Thursday, July 7, 2011

WAREMBO WA REDDS MISS TEMEKE, ILALA NA KINONDONI KUSHIRIKIANA NA WAANDISHI WA HABARI WA KIKE KWENYE SIKU YA MICHEZO.

Muaandaaji wa Redd's Miss Kinondoni Bw Boi George, akizungimza na vyombo vya habari
Dar es Salaam, July 6th  2011:
 Warembo wa Redds Miss Temeke, Ilala na Kinondoni  wanatarajia kushiriki kwenye siku ya michezo itakayojumuisha mechi za kirafiki kati ya warembo wa kanda hizi  za Dar es Salaam pamoja na wanahabari wa kike kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original ni wafadhili wakuu wa mashindano ya urembo ya kanda za Dar es Salaam yajulikanayo kama Redds Miss Temeke, Redds Miss  Ilala na Redds Miss Kinondoni.
  Bw. Jackson Kalikumtima Mwaandaji wa Redd's Miss Ilala
 
Akiwa anaongea na waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kuzindua siku hii ya michezo ya warembo wa kanda za Dar es Salaam meneja masoko wa kampuni ya TBL Bwana Fimbo Butallah alisema “Redds imeshiriki ipasavyo kwenye mashindano ya urembo ya mwaka huu ikiwa ni mtiririko ulioanza miaka kadhaa iliyopita. Tasnia ya urembo ina mchango mkubwa kwenye jamii yetu sio tu kwa upande wa burudani bali inawapatia nafasi warembo mbalimbali Tanzania kukuza vipaji vyao na kuweka msingi ambao wakijipanga vizuri utawajenga na kuwaletea mafanikio mbalimbali kweye maisha yao. Kwa kuzingatia hilo TBL kupitia kinywaji chake cha Redds imejikita sambaba na mashindano haya na imefadhili zaidi ya vitongoji na kanda 35. Kanda za Dar es Salaam ambazo Redds ni mdhamini mkuu zitakuwa na heka heka mbali mbali kama ambavyo mtaanza kushuhudia tukianza na siku ya michezo itakayojumuisha kanda tatu ambazo ni Temeke, Ilala na Kinondoni’’. Bwana Butallah aliendelea kusema kuwa “siku hiyo itajumuisha michezo kama kandanda, mpira wa mikono, mashindano ya kukimbia nk. ambapo warembo watawashirikisha waandishi wa habari wa kike kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili kuongeza vionjo na kuleta msisimko zaidi. Tunaamini kuwa michezo ni njia nzuri ya kujenga mahusiano baina ya warembo wenyewe na ina burudani ya kipekee kabisa”
Vicky Kimaro kutoka Mwananchi communication akiongea kwa niaba ya waandashi wa habari wa kike
Michezo hiyo itafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 9, mwezi huu wa saba kwenye ufukwe wa mbalamwezi ulioko old bagamoyo road.
Na mwanadada Vicky Kimaro kutoka Mwananchi Communication akiongea kwa niaba ya wanahabari wa kike watakaoshiriki na warembo kwenye siku hii ya michezo alisema ‘Kwanza ningependa kutoa pongezi za kipekee kwa Redds  na waandaaji wa mashindano haya ya kanda Ben Kisaka, Jackson Kalikumtima na Boy George kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye kuboresha mashindano ya urembo nchini. Tuna msisimko mkubwa sana kuhusu siku hii ya michezo ambayo tunatarajia itakuwa na ushindani wa kirafiki. Tukiwa kama wana habari wa kike tuna matumaini makubwa na warembo wetu kwa ujumla kwamba wao ndio viongozi wa taifa letu la kesho. Mashindano haya yatatuweka karibu na warembo hawa wa kanda na kutupa nafasi ya kipekee ya kuburudika na michezo mbalimbali. Tunafurahia nafasi hii ambayo tutaishiriki kikamilifu”.
Redd’s Original imekuwa mstari wa mbele kwa miaka mingi kufadhili mashindano ya Miss Tanzania na imetoa mchango mkubwa kuhakikisha kuwa mashindano haya yanaboreshwa kadri miaka inavyoendelea na imefanikisha kwa kiasi kikubwa sana kunyanyua tasnia ya urembo nchini.

No comments:

Post a Comment