kwa pamoja wanamleta kwenu msanii wa kike anaekuja kutake over! sio mwingine basi ni huyu hapa! Sio mwingine bali na NANDERA! kaeni tayari!

Wednesday, July 27, 2011

MILLIONAIRE PARTY

Come and Dance with us in dic show

Anyone anaweza kushinda 1,000,000 tsh akinunuwa ticket ya kingilio kwenye event hapoo mbalamwezi, ticket 10,000 tsh.
Host wa event ni: Witness na CBH.
International Dj from france will be performing. DJ Mark and Team will be performing and other top Dj'z will be featured.
Celebrities and Bongo Flava Artists featured ni: Special guest Miss Tanzania, Moracka, Witness, CBH, Nas3 and many more will be giving interview, signature on Cd's and T-shirts etc.
Beach Games and activities zitakuwepo.
Live streaming of Ms.Ilala itakuwaa inaonyeshwa pale pale.

Ezekiel Wenje(Mbunge wa Mwanza Mjini - Chadema) Atolewa Bungeni

  
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa upinzani baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.  
  
Pamoja na kusepa lakini Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) aliendelea kula nae sahani moja.   
  
Pamoja na kusepa lakini Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) aliendelea kula nae sahani moja.   
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge baada ya kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
 
Mbunge wa Ilemela kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ezekiel Wenje ametolewa nje ya Bunge katika leo Mjini Dodoma.Mheshimiwa Wenje ametolewa nje ya bunge na Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba ambaye ndiye anayeongoza kikao hicho, baada ya kuvuana huku akihoji kuwa mwenyekiti huyo anaongoza kwa kuwaburuza wabunge.
Wakati Wenje akiwasha kipaza sauti kuzungumza tayari kulikuwa na mabishano yakiendelea kati ya Mbunge Moses Machali (NCCR-Magezi Kasulu Mjini) aliyekuwa akihoji muda mfupi aliokuwa amepewa mbunge wa CHADEMA, Tindu Lisu kuthibitisha kauli yake ambayo alidai mmoja wa mawaziri wenye dhamana na kodi amelidanganya bunge katika majibu yake.
Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo ya Wenje baada ya kutolewa nje anasema mbali na mabishano hayo alitaka kutoa taarifa ya uwepo wa taarifa za kuingia kwa samaki wa sumu nchini jambo ambalo ni hatari kwa wananchi.
Kitendo cha kutolewa kwa Mbunge Wenje bungeni hakikuwapendeza wabunge wa CHADEMA hivyo nao kutoka nje ya Bunge na Kuzungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi huku bunge likiendelea bila ya wao kuwepo Bunge linaendela na Kikao Chake Jioni Hii

Friday, July 22, 2011

WATEULE TOUR IN SOUTH AFRICA with Dj Choka

Show zinaanza rasmi Jumamosi hii ya tarehe 23 pale Joburg halafu Jumapili ya tarehe 24 tutaelekea Pretoria, baada ya hapo wiki ijayo Jumamosi ya tarehe 30 tutakuwa Cape Town kwenye Vunja Jungu na kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Tunawakaribisha watanzania wote pamoja na marafiki zetu wa huku huku South kuja kuona show nzuri kutoka bongo.

Thursday, July 21, 2011

TOTO ZE BINGWA NA SHARAMA WAZUNGUMZIA UZINDUZI WA ALBAMU ZAO UTAKAOFANYIKA JULY 23

Totoo ze Bingwa akiongea na waandishi wa habari asubuhi ya leo katika ukumbi wa habari maelezo, kushoto ni msanii Sharama kutoka nchini Kenya
Rapa wa bendi ya akudo impact Totoo Ze Bingwa (katikati) akiongea na waandishi wa habari katika ukubi wa habari maelezo leo asubuhi alipokuwa akizungumzia uzinduzi wa albam yake ya Hii Mambo haieleweki utakaofanyika siku ya jumamosi tarehe 23/07/2011. Kushoto ni msanii kutoka Kenya naefahamika kwa jina la Sharama ambae nae pia siku hiyo atazindua albamu yake ya VUNJA WINGA na kulia ni msanii Lai K kutoka kundi la Ukoo Flani maumau ambao watasindikiza uzinduzi huo.

EXCLUSIVE: NAPE AMPONGEZA ROSTAM AZIZ KUJIUZULU

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliyasema hayo wakati akiongea na baadti ya waandishi wa habari wa Mbeya katika ukumbi wa Hotel ya Paradise amesema Chama hakina la kusema, lakini kikubwa ni kuwa amefanya jambo jema, kwa kuitikia wito wa Chama, uamuzi ambao ni mzuri na wa busara," alisema Nape. Kuhusu mkutano wa hadhara wa mjini Mbeya, Nape alisema unalenga kuwaelezea wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla, juu ya mabadiliko ya uongozi ndani ya Chama, msingi wake ili waweze kuelewa, CCM imetoka wapi, ipo wapi na inakwenda wapi,
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza kwa makini KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye

SHARAMA: NIMEKUJA BONGO KUWASHIKA

Sharama
Msanii mkali wa hip hop kutoka nchini Kenya Ramadhani chambo anaejulikana kwa jina la Sharama amesema ameamua kuja kufanya uzinduzi wa albamu yake ya vunja winga hapa Tanzania kutokana na kuona ana mashabiki wengi hapa nchini halaf hawajapata kile wanachostahili kutoka kwake

Akizungumza na mwandishi wetu Sharama alikuwa na haya ya kusema “unajua nilikaa na kuona kuwa watanzania ni miongoni mwa mashabiki wangu na ninawapenda sana ndio maana nimeamua kiuja kuwapa kile wanachokihitaji kutoka kwangu”

Sharama ambae kwa sasa yupo hapa bongo akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kutoka katika lile kundi la Ukoo Flani Maumau wote kwa pamoja wakiwa wamepiga kambi pale katika studio za Mzuka Record wakipata madini tofauti kutoka kwa mtu mzima Benjamini wa mambojambo

Aliendelea sharama kwa kuwaomba mashabiki wake wote kuhudhuria kwa wingi pale Diamond jubilee siku ya tarehe 23/07 ambapo ndipo atakuwa akizindua albamu yake ya VUNJA WINGA. “mimi ninachowaomba mashabiki wangu wa Tanzania ni kuibuka kwa wingi pale Diamond ili kuona nimewaandalia nini kama zawadi yao maana nina imani kuwa kuna kitu kikubwa mashabiki wangu wanakihitaji kutoka kwangu hivyo na mimi nitawapa siku hiyo”

Sharama pia ameishukuru taasisi isiyo ya kiserikali ya Art In Tanzania kwa kuwezesha mpango mzima wa uzinduzi wake.

Katika uzinduzi huu pia kutakuwa na uzinduzi wa albamu ya HAIELEWEKI yak wake Totoo ze bingwa ambao nao kwa kiasi kikubwa umewezeshwa na kuletwa kwenu na Art In Tanzania

Katika shoo hii watu wazima hawa watasindikizwa na kundi zima la ukoo flani maumau, Abasi kutoka nchini Kenya na kutoka tanzanina watakuwepo 20%, Benjamini wa mambojambo, Zolla D, Sana asana Band na bendi ya Akudo Impact.

Monday, July 18, 2011

MWANAUME KAZINI.............................

THT ARTISTS JOIN USHER RAYMOND IN ATLANTA

Usher's New Look Foundation, established in 1999 has invited THT artists to join him at the World Leadership Conference and Awards in Atlanta this week.
Mwasiti, Amini, Barnaba, Linah, Ditto & Keyboard player Mose Delema will be flying to the United States to join him at the World Conference where they will perform on stage with one of their most popular icons Usher Reymond.
Usher’s team has invited the THT Artists to participate in a 4-day conference that includes sharing experiences, discussing local, national and global issues, working together in an international choir featuring a solo performance by Usher as well as performing their own songs during the Awards Night.
Traveling with Ruge Mutahaba the Founder of Tanzania House of Talent and B12 popular Radio DJ from Clouds Fm, Ruge Mutahaba says ‘The artists have been given an amazing opportunity to travel to Atlanta to participate not only with an international artist for the Awards Night but to also contribute and learn by participating in the youth conference.’
B12 said ‘It’s great to see first hand how Usher Reymond is celebrating youth’s involvement in leadership. He is keen to demonstrate how young talent, education and public service can make a difference and I will be following the conference and giving updates regularly on Clouds FM.’ 
 

Thursday, July 14, 2011

One, Nikki Mbishi, Stereo, Fid Q - Classic *Download for Promo ONLY*

Huu ni wimbo mpya kutoka kwa wasanii hao unaowaona kwenye picha, usikilize halafu unipe maoni yako

ALEX KAJUMULO AJIBU TUHUHUMA ZA KUONDOKA BONGO HARAKA HARAKA.

Alex KLajumulo akiwa na mmoja wa wachezaji wa mpira wa kikapu
 
OK NIMEULIZWA SANA MASWALI KWA NINI SIKUKAA SANA TANZANIA? NI KWA SABABU KILA SUMMER NINAYO KAZI YA KUWAFUNDI SHA BAADHI YA NBA PLAYER JINSI YA KUTUMIA MIGUU KAMA WACHEZAJI MPIRA WA MIGUU KWA SABABU HAWAJUI SANA KUTUMIA MIGUU NAFUNDISHA WACHEZAJI WA NANE 8 NBA WAKATI WA LIKIZO ZAO KWA SABABU WANATAKA KUA KAMA KHAKIMU OLWAJA ALIYE KUA ANACHEZEA HOUSTON. HUYU NI MMOJA WA WACHEZAJI NINAYE MFUDISHA NA KANIRUHUSU NITUMIE PICHA YAKE KWA HIYO KAMA PIA KUNA MCHEZAJI YEYOTE ANATAKA KUSAIDIWA NAWEZA NI KAMSAIDIA ,  UKIJUA KUTUMIA MIGUU VIZURI UNAWEZA KUCHEZA MICHEZO YOYOTE ILE. THENKXX ONE LOVE IS LAW
BY ALEX KAJUMULO NA KWENYE MAISHA YANGU NINA BAHATI YA KUJUA MENGI THENKX.

DONT MISS DA SHOW OF ALBUM LOUNCH (HAIELEWEKI) OF TOTOO ZE BINGWA

CHEKI NA HII AFU TUONEEEEE

TOTO ZE BINGWA KUZINDUA ALBAM YA MAMBO HAIELEWEKI JULY 23

 
Art in Tanzania Mzuka Records Album Launch - New albums of Totoo ze Bingwa and Sharamaa (Kenya), also 20%, Benjamin Mambo Jambo, Sanaa Sanaa Band, Zola D, Richie Rich, Akudo Impact Band and others. This is an event not to miss. Diamond Jubilee 23rd July 2011. Tickets available at numerous sales points in town.

Monday, July 11, 2011

MESEJI KUTOKA KWA SUGU - MBUNGE WA MBEYA MJINI

Jana tarehe 8 Julai 2011 Polisi walinikamata kwa kile walichokiita kuwa ni kufanya mkutano bila kibali.Hata hivyo, mtiririko wa matukio unaonyesha kwamba polisi walisukumwa na sababu nyingine kwa kuwa suala la taarifa kupelekwa polisi kama sheria zinavyohitaji lilishashughulikiwa na viongozi wa CHADEMA mkoa na wilaya ya Mbeya Mjini.
Leo tarehe 9 Julai 2011 pamoja na kutolewa kwa dhamana polisi wameonyesha nia ya kutaka kuzuia tamasha la wazi la bure ( ‘Burudani Nyumbani’) ambalo wasanii mbalimbali walikuwa walifanye kwa mwito wangu kwa ajili ya kutoa burudani na kuhamasisha maendeleo. Polisi wameonyesha vitendo vya kutaka leo kufanyike tamasha la fiesta pekee wakati ambapo matamasha haya yote mawili yameandaliwa na wadau tofauti katika maeneo tofauti.
Mpaka wakati huu ninapotoa taarifa hii wananchi wengi wamejikusanya katika uwanja wa Ruanda Nzovwe ambao ni maarufu kama Uwanja wa Dr Slaa wakisubiri tamasha hilo lakini polisi wameonyesha dhamira ya kutaka kuwatawanya.
Maneno na vitendo vya Jeshi la Polisi vinaelekea kuwa na uhusiano na kauli ambayo niliitoa hivi karibuni kupitia mtandao wa Facebook ya kutohitaji tamasha la Fiesta kufanyika Mbeya.Katika mazingira haya ni muhimu nikaeleza tu kuwa kauli yangu kuhusu Fiesta ilikuwa na madhumuni ya kuanzisha mjadala kuhusiana na suala zima la wizi na unyonyaji uliopo kwenye Sanaa, ambao sio tu unawanyima haki Wasanii, bali pia kukosesha mapato kwa Serikali ambayo yangetokana na kodi kupitia Sanaa ikiwemo muziki.
Nilifanya hivyo baada ya tamasha hilo kutangazwa kufanyika katika eneo ambalo wananchi wamenipa wajibu wa uongozi wa kuwatumikia na kuwawakilisha. Hivyo kwa niaba ya wananchi wa Mbeya Mjini wanaokosa mapato katika sanaa na wasanii wa Mbeya wanaokosa fursa kutokana na vikwazo nilichukua uamuzi wa kuwakilisha kupaza sauti kama ambavyo nimekuwa nikipaza sauti katika masuala mengine yanayogusa umma kama viwanda, kilimo, barabara za Mbeya Mjini na Haki za wanafunzi wa Elimu ya Juu pamoja na makundi mengine katika jamii.
Niliamua kupaza sauti katika hili kupitia Fiesta, kwa kuwa waandaji wake kimsingi ni sehemu ya vyanzo vya maovu kwenye maendeleo ya muziki hapa nchini. Fiesta ikiwa kitovu cha uonezi kwani hata Wasanii wanaoshiriki halipwi ipasavyo au hawalipwi kabisa. Na hii ni kutokana na wao kutumia njia haramu kuhodhi (monopolise)biashara ya muziki hapa nchini, huku wakiwanyima nafasi watanzania wengi kutumia vipaji na ubunifu wao kwenye biashara ya muziki.Waandaji wa Fiesta ndio wenye redio ya Clouds, Kampuni ya promotion ya Primetime, na pia wanahusika na N.G.O ya THT, waandaji wa matamasha ya injili, ikiwemo kuwa na ushirika katika Tamasha la Pasaka.Huku wakiwa na ushawishi wa hila kwenye Kili Music Awards (One Call Promotion) na mambo mengine yote muhimu yanayohusu Sanaa. Ikiwemo ujumbe wa bodi kwenye Tamasha la majahazi, Zanzibar. Lisingekuwa jambo baya kama wangetumia nafasi hizo kwa haki na maendeleo ya sanaa.

Kutokana na haya, kwa miaka mingi himaya (“empire”) hii imetumia nafasi yake dhalimu kukandamiza watu wengine hasa Wasanii. Kwa mfano kama Msanii hayupo kwenye hiyo “himaya” yao basi hana nafasi ya kutimiza ndoto yake. Na iwapo Msanii hakubaliani na taratibu zao au malipo finyu wanayowalipa Wasanii, basi watahakikisha wanampiga vita na hatimaye kuhujumu usanii wake ili atoweke, kwa kuwa tu hakubaliani nao. Msanii hana haki ya kufanya majadiliano ya kibiashara mbele yao. “Empire” hii imehodhi mpaka makampuni ya udhamini hapa nchini, ambapo makampuni haya yamekuwa magumu kutoa udhamini kwa wadau wengine kwa kuwa tu wao ni washirika wa “Empire” hii.
Walifikia hatua ya kuhodhi mpaka biashara ya usambazaji kwa “Wadosi” ambapo bila ya wao kuruhusu basi Msanii yeyote kazi yake haipewi nafasi ya kusambazwa wala kusikika. Hata kama nyimbo au album yake ni nzuri kwa kiasi gani.Kibaya zaidi wamehodhi mpaka nia njema ya Rais Kikwete katika kusaidia Sanaa na Wasanii. Mfano ni Studio ambayo Rais kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii wa Tanzania, lakini baadaye tukashangaa kusikia ipo mkononi! Pia Rais aliahidi na kutoa nyumba ya Serikali kwa Wasanii ambayo ingetumika kuendeshea Studio husika, lakini nyumba hiyo ya Serikali iliyotolewa na Rais sasa iko chini yao na ndio makao ya THT! Wamefanikiwa kumhadaa Rais kuwa wao ndio “Care takers” wa Sanaa ya Tanzania akawaamini na wao wanaitumia vibaya imani njema ya Rais kwao kufanya dhuluma.

Yote niliyoyataja juu, japokuwa hayo ni kwa uchache tu! Yanalalamikiwa sana na wasanii wengi na wadau hapa nchini, japokuwa wengi wameshindwa kujitokeza waziwazi kutoka na vitisho vya watu hawa. Vitendo hivyo wanavyofanya vimeleta madhara katika tasnia ya sanaa na matokeo yake ni kudumaa kwa maendeleo ya muziki hapa nchini. Vijana wengi wanaojihusisha na sanaa wamepoteza matumaini. Wengi walipata tegemeo la ajira kupitia muziki, lakini hali haipo hivyo tena. Vijana wengi wasanii wamekata tamaa kwa ajili ya ukandamizaji wa “empire” hii.
Na sio tu wasanii na wadau wengine wanawapoteza katika hili. Kwa watu hawa kuhodhi na kuvuruga kabisa biashara ya muziki, hata Serikali inapoteza fedha nyingi kupitia kodi. Kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Jehovaness Aikaeli ambaye ni mchumi wa UDSM, hata katika hali hii mbaya ya biashara ya muziki, Serikali imepoteza Tsh. Milioni 18, kwa kutokusanya kodi kupitia muziki tu, ukiachilia mbali filamu na sanaa nyingine. Na iwapo hali itaboreshwa basi kodi hiyo itapanda mpaka wastani wa Tshs. Bilioni 50 kwa mwaka! Hizi sio pesa kidogo kwaserikali, hasa ukizingatia bajeti ya Wizara inayohusika na Utamadnuni ni Tsh bilioni 14, kwa mwaka, fedha ambazo mara nyingi hawapewi zote kutokana na Serikali kutokuwa na fedha ya kutosha! Lakini hapa utaona kukwa kodi ya mwaka peke yake ingetosha kwa bajeti ya Wizara na ziada kubwa ingebaki kwa miradi ya maendeleo kama kujenga Art Theatres n.k
Napenda ieleweke wazi kwamba mimi binafsi ni “Mhanga” au “victim” wa uharamia wa “himaya” hii kwa miaka mingi, tukupitia migogoro kadhaa ya kibiashara lakini kilichonisikuma kuchukua hatua hii; sio nafsi yangu pekee bali wajibu nilionao hivi sasa kama mwakilishi umma.Izingatiwe kuwa baada ya mimi kuchaguliwa kuwa Mbunge na wananchi wa Mbeya tena kwa kishindo, Serikali kupitia Wizara inayohusika na utamaduni na pia Baraza la Sanaa (BASATA), walinipongeza kwa barua huku wakinitaka niendelee na harakati za kupigania sanaa na wasanii kwa kutumia nafsi au jukwaa langu jipya Bungeni na nje ya Bunge. Jukumu ambalo nililikubali kwa mikono miwili kwani harakati za muziki huu si kitu kipya kwangu, ulianza kabla ya Ubunge na ndio ninachokifanya na hasa ukizingatia mimi pia sasa ni Waziri Kivuli (Shadow Minister) wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Kwa lugha nyingine ujumbe nilioutoa wa kukataa Fiesta ni ishara ya mgomo wenye nia ya kutuma ujumbe wa madai ya msingi. Na historia inaonyesha kuwa, Wasanii wa Nigeria walianza kulipwa vizuri kama wanavyolipwa sasa baada ya kuanzisha migomo dhidi ya mapromota wanyonyaji wa nchini kwao.Na kama ni suala la kukuza uchumi na ajira, Ni nini mchango wa Fiesta na matamasha mengine kwa halmashauri za mji na majiji wanayopita na kuvuna mamilioni ya fedha kila siku?
Wenu katika kutaka haki,
Joseph Mbilinyi (Mb)
9/7/2011-Mbeya Mjini

HAPA JHIKO MAN PALE AFRICABISA BAND (DONT MISS DA SHOW

Thursday, July 7, 2011

WAREMBO WA REDDS MISS TEMEKE, ILALA NA KINONDONI KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI WA HABARI WA KIKE KWENYE SIKU YA MICHEZO.

Muaandaaji wa Redd's Miss Kinondoni Bw Boi George, akizungimza na vyombo vya habari
Dar es Salaam, July 6th  2011:
 Warembo wa Redds Miss Temeke, Ilala na Kinondoni  wanatarajia kushiriki kwenye siku ya michezo itakayojumuisha mechi za kirafiki kati ya warembo wa kanda hizi  za Dar es Salaam pamoja na wanahabari wa kike kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original ni wafadhili wakuu wa mashindano ya urembo ya kanda za Dar es Salaam yajulikanayo kama Redds Miss Temeke, Redds Miss  Ilala na Redds Miss Kinondoni.
  Bw. Jackson Kalikumtima Mwaandaji wa Redd's Miss Ilala
 
Akiwa anaongea na waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kuzindua siku hii ya michezo ya warembo wa kanda za Dar es Salaam meneja masoko wa kampuni ya TBL Bwana Fimbo Butallah alisema “Redds imeshiriki ipasavyo kwenye mashindano ya urembo ya mwaka huu ikiwa ni mtiririko ulioanza miaka kadhaa iliyopita. Tasnia ya urembo ina mchango mkubwa kwenye jamii yetu sio tu kwa upande wa burudani bali inawapatia nafasi warembo mbalimbali Tanzania kukuza vipaji vyao na kuweka msingi ambao wakijipanga vizuri utawajenga na kuwaletea mafanikio mbalimbali kweye maisha yao. Kwa kuzingatia hilo TBL kupitia kinywaji chake cha Redds imejikita sambaba na mashindano haya na imefadhili zaidi ya vitongoji na kanda 35. Kanda za Dar es Salaam ambazo Redds ni mdhamini mkuu zitakuwa na heka heka mbali mbali kama ambavyo mtaanza kushuhudia tukianza na siku ya michezo itakayojumuisha kanda tatu ambazo ni Temeke, Ilala na Kinondoni’’. Bwana Butallah aliendelea kusema kuwa “siku hiyo itajumuisha michezo kama kandanda, mpira wa mikono, mashindano ya kukimbia nk. ambapo warembo watawashirikisha waandishi wa habari wa kike kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili kuongeza vionjo na kuleta msisimko zaidi. Tunaamini kuwa michezo ni njia nzuri ya kujenga mahusiano baina ya warembo wenyewe na ina burudani ya kipekee kabisa”
Vicky Kimaro kutoka Mwananchi communication akiongea kwa niaba ya waandashi wa habari wa kike
Michezo hiyo itafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 9, mwezi huu wa saba kwenye ufukwe wa mbalamwezi ulioko old bagamoyo road.
Na mwanadada Vicky Kimaro kutoka Mwananchi Communication akiongea kwa niaba ya wanahabari wa kike watakaoshiriki na warembo kwenye siku hii ya michezo alisema ‘Kwanza ningependa kutoa pongezi za kipekee kwa Redds  na waandaaji wa mashindano haya ya kanda Ben Kisaka, Jackson Kalikumtima na Boy George kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye kuboresha mashindano ya urembo nchini. Tuna msisimko mkubwa sana kuhusu siku hii ya michezo ambayo tunatarajia itakuwa na ushindani wa kirafiki. Tukiwa kama wana habari wa kike tuna matumaini makubwa na warembo wetu kwa ujumla kwamba wao ndio viongozi wa taifa letu la kesho. Mashindano haya yatatuweka karibu na warembo hawa wa kanda na kutupa nafasi ya kipekee ya kuburudika na michezo mbalimbali. Tunafurahia nafasi hii ambayo tutaishiriki kikamilifu”.
Redd’s Original imekuwa mstari wa mbele kwa miaka mingi kufadhili mashindano ya Miss Tanzania na imetoa mchango mkubwa kuhakikisha kuwa mashindano haya yanaboreshwa kadri miaka inavyoendelea na imefanikisha kwa kiasi kikubwa sana kunyanyua tasnia ya urembo nchini.

Sunday, July 3, 2011

Miss Tourism walitembelea Bunge Mjini Dodoma 01-07-2011

Hawa ndio warembo wa miss Tourism wakiwa katika picha za pamoja walipotembelea bunge la bajeti mjini DODOMA juzi.
Kiongozi kutoka kamati ya miss Tourism DIMO DEBWE mbaye aliongozana nao