Wednesday, August 13, 2014

NILIJITOA MAISHA YANGU KWENYE MUVI YA MSHALE WA KIFO - AISHA BUI


Na Mwandishi Wetu
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Asha Bui, amedai kuwa alijitoa maisha yake kutoka na filamu yake ya Mshale wa Kifo, kutokana na sinema hiyo kutengeneza porini katika msitu hatari wenye wanyama wakali.
Msanii huyo amedai alifanya hivyo kufuatia maoni ya wapenzi wa filamu ambao kila siku wanalalamika kwa kusema kuwa filamu zetu nyingi zimekuwa za mijini tu, huku baadhi ya matukio yakirudiwa kila katika sinema hizo jambo ambalo limekuwa likiongelewa mara kwa mara.
“Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, lakini najua na deni kwa wapenzi wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila mwaka,”anasema Aisha .
Filamu ya Mshale wa Kifo Imetengenezwa na Yuneda Entertainment na imewashirikisha wasanii nyota kama Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Aisha Bui, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ na wasanii wengine 

No comments:

Post a Comment