b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, November 19, 2014

MDAU ANDREW CHALE KUTOA VITABU VYA MAISHA YAKE

Andrew Chale (kulia) akiteta jambo na 'Mwenyekiti'  Maggid Mjengwa wa Mjengwa Blog.
================================

Na Mwandishi Wetu
Mwandishi wa Habari nchini Tanzania, Andrew Chale anayeandikia magazeti ya Tanzania Daima na Sayari yanayotolewa na kampuni ya Free Media ya jijini Dar es Salaam, ambaye pia mwandishi 'msaada' wa blog za habari mbalimbali za hapa nchini na nje ya Tanzania ameanza mchakato rasmi wa kuandika vitabu  vitatu (3) vitakavyokuwa vikielezea juu ya Maisha yake.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Novemba 19,  Andrew Chale alibainisha juu ya kusudio hilo  la kutoa Vitabu  vya kuelezea Maisha yake ni ndoto aliyonayo kwa miaka mingi na kwa sasa imetimia.
"Wengi watajiuliza sasa nimepata wapi ujasiri wa kufanya jambo hili kubwa la kuelezea Maisha yangu?.Ni rahisi sana, Unapokuwa na Mungu kila jambo linawezekana hivyo vitabu hivi vitakuwa ni muongozo kwa Vijana wote hapa Duniani kuelewa kuwa yale yote wanayopitia si ya kuyakatia tamaa, bali kuangalia wapi wataweza kujikomboa na hata kuendana na hali iliyopo kwa kujithamini, kujielewa, uvumilivu na kufikia malengo stahiki ya maisha" alifafanua Andrew Chale.
Alivitaja vitabu hivyo kuwa ni: "Who Is Andrew Chale?" Sehemu ya Kwanza), 'Who Is Andrew Chale 2?"- 'Nimnukuu Nani?' (Sehemu ya Pili)  na Kitabu cha mwisho kitakachojulikana kama "Mimi ni Historia".
Akifafanua vitabu hivyo vya 'Who Is Andrew Chale' cha kwanza na kile cha pili cha 'Who Is Andrew Chale 2- 'Nimnukuu Nani?', alibainisha kuwa vitaelezea kwa kina Historia yake tokea kuzaliwa hadi alipofikia sasa huku cha Pili cha 'Who Is Andrew Chale 2-'Nimnukuu Nani' kikielezea yale mambo yote yaliyojificha nyuma ya pazia na ukakasi wa maisha aliyopambana nayo kutoka kwa walimwengu na mwishowe anauliza "Nimnukuu Nani?".

Aidha, kwa upande wa kitabu cha : "Mimi ni Historia" ameweza kuelezea ujumbe juu ya Vijana kutokata tamaa na baadala yake wasonge mbele kwa magumu yote waliyopitia, ikiwemo yeye.
"Mimi ni Historia", mimi mwenyewe naogopa sana, kwanza kuanzia jina la Kitabu, Nakumbuka nilimuuliza Mama yangu Mzazi juu ya jambo fulani la kifamilia baina yake na Baba,  lakini jibu alilonipa ndilo lililonifanya nishike neno hili 'Mimi ni Historia'. Kikubwa kwenye kitabu hichi nitafafanua mambo mbalimbali ya kihistoria  bila shaka hata atakayesoma ambaye alipitia mambo kama yangu naye itakuwa ni Historia" alimalizia Andrew Chale.
Vitabu hivyo vyote vitajaa Historia ya kweli, itakayotoa mafunzo kwa kila mmoja atakayebahatika kuvisoma Pia vitakuwa ni kama mafunzo, mfano wa kuigwa, na kukuacha ki mdomo wazi na hata kububujikwa machozi.
Aidha, Andrew Chale, aliomba ushirikiano kwa wadau kujitokeza kumsapoti ilikufanikisha juhudi za vitabu hivyo ikiwemo gharama za kuandaa Mswada, mapitio na uchapaji.
"Kwa sasa nipo katika andalio la Simulizi, na lengo kuu nije nichapishe Mkuki na Nyota.Kwa sasa natafuta watu watakao kuwa msaada wa awali wa kufanikisha dhumuni langu hili Ikiwemo ushahuri, msaada wa kifedha, mchango wa kimawazo na mengineo. Tuwasiliane kupitia 0719076376 au 0767076376 au 0688076376 au chalefamily@yahoo.com" alimalizia Andrew Chale.
Andrew Chale, ambaye kwa sasa anaishi Bagamoyo, Mkoani Pwani akifanya shughuli zake hizo za Uandishi wa Habari, Pia ni Mwanaharakati wa Haki za Watoto nchini, msanii wa masuala ya Vichekesho, Mtunzi wa filamu, maigizo na mshahuri kwenye matamasha ya sanaa na Muziki, mbali hayo pia ni Mjasiriamali katika Sanaa na Utamaduni ikiwemo kukuza Sanaa na Utamaduni kwa Mkoa wa Pwani.

BASATA NA KITUO CHA UTAMADUNI CHA UJERUMAN (GOETH INSTITUT) WAENDESHA MAFUNZO KWA WASANII WA SANAA ZA MIKONO

Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza (Kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa batiki yaliyoanza mapema wiki hii kwenye Ofisi za Baraza hilo zilizoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni  Bi. Leah Ruhimbi

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla akiongea na Wasanii (hawako pichani) waliohudhuria kwenye mafunzo ya wiki moja ya utengenezaji batiki yanayoandaliwa na kituo chake kwa kushirikiana na BASATA na kufanyika makao makuu ya BASATA. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi akifungua mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi yanayofanyika kwa wiki moja makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba. Wengine kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua akiwaelekeza jambo wasanii wanaoshiriki mafunzo ya utengenezaji batiki 
Sehemu ya Wasanii wa utengenezaji batiki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
=======================================

Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ujeruman maarufu kama Goeth Insitut wameendesha mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za mikono yanayofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanayotazamiwa kudumu kwa siku tano yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa yanalenga kuongeza ubunifu na weledi miongoni mwa wasanii wa Sanaa za mikono ili kuongeza ubora na tija katika uzalishaji.  
Mapema akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Leah Ruhimbi alisema kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija kwa wasanii hao na kuwawezesha kubuni Sanaa zenye ubora zitakazopenya masoko mbalimbali ya Sanaa.
“Ni matarajio ya BASATA na wizara kwamba mafunzo haya yatakuwa yenye tija kwa wasanii na yatawawezesha kusambaza ubunifu na uzoefu kwa wasanii wengine nchini. Lengo ni kuwa na sanaa zenye ubunifu na ubora” alisisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Goeth Institut Bi. Eleonore Sylla alisema kwamba mafunzo hayo yanahusisha wasanii wenye uwezo wa kutengeneza batiki na lengo kuu ni kuwaweka pamoja ili wachangie uzoefu na baadaye kutengeneza batiki zenye ubora zaidi.
“Tunajua mnatoka sehemu mbalimbali nchini na wote mna uzoefu katika utengenezaji wa batiki lakini kuwa kwenu pamoja kwenye mafunzo haya kutawafanya mpate uzoefu zaidi na hatimaye kubuni batiki zenye ubora” aliongeza Sylla.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba BASATA kwa kushirikiana na Goeth Insitut wameona kwamba kuna haja ya mafunzo hayo ya wasanii na kwamba baraza litaendelea kuboresha ubora wa kazi za Wasanii kupitia kuwajengea uwezo.


Sunday, November 2, 2014

MABONDIA WAZIPIGA MAZOEZINI WAKISIMAMIWA NA KOCHA SUPER D

Bondia Shabani Kaoneka kulia
akimtupia konde  Obago Kamata wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na Super D Boxing Coach Dar es salaam

Bondia Shabani Kaoneka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Obago Kamata wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na Super D Boxing Coach Dar es salaam
Bondia Jumaa Rashid akioneshana ubavu na Juma Biglee wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya uhuru uwanja wa basket yaliyokuwa yakisimamiwa na Super D Boxing Coach Dar es salaam.
Bodia Obaga Kamata kushoto akipambana na Idrisa Mweta wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na Super D Boxing Coach
Bondia Omari Bai kushoto akipambana ya Kelvin Majiba wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa basket shule ya uhuru yaliyokuwa yakisimamiwa na Super D bOXING coach Dar es salaam juzi.
Picha zote na SUPER D BLOG