Thursday, July 21, 2011

SHARAMA: NIMEKUJA BONGO KUWASHIKA

Sharama
Msanii mkali wa hip hop kutoka nchini Kenya Ramadhani chambo anaejulikana kwa jina la Sharama amesema ameamua kuja kufanya uzinduzi wa albamu yake ya vunja winga hapa Tanzania kutokana na kuona ana mashabiki wengi hapa nchini halaf hawajapata kile wanachostahili kutoka kwake

Akizungumza na mwandishi wetu Sharama alikuwa na haya ya kusema “unajua nilikaa na kuona kuwa watanzania ni miongoni mwa mashabiki wangu na ninawapenda sana ndio maana nimeamua kiuja kuwapa kile wanachokihitaji kutoka kwangu”

Sharama ambae kwa sasa yupo hapa bongo akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kutoka katika lile kundi la Ukoo Flani Maumau wote kwa pamoja wakiwa wamepiga kambi pale katika studio za Mzuka Record wakipata madini tofauti kutoka kwa mtu mzima Benjamini wa mambojambo

Aliendelea sharama kwa kuwaomba mashabiki wake wote kuhudhuria kwa wingi pale Diamond jubilee siku ya tarehe 23/07 ambapo ndipo atakuwa akizindua albamu yake ya VUNJA WINGA. “mimi ninachowaomba mashabiki wangu wa Tanzania ni kuibuka kwa wingi pale Diamond ili kuona nimewaandalia nini kama zawadi yao maana nina imani kuwa kuna kitu kikubwa mashabiki wangu wanakihitaji kutoka kwangu hivyo na mimi nitawapa siku hiyo”

Sharama pia ameishukuru taasisi isiyo ya kiserikali ya Art In Tanzania kwa kuwezesha mpango mzima wa uzinduzi wake.

Katika uzinduzi huu pia kutakuwa na uzinduzi wa albamu ya HAIELEWEKI yak wake Totoo ze bingwa ambao nao kwa kiasi kikubwa umewezeshwa na kuletwa kwenu na Art In Tanzania

Katika shoo hii watu wazima hawa watasindikizwa na kundi zima la ukoo flani maumau, Abasi kutoka nchini Kenya na kutoka tanzanina watakuwepo 20%, Benjamini wa mambojambo, Zolla D, Sana asana Band na bendi ya Akudo Impact.

No comments:

Post a Comment