Tuesday, May 28, 2013

BREAKING NEWS!!!!!!!: MSANII ALBERT MANGWEA (Ngwair) AFARIKI DUNIA NCHINI AFRIKA YA KUSINI

#BREAKING: Msanii ALBERT MANGWEA (Ngwair), amefariki dunia leo akiwa Afrika Kusini, rafiki anasema hakuamka toka jana alipolala. #R.I.P

Tuesday, May 21, 2013

PROF. JAY AINGIA RSMI KWENYE SIASA, ACHUKUA KADI YA UANACHAMA YA CHADEMA

Mtu mzima Joseph Haulea a.k.a Prof. Jay 'Jzze' the havy weight MC, ameamua kuingia rasmi kwenye siasa baada ya kuchukua kadi ya chama ya CHADEMA. 
Prof. Jay amekabidhiwa kadi hiyo leo na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu'.

TUNDU LISSU, ANNE KILANGO NUSURA WAZICHAPE NJE YA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMABaada ya Bunge kuahirishwa jana, nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri baina ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.
Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu.
Maneno hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia Lissu.

Monday, May 20, 2013

MH. MSIGWA ALIPOFIKISHWA MAHAKAMANI LEO ASUBUHI


Uilinzi uliimarishwa mahakamani hapo

Mchngaji Msigwa akishuka kutoka kwenye gari la polisi

Umati na wafuasi wa Mchungaji Msigwa wakiwa nje ya mahakama

TASWA FC YACHAKAZA TIMU YA MABONDIA JANA


Bonia Daudi Muhuzi akishindana na Mbuyu wa timu ya TASWA FC Majuto Omari wakati wa mpambano wao

Mchezaji wa timu ya Taswa akipambana na bondia kuwania mpira

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akitoa maelekezo kuhuzu mchezo huo walipocheza timu ya mpira ya mabondia na TASWA FC.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, May 12, 2013

KUMBUKUMBU YA BOB MARLEY ' BOB MARLE DAY' NDANI VIWANJA VYA POSTA

RUGE AOMBA KUKUTANISHWA NA JAY DEE


MKURUGENZI wa Kampuni ya Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema yu tayari kukutana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla aliyejitolea kuleta suluhu kati yake na nyota wa kike wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee', limeandika gazeti la Mtanzania.
Mutahaba ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu Waziri Makalla atamke kuwa yu tayari kuingilia kati mvutano uliopo baina ya msanii huyo na Ruge kwa kuwaita kuzungumza nao kwa maslahi ya wahusika na tasnia ya muziki nchini.“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita, kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize pande zote mbili, hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amezungumza mengi,” alisema.
Wakati huohuo, Ruge ameongeza kwamba tayari ameshachukua taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungua jalada polisi la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee.“Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni dogo na la mzaha, lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka,” anasema Ruge.Mwanzoni mwa mwezi huu, Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na blog yake kuwa inamuhujumu kimuziki, kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumla, tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.


Monday, May 6, 2013

JANUARY MAKAMBA AWAPONDA CLOUDS KWA KUTOPIGA BONGO FLEVA

Huenda mjadala kuhusu uamuzi wa kituo cha radio cha Clouds FM, leo kutopiga Bongo Flava siku nzima haujalikuna sikio la naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Kupitia Twitter, Makamba ameandika kuwa Tanzania ina matatizo matatizo mengi ya kujadili kuliko nyimbo za kuchagua kucheza redioni. “We’ve got much bigger problems than radio playlists, ” ametweet.
Katika mahojiano maalum leo kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alidai kuwa ametoa amri leo kituo chake kisicheze Bongo Flava.
Uamuzi huo leo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

RUGE AMJIBU JIDE KUPITIA POWER BREAKFAST LEO.

Sikiliza alichokisema ruge leo asubuhi.

Friday, May 3, 2013

GADNER ALONGA JUU YA BIFU LA JAYDEE NA RUGE / KUSAGA (CLOUDS)

Kutokana na bifu linaloendelea kati ya msanii Lady Jay Dee na Radio ya Clouds fm, Gadna G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki huyo maarufu ameibuka na kuzungumzia yale yanayofahamika kuwa  ni wosia wa msanii huyo.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yaliyokuwa majibu ya maswali aliyoulizwa na presenter wa kipindi hicho.

  
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?
Gadna G: Ni maneno  ambayo yametoka moyoni mwake na  ni maneno  mbayo anajitetea kama msanii,  mimi kama Meneja ukiacha pia kama  mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport  na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba  watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.

Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati  ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.

Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie  naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama  lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia  kulekule ambapo yeye alipo

Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna G
: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale  pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia  akaona kama unafaidi, mwisho  akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.

Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?
Gadna G:
 Cha kushukuru Mungu ni  kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategemea umma wa Watanzania au  hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.

Jay Dee anapata saport nzuri kutoka kwa Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake.

 Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.

Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa. 

Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....

Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G:
 Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli  anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho  ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na  kusikia ukweli  ili kama wanakosea wasiendelee kukosea  wabadilikee….

Wednesday, May 1, 2013

JAMBO SQUAD - TUKUNYEMA (OFFICIAL VIDEO)

JAY DEE: HUU NI WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige mawe Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

JIDE