Friday, November 13, 2015

MABONDIA HAMISI MWAKINYO NA MESHACK MWANKEMWA KUPIGANA KESHO JUMAMOSI


Promota Shomari Kimbau akiwainua mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho


Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau akiwa na mkanda utakaogombaniwa Picha na SUPER D BOXING NESWNA Mwandishi Wetu

MABONDIA Meshack Mwankemwa na Hamisi Mwakinyo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 66 unaotambuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchi mkanda uho uliokuwa umeachwa wazi na bondia Selemani Zogo kwa kuto utetea kwa wakati sasa utapiganiwa na mabondia hawo kesho
akizungumza wakati wa upimaji wa uzito promota wa mpambano uho Shomari Kimbau amesema mkanda uho utapiganiwa na mabondia hawo ili apatikane bingwa mpya wa uzito wa kg 66
mpambano uho utasimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini chini ya rais wake Chauremba Palasa aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na ngumi za utangulizi za mabondia mbalimbali
Said Mayanga atamenyana na Gido Selemani wakati Mohamed Amir atapambana na Hemed Hemed
na mpambano mwingine wa kusisimua utakuwa ni wa akina mama ambapo bondia mnaschachali Asha Nzowa 'Asha Ngedere' atapambana na Joyce Awino ambambao ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wanawake wa mchezo wa masumbwi.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akiwakumbusha baadhi ya sheria zitakazo tumika katika mchezo wa ngumi utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Dar es salaam

Sunday, November 1, 2015

WIZ KID AFUNIKA LEADERS CLUB

Msanii kutoka Nigeria, Wiz Kid Akifanya mambo jukwaani kwenye viwanja vya Leaders Club.
Msanii kutoka Nigeria, Wiz Kid Akifanya mambo jukwaani kwenye viwanja vya Leaders Club.
Msanii kutoka Nigeria, Wiz Kid akiimba huku akiwa nyuma ya jukwaa ikiwa ni muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani. 
Msanii Fid Q akiwaburudisa mashabiki wa muziki waliohudhuria tamasha la Wiz Kid, msanii kutoka Nigeria
Msanii Christian Bella kaifanya yake jukwaani.
Msanii wa Filamu nchini, Ray Kigosi akimtunza msanii Christian Bella alivyokua akiimba katika tamasha la Wiz Kid jana.
Msanii Diamond Akiwapa burudani wakazi jiji la Dar na mashabiki wake katika shoo ya Wiz Kid iliyofanyika kwenye viwanja vya Leader Club. 
Sehemu ya mashabiki wa muziki waliohudhuria tamasha la Wiz Kid, msanii kutoka Nigeria
Mc wa Tamasha na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha EATV, Sam Missago akifanya yake
Dj Sinyoritha.
Dj Sinyoritha akiwa na mgeni wake kwenye Mashine