Monday, August 25, 2014

MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI YAENDELEA VIWANJA VYA MASHUJAA MJINI DODOMA

Baadhi ya akina mama wakiwa wanaangalia moja ya bidhaa za katika mabanda ya wajasiriamali hao yanayoendelea hivi sasa.

Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo (Kulia) akipata maelezo ya moja ya banda linaloonyesha na kuuza bidhaa zake  za madishi na vifaa vya umeme, kwenye maonesho ya biashara za wajasiriamali yanayoendelea katika viwanja vya Mashujaa, mjini Dodoma.
Baadhi ya wateja wakichagua moja ya bidhaa za dvd na cd zinazouzwa kwenye mabanda hayo.

Na Andrew Chale, Dodoma.
MAONESHO ya wafanyabiashara kipindi cha Bunge la Maalum la Katiba yanaendelea kwa kasi mjini hapa na kuwakutanisha wajasiriamali zaidi ya 100 katika viwanja vya Mashujaa.
Akizungumza Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo, alisema lengo kuu la maonesho hayo ni kutoa fursa kwao kuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.
“Mpaka sasa tuna wajasiriamali 100,  ambao wanaendelea na maonesho  yao kwenye viwanja hivi vya Mashujaa kuanzia Agosti 10 mwaka huu, na maonesho yataendelea mpaka litakapomalizika Bunge la Katiba, hivyo bado tunaendelea kupokea wajasiliamari wengine zaidi,” alisema Dk. Kifimbo.
Alisema kuwa maonesho hayo yanajumuisha wauzaji wa bidhaa za tiba mbadala, bidhaa za majumbani, kazi za mikono kutoka ndani na bidhaa zingine mbalimbali.
Kifimbo ambaye ni mganga wa tiba mbadala alisema maonesho hayo yatazinduliwa rasmi Agosti 21, mwaka huu, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki.
Lengo ya maonyesho ni kutoa fursa kwakuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.

Thursday, August 14, 2014

MAZISHI YA MAMA TUNDA (MKE WA MSANII AFANDE SELE) YAMEFANYIKA LEO MJINI MOROGORO

UO
Professor Jay amesafiri hadi mkoani Morogoro kwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa msanii mwenzake Afande Sele.

xxxxxx

Kupitia Instagram, Professor ameshare picha akiwa kwenye mazishi na kuandika: Msibani Morogoro nyumbani kwao marehemu Asha au mama Tunda sasa hivi… tunajiandaa kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele saa kumi jioni ya leo, bwana alitoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe….Amen
Awali Afande Sele alisema kifo cha Mama Tunda kimetokana na uzembe wa madaktari. Mama Tunda alifariki baada ya kulazwa kutokana na kuugua Malaria. Akizungumzia tukio hilo, Afande alidai kuwa bila uzembe wa madaktari huenda malaria isingechukua uhai wa Mama Tunda.
“Mama Tunda ametuachia pengo kubwa sana kwenye familia,” alisema Afande. “Amefariki jana saa tano usiku katika hospitali kubwa hapa Morogoro kutokana na uzembe wa madaktari. Walimpa matibabu akarudi nyumbani, sitaki kulizungumzia kiundani kwa sasa hivi kwa sababu tupo kwenye wakati mgumu. Huku mazishi yatafanyika kuanzia kama saa tisa hivi lakini bado hatutajua itakuwa wapi bado tupo kwenye mipango. Malaria ilimchukua sana, kwa familia na watoto kwetu ni msiba mkubwa sana, yaani ni huzuni sana,” aliongeza.

Wednesday, August 13, 2014

NILIJITOA MAISHA YANGU KWENYE MUVI YA MSHALE WA KIFO - AISHA BUI


Na Mwandishi Wetu
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Asha Bui, amedai kuwa alijitoa maisha yake kutoka na filamu yake ya Mshale wa Kifo, kutokana na sinema hiyo kutengeneza porini katika msitu hatari wenye wanyama wakali.
Msanii huyo amedai alifanya hivyo kufuatia maoni ya wapenzi wa filamu ambao kila siku wanalalamika kwa kusema kuwa filamu zetu nyingi zimekuwa za mijini tu, huku baadhi ya matukio yakirudiwa kila katika sinema hizo jambo ambalo limekuwa likiongelewa mara kwa mara.
“Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, lakini najua na deni kwa wapenzi wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila mwaka,”anasema Aisha .
Filamu ya Mshale wa Kifo Imetengenezwa na Yuneda Entertainment na imewashirikisha wasanii nyota kama Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Aisha Bui, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ na wasanii wengine 

Monday, August 11, 2014

(Audio) Wille - Uze Mbela

Cheki na hii link kusikiliza na kupakua wimbo huu 

PSPF YAFUNGA NANENANE LINDI KWA KISHINDO

AFISA UHUSIANO MFUKO WA PESHENI WA PSPF, COLETA MNYAMANI AKITOA MAELEZO YA NAMNA YA KUJAZA FOMU YA UCHANGIAJI WA HIARI MOHAMED MUSSAALITPOTEMBELEA BANDA LA PSPF KWENYE MAONYESHO YA NANENANE MKOANI LINDI MWISHONI MWA WIKI
 BALOZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF, MRISHO MPOTO “MJOMBA”AKITOA BURUDANI KWA WAKAZI WA MKOA WA LINDI WALIOTEMBELEA BANDA LA PSPF WAKATI WA MAONYESHO YA NANENANE
BAADHI YA WANANCHI WA MKOA WA LINDI WAKIWA KATIBA BANDA LA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAKISHUHUDIA BURUDANI KUTOKA MJOMBA BAND

Sunday, August 10, 2014

MABONDIA MANENO OSWARD NA ABDALLA PAZI WAPIMA UZITO KUZIPIGA KESHO JUMAPILI MWANANYAMALA CCM MWIJUMA
Bondia Juma Biglee akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake kesho

 Bondia Abdallah Pazi akipima uzito kushoto ni Maneno Osward

Mabondia Maneno Osward kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumapili katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala jijini Dar es salaam picha zote na WWW.SUPESDBOXINGCOACH.BLOGSPOT.COM

Friday, August 1, 2014

'AUDIO' CHUGA EMCEEZ FT ft BOU NAKO - CHAFF YA PAFF

Inline image 1
Bofya HAPA kudowload ngoma ya Chuga Emceez wakimshirikisha BouNako ngoma ni HipHop Category kwa jina la "Chaff ya Paff"