Tuesday, June 30, 2015

WASANII WAOMBA MSAMAHA WA KODI VIFAA VYA MUZIKI

Inline image
Msanii G Nako kutoka Kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi akiimba sambamba na msanii mchanga ambaye hakufahamika mara moja kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.
--------xxxxxxxxxxxx----------


Na Mwandishi Wetu

Baadhi ya wasanii nchini wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Fedha kufikiria kupunguza au kufuta kabisa ushuru wa forodha unaotozwa kwenye vifaa vya muziki wanavyoagiza kutoka nje ili kukuza Sanaa na kusaidia mamilioni ya vijana ambao wamejiajiri kupitia sekta hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wasanii mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mmoja wa wasanii anayeunda kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi Nick wa Pili alisema kwamba, kwa sasa sekta hiyo ni kimbilio la ajira kwa vijana wengi kwa hiyo Serikali haina budi kupunguza kodi kwa zana mbalimbali zinazotumiwa na wasanii ili kurahisisha uzalishaji, kukuza tija na uchumi.
“Wasanii wengi kwa sasa wanakwenda kufanya video na kutengeneza muziki nje ya nchi. Hii inatokana na teknolojia yetu kuwa chini ya wenzetu. Naamini Serikali ikipunguza kodi katika vifaa hivi na kuwawezesha wataalam tulionao basi nchi zote jirani zitakimbilia kwetu” alisema Nick
Aliongeza kwamba vipaji vya wasanii vipo vingi lakini kutokana na uzalishaji duni wa kazi za muziki na hata filamu wasanii wamejikuta wakishindwa kushindana ipasavyo nje ya nchi na mara nyingi kutumia gharama kubwa katika kufuata teknolojia hizo za juu nchi za nje na hivyo kuikosesha serikali mapato.
“Wasanii wanakwenda kulipa zaidi ya milioni arobaini kwa video moja tu nje ya nchi, hizi fedha zinakwenda kukuza uchumi wa nchi zingine. Naamini kama Serikali ikijenga mazingira mazuri ya kiteknolojia na zaidi kushusha gharama hizi basi nchi yetu itafaidika zaidi na Sanaa” alizidi kusisitiza Nick.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mitaji na Misaada kwa wasanii kutoka BASATA Bi. Elineca Ndowo alisema kwamba sekta ya Sanaa nchini inazidi kukua na hivyo lazima wasanii nao wafikirie kufanya kazi kisasa na kwa kufuata taratibu zote ili kuipa serikali uhakika katika kupanga kulingana na hali halisi.
“Sekta ya Sanaa inakua, lazima tuisaidie Serikali kuipa takwimu sahihi na moja ya njia ya kuhakikisha hili ni kwa wasanii kujisajili, kusajili kazi zao na kuhakikisha taarifa sahihi na kwa wakati zinapatikana. Hili litarahisisha upangaji wa mipango” alisema Bi. Ndowo.
Jukwaa la Sanaa la BASATA ni programu ambayo hufanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu na hutumika kama jamvi la kuwaelimisha wasanii na kuwakutanisha kwa pamoja katika kubadilishana uzoefu na mawazo kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo sekta yao.


Inline image
Msanii anayechipukia kwenye tasnia ya filamu kutoka taasisi ya mafunzo ya TAMAP akiwauliza maswali mbalimbali wasanii wa kundi la Weusi kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.

Inline image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kundi la Weusi Nick wa Pili (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayofanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake ni wasanii wanaounda kundi hilo John Simon aka Joh Makini na G Nako na Afisa kutoka BASATA Bi. Elineca Ndowo

Inline image
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu hiyo ya Jukwaa la Sanaa ya BASATA.

Inline image
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mitaji na Misaada kwa wasanii kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi. Elineca Ndowo (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) kuhusu masuala mbalimbali kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo huandaliwa kwa mwezi mara mbili ziku ya Jumatatu na Baraza hilo. Wengine katika picha kulia kwake ni Wasanii G Nako na John Simon maarufu kama Joh Makini wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi.

Sunday, June 28, 2015

JANUARY MAKAMBA AMALIZA KAZI ARUSHA MJINI, WANANCHI WAMFAGILIA KWA HOTUBA NA MIPANGO YAKE, WAMTAKIA USHINDI MNENE

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akisalimiana na wananchi na wananchama wa CCM mkoa wa Arusha waliojitokeza katika viwanja vya ofisi za CCM mkoa kumuunga mkono katika harakati zake za kusaka wadhamini mkoani hapo. January amejizolea wadhamini 2227 kutoka mkoa huo.

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya katibu wa CCM mkoa wa arusha mara baada ya kuwasili mkoani hapo kwa ajili ya kuomba udhamini wa wanachama wa CCM utakaomuwezesha  kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM. Ambapo mkoani Manyara amepata wadhamini 2227. Kushoto ni mke wake, Ramona Makamba.

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akiwapungia mkono wananchi na wananchama wa CCM mkoa wa Arusha alipokuwa akiingia ukumbini kuhutubia na kuomba udhamini wa wanachama hao ili kupata ridhaa ya chama kuteuliwa na chama kugombea nafasi ya urais. Mbele kabisa na katibu wa CCM arusha Mjini, Feruzy Bano

Katibu wa CCM arusha Mjini, Feruzy Bano akimkabidhi mh January Makamba fomu yenye majina na sahihi za wanachama wa CCM waliomdhamini katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Arusha. January amepata wadhamini 2227.
Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akionyesha  fomu yenye majina na sahihi za wanachama wa CCM waliomdhamini katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Arusha. January amepata wadhamini 2227.

Mh January Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM mkoani Arusha waliojitokeza katika Ukumbi wa ndani wa CCM mkoa wa Arusha. January yupo katika ziara yake ya kusaka wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM. Ambapo mkoani Manyara amepata wadhamini 2227.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Arusha wakiwa wanafuatilia hutuba ya mh January Makamba  nje ya ukumbi wa CCM mkoa kupitia Runinga maalumu zilizokuwa nje ya ukumbi huo, Januray alihutubia wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Arusha ambapo alipata wadhamini 2237 kwa mkoa huo.

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi wa jiji la Arusha kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Arusha jana. Picha zote na Mpigapicha wetu.

Saturday, June 27, 2015

JUMA NATURE AWAASA WASANII WANAOUTAKA UONGOZI WA KISIASA


Dar es Salaam. Msanii Juma Nature, ametoa rai kwa wasanii waliotangaza nia kuwania viti mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao, akiwataka kusimama kwenye misingi ya kusaidia jamii badala na si vinginevyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nature ambaye mapema mwaka huu alifuta msimamo wake wa kutaka kugombea ubunge Jimbo la Temeke alioutangaza miaka mitatu iliyopita, alisema kwamba ni vyema wasanii wanaosaka nafasi za kisiasa kuzingatia watakayotakiwa kufanya kwa mujibu wa nafasi hizo za uwakilishi.
Nature alisema ni muhimu kufuata matakwa ya wananchi watakaowaongoza na kuacha kuweka mbele tamaa ya fedha kwa kuwa hayo siyo malengo ya uongozi wa kijamii bali huduma kwa wananchi.
“Kama wanaingia kwa ajili ya kwenda kwenye ubunge ni sawa, kwani wao ni watunzi wazuri wa zamani na uandishi wao upo kwenye jamii, lakini wasiende wakifikiria uongozi kuwa sehemu ya kujipatia fedha. Wawe karibu na wananchi watakaowaongoza kwa sababu hiyo ndiyo iliyo chini yao na inawategemea,” alisema Nature.
Kwa mujibu wa Nature ameamua kukaa pembeni kwa muda kutokana na utitiri wa wasanii walioweka wazi dhamira zao za kujiingiza katika siasa mwaka huu.
Alisema wazo hilo alilokuwa nalo muda mrefu, ameamua kujipa muda hadi ifikapo mwaka 2020 ili kuwaacha waliotangaza nia sasa kuendeleza mchakato huo.
“Mwenyezi Mungu akipenda ni tagombea mwaka 2020, nimeamua kwa mwaka huu niache mambo haya kwanza. Sasa nina kazi nyingi. Pili wasanii wengi wameshajitokeza, inatosha sana. Tusubiri tuone kwamba watafanya nini, ndipo na sisi tutaona nini tunafanya,” alisema Nature akiongeza kuwa kwa sasa yupo katika matengenezo ya video ya “Inaniuma Sana Remix” aliyomshirikisha Msaga Sumu.

Friday, June 26, 2015

NGOMA MPYA YA MCHIZI MOX FT J'DEAL - SIMBA BADO ANAWINDA

Bofya HAPA https://mkito.com/song/simba-bado-anawinda/14830 kupakua wimbo wa Mchizi Moxie akimshirikisha "J Deal" Wimbo kwa Jina "Simba Bado Anawinda" ikiwa ni HipHop Category Toka @noizmekah chini ya @defxtro powered by @vmgafrica

Thursday, June 25, 2015

MR. BLUE AIPA KISOGO MIHADARATI

Anaitwa Khery Sameer aka Lil Sama...wengi tunamjua kwa jina la Mr.Blue ingawa jina hili hakujipa yeye,Ni jina lililozaliwa baada ya single yake ya Blue Blue kufanya vizuri na watu kuamua kumpachika jina hilo.
Wakati anatoka alikua akishindanishwa na Joselin mkali mwingine ambaye style yao ya kuchana ilikua ikiwachanganya mashabiki wengi mpaka @princedullysykes alipoamua kuwaweka pamoja kwenye wimbo wa DHAHABU.
Zaidi ya miaka 12 Blue amedhihirisha ukali wake kwa kuwaacha mbali watu aliokuwa akishirikiana nao kwa kipindi kile akiwemo Abbyskils.
Blue ni miongoni mwa wasanii wachache wenye bahati ya kuliteka jukwaa hata bila ya kuwa na single mpya na mashabiki wakampokea na kumshangilia,ana mfululizo wa single kadhaa zilizompa mafanikio ikiwemo single ya PESA aliyoitoa mwaka 2013.
Leo tunamsherehekea kwa maamuzi mazito aliyoamua kuyatangaza na kuyaweka wazi wiki chache zilizopita maamuzi ya kuamua kuacha kutumia Mihadarati yote aliyowahi kutumia kipindi cha nyuma.
Blue ameishukuru Familia yake ambayo ni mkewe na mtoto wake kwa nguvu yao kubwa iliyosababisha aache kutumia vilevi hivyo.
Hiko ni kwa uchache kutoka kwa super star wetu wa Tanzania @mrbluebyser1988 @mrbluebyser1988 ipi sifa nyingine ya Blue unayoifahamu?? #‎kuzamuzikitanzania #kuzamuzikitanzania c


NGOMA MPYA YA G HOOD -GOOD LIF (NOIZ)

Inline image 1
Bofya HAPA https://mkito.com/song/good-life/14867 kupakua wimbo wa G-Hood kwa jina "Good Life" na kwa mawasilano/mahojiano zaidi check na G-Hood kwa nambari +255 769 141 893 powered by @vmgafric

JANUARI AITIKISA MISENYI KAGERA, AJIZOLEA WADHAMINI 8024

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akivishwa skafu na vijana chipukizi wa CCM wilaya ya Misenyi mara baada ya kuwasili wilayani hapo. Januari, jana alizungumza na wanachama na wananchi wa CCM wilaya ya Misenyi katika harakati ya kutafuta wadhamini wa ndani ya chama kwa ajili ya kupewa ridhaa na chama hicho kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM ambapo amepata wadhamini zaidi ya 8000.

Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakiwapungia mkono wananchi na wanachama wa CCM wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera mara walipowasili wilayani hapo kwa ajili ya kuomba udhamini kutoka kwa wanachama hao utakaomuwezesha kupata ridhaa ya chama kugombea nafasi ya urais wa Tanzania ambapo amejizolea wadhamini zaidi ya 8000.

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakisalimiana na wanchama wa CCM wilayani Misenyi moani Kagera mara baada ya kuwasili wilayani hapo.

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akionesha fomu ya udhamini alioupata wilayani Misenyi mkoa wa Kagera ambapo amejizolea kuoa 8024.

Mke wa january Makamba, Ramona Makamba akisalimia wanchi na wanachama wa CCM wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera wakati Mh january alipofika wilayni hapo kwa ajili kusaka ya kuomba udhamini kutoka kwa wanachama hao utakaomuwezesha kupata ridhaa ya chama kugombea nafasi ya urais wa Tanzania ambapo amejizolea wadhamini zaidi ya 8000.

Mh anuary Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera waliojitokeza katika Viwanja vya CCM Wilayani hapo . January yupo katika ziara yake ya kusaka wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM. Ambapo mkoani Sinyanga amejizolea wadhamini 8024 mkoa wa Kagera. Picha na Mpigapicha Wetu


Wednesday, June 24, 2015

WASAMBAZAJI WA FILAMU KUGOMA KULIPA KODI IFIKAPO JULAI 2015

Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa Filam TAnzania 'TAFDA' Moses Mwanyilu kushoto akionesho moja ya filamu  kwa wahandishi wa habari katika ukumbi wa Idara Habari Maelezo Dar es salaa  awapo pichana juu ya filamu ambazo zinauzwa kiolela bila ya kulipa kodi tena kwa galam nafuu kulinganisha na zao ambao wanalipa kodi kupitia mamlaka ya Mapato TRA  ambapo julay mosi wameazimia kuto peleka filamu zao bodi ya filamu na kutonunua stemp kwa ajili ya ulipaji wa kodi wa pili kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa chama hico Suleiman Ling'ande

Mjumbe wa Chama Cha Usambazaji wa Filamu nchini Saleh Abdallah kushoto akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani kuhusu filamu zilizojaa mtaani ambazo azijalipiwa kodi uku zikiachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote ile wakati wao filamu zao zinakaguliwa na Bodi pamoja na kulipa kodi katika mamlaka ya mapato TRA kulia ni Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa Filam TAnzania 'TAFDA' Moses MwanyiluNa Mwandishi Wetu
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu 

Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.

Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.

Tuesday, June 23, 2015

BONDIA WA KIKE, MWANNE HAJI AWATAKA MABONDIA DAR

Na Mwandishi Wetu 
BONDIA wa kike Mwanne Haji ambaye amejitokeza kupambana na mabondia kwa kike wa Dar es salaam baada ya kuwasumbua sana mabondia wenzake wanaotoka Chunya Mkoa wa Mbeya na sasa kujikita jijini akitokea katika GYM ya Zugo iliyopo Gongolamboto.
Bondia huyo wa kike ambaye ameshapanda ulingoni kupambana na baadhi ya mabondia wa mkoani, amesema amekuja kwa ajili ya mchezo wa masumbwi jijini. Hivyo mabondia wa kike wakae pembeni kwani sasa ata wasambaratisha mmoja baada ya mwingine alitolea mfano wa mabondia wanaotamba Dar es salaam kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe kila wakati ni Lulu Kayage, Halima Ramadhani, Fatuma Yazidu.
Sasa wakae foleni kwani atawapa vipigo mmoja baada ya mwingine bondia uyo mpaka sasa amecheza michezo mitatu ambapo mchezo wake wa kwanza alicheza na Vailet Modest na kufanikiwa kumtwanga kwa point mchezo wake wa pili alicheza na Telesia Kiwale na mchezo wake wa tatu alicheza na Jennifer Pius na kumsambalatisha kwa pointi.
Hivyo amewaomba mapromota wajitokeza kumsaidi kupambanishwa na mambondia aliowataja hapo juu kwa uzito wa kg 49.
Mbali na hivyo ametowa wito kwa tasisi mbalimbali pamoja na kmpuni kujitokeza kudhamini mchezo wa masumbwi kwani unapendwa na mashabiki lukuki nchini.


Super D Boxing Coach
 Mob;+255787 406938
        +255713 406938 
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

ILIVYOKUWA KWENYE ZIARA YA JANUARY MAKAMBA MKOANI SHINYANGA.

Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akisalimiana na kuzungumza jambo na mmoja wa wananchama wa CCM Mkoa wa Shinyanga alijitokeza kumdhamini. Ambapo mkoani Sinyanga amejizolea wadhamini 6228 ikiwa ni idadi ya Shinyanga Mjini na Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Mh January Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Shinyanga waliojitokeza katika Viwanja vya CCM Wilaya wa Shinyanga Mjini. January yupo katika ziara yake ya kusaka wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM. Ambapo mkoani Sinyanga amejizolea wadhamini 6228 ikiwa ni idadi ya Shinyanga Mjini na Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akionesha fomu ya udhamini iliyowekwa sahihi na na wanachama 6228 mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na katibu wa wilaya ya Shinyanga mjini.
Mbunge wa Shinyanga Mjini Steven Masele azungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM mkoa wa Shinyanga na kumkaribisha Mh January Makamba kuzungumza na wananchi hao waliojitokeza katika viwanja vya ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mbunge wa Bumbuli na naibu waziri wa mawasilano, sayansi na teknolojia, January Makamba akiteta jambo na mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele walipokuwa katika mkutano na wananchi pamoja na wanachama wa CCM mkoani Shinyanga. Mkutano huo ulifanyika katika viwanja vya CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mh. January Makamba akiweka sahihi kwenye vitabu vya wageni katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mh anuary Makamba akiwapungia mkono wananchi na wanachama wa CCM nje ya Ofisi ya Chama hicho wilayaya Shinyanga Mjini mara alipowasili kwa ajili ya kuomba udhamini kutoka kwa wanachama hao utakaomuwezesha kupata ridhaa ya chama kugombea nafasi ya urais wa Tanzania.
Baadhi ya waendesha Bodaboda waliojitokeza kumpokea Mh January Makambawakiwa kwenye msafara wa kuelekea katika viwanja vya CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. Ambapo mkoani Sinyanga amejizolea wadhamini 6228 ikiwa ni idadi ya Shinyanga Mjini na Wilaya ya Shinyanga Vijijini. Picha zote na Mpiga Picha wetu.

Sunday, June 21, 2015

HOTUBA YA NDUGU ADO NOVEMBA ATANGAZA NIA- UBUNGE (CCM) JIMBO LA IRINGA MJINI


Ndugu wananchi na wanahabari,  leo tarehe 21 Juni 2015 nimekuiteni kuwaeleza juu ya Nia yangu ya kugombea Ubunge Iringa Mjini kwa ticket ya CCM. Sababu ninayo Nia ninayo na uwezo ninao kwa wananchi wangu wa Iringa na Tanzania kwa ujumla. Natambua ya kua uongoZi ni Mzigo... Uongozi ni kipaji na uongoZi ni kubeba Majukumu ya kuwaongoza wengine na siyo Ubwana au Ubwanyenye Kama dhana hii inavyoharibiwa na wengi.

Ndugu wananchi na wanahabari, Uongozi ni Wito... Mimi nimezaliwa hospitali ya serikali ya Mkoa Iringa na kukulia  Frelimo kata ya Mivinjeni na nimekua Kiongozi tangu nikiwa Mtoto pale Sokoni Iringa Kanisa Kuu na baadae kuwa Kiranja Prefect nikiwa Wilolesi Shule ya Msingi Hali hiyo iliendelea nikawa Waziri Katika wizara mbali mbali miaka yote mitatu nilipokua Chuo Kikuu baada ya Kumaliza Masomo yangu ya Sheria CCM makao Makuu walinileta Iringa Kama Katibu wa Wilaya kazi ambayo nayo ilininoa vilivyo.

Ndugu wana Habari kazi hiyo haikuishia hapo... Katika kujifunza uongozi Mungu amenibariki kuwa Msaidizi wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Kama Mzee Makamba, George Mkuchika na Jaka Mwambi Mpaka baadae Mwenyekiti wa Chama Changu CCM aliporidhia kuanzishwa kwa taasisi ya wasomi yaani vyuo Vikuu ambapo nilipelekwa kuongoza na nikiwa huko niliweza kujenga takribani matawi yote ya vyuo Vikuu Nchi nzima kwa kuhakikisha wana kuwa na Uongozi na ofisi zao ushahidi ni hapa kwetu Iringa nilifungua matawi matatu na kujenga ofisi za Mkwawa na Tumaini. Nimepitia mafunzo mbali mbali ya Chama tangu mwaka 2006 Katika Chuo Kikuu cha CCM Ihemi na kufaulu kwa distinction jambo ambalo linanipa unyenyekevu kuwatumikia Wananchi wangu wa Iringa.                             
Ndugu wana wananchi na wanahabari, nimejiunga na CCM tar 31.12.1998 Tawi la Tandamti Frelimo kwa Balozi wangu Mzee Mlosi (Mungu amuweke mahala pema) hivyo ni karibu miaka 14 nipo ndani ya Chama Changu na ninaona ninayo haki na wajibu kuwaongoza wana Iringa wenzangu ambao najua changamoto zao zinazowakabili Katika Chama na Nje ya Chama.

Ndugu wananchi na wanahabari,  kwa kutumia uzoefu nilionao hapo juu vilevile Kama Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Rais wa WanamuZiki wa Injili Tanzania, Wakili (Advocate) na kada wa CCM Mume wa Mke Mmoja na watoto watatu, hii Kabisa  ni ishara kubwa kuwa ninao uwezo wa kupambana na changamoto za Iringa Mjini na Nchi yangu kwa Ujumla. 

Changamoto tulizonazo… 
Ndani ya Chama
…Bila kupepesa maneno natambua mpasuko uliopo na ambao umesababishwa na Viongozi wa juu wa Chama Wilayani na Mkoani hapa na wengine wamepewa nafasi za serikali lakini bado wamekipasua Chama kwa makundi hivyo mtu Pekee atakayeleta Umoja na mshikamano ni Mimi Addo November Mwasongwe ambaye sina kundi na nipo Tayari kuongoza watu wote, mtu wa watu Mpenda watu ambaye Nafahamu taratibu za Chama Changu ndio maana Mpaka leo sijafanya vurugu yeyote jimboni Kama wanavyofanya wenzangu ambao mnawajua.

…na mmewaona wakijipitisha kila kukicha. Mara Zote napata sana Faraja ninapokumbuka Kauli inayosema Kizuri Chajiuza Kibaya Chajitembeza Natambua changamoto ya ofisi bora za CCM na usafiri kwa kila Kata na Hilo nitalichukua Kama jukumu langu binafsi Kama mjumbe wa Kamati ya Siasa pale mtakaponipa ridhaa ya Ubunge. Natambua kuwa mafunzo ya uongozi tanatakiwa kuanzia ngazi za shina Mpaka Kata na Wilaya.

Changamoto za Wananchi 
 1. Miundo Mbinu na Umeme jambo hili litakua kipaumbele kuhakikisha maeneo yote yanafikika kwa Lami hii inaweZekana kwa kupata Mbunge safi ambae ni mie na madiwani safi
 2. Iringa kuwa kitovu cha Utalii Kama ilivyo Arusha... Wote tunatambua kuwa Mbuga ya Ruaha ndiyo kubwa kuliko Zote Duniani hivyo ni jukumu letu kuitangaza na  kuweka vivutio vya utalii Kama vile Mahoteli makubwa Tour Guide Offices jambo ambalo litakuza uchumi wa Iringa kwa kupitia Utalii na kutoa ajira kwa wana Iringa na wengine wengi.
 3. Kuwamilikisha wananchi wetu ardhi zao ili wasiweze kudhurumiwa lakini waweze kukopea inapobidi kwa maendeleo Yao.
 4. Kukuza Michezo na Sanaa kuwa na uwekezaji wenye tija wa Sanaa na Michezo jambo litakalotoa ajira ya kudumu na kukuza uchumi wetu.
 5. Matibabu ya uhakika kwa wazee  wanawake na wasiojiweza.
 6. Utawala bora na uwajibikaji.
 7. Wananchi kupata mikopo nafuu ya Nyumba.
 8. Kupiga Vita ukimwi na malaria.
 9. Kukuza Kilimo na kutafuta Masoko ya uhakika ya maZao yetu.
 10. Kukuza Elimu na kutoa Motisha kwa Vijana wetu walioko kuanzia Shule za Msingi na Sekondari ili tujipatie vijana wenye uwezo mkubwa kwa maendeleo ya Taifa na hili halitawezekana bila walimu bora wanaolipwa vizuri.
 11. Uongozi wa Vitendo.
 12. Kukuza Miundo Mbinu hasa usafiri wa Anga kwa kurekebisha Airport yetu ili kuharakisha maendeleo na Utalii.
 13. Rasilimali ziwanufaishe wananchi wetu
 14. Kukemea Rushwa na Ufisadi ifikie hatua ikibidi tuapishwe kwa Jina la Mwenyezi Mungu kuwa Kati ya Sisi Wagombea yeyote anayetumia pesa kuhonga Katika uchaguzi huu basi na afe kwa Jina la Mwenyezi Mungu  kwenye hili tusilete mzaha tujiulize hawa wanaotumia pesa watazirudishaje?? Kwa Njia ipi.
 15. Wanawake, wazee Vijana na Watoto kuwa na Mfuko wao maalum wa kuwakwamua.
 16. Lugha ya Kiswahili kuitumia kama mtaji kwa kuanzisha madarasa yatakayowaleta watalii kuja kujifunza Kiswahili na ikibidi watu wetu kwenda Nje ya Nchi kufundisha Kiswahili jambo litakalonipa sana Faraja.
 17. Kuziba pengo Kati ya asiye Nacho na mwenye nacho.
 18. Kupunguza Kabisa kero ya Maji na  gharama ya maji mwananchi wa kawaida apate maji pasipo Shaka.
 19. Kuwa na usafiri wa Ambulance ikibidi kila Kata ili kunusuru maisha hasa Akina Mama wanaokwenda kujifungua Hospitali.
 20. Kukaribisha wawekezaji wenye tija kwa maendeleo ya wote.
Ndugu zanguni ninayo mengi mema kwa Jimbo langu na Taifa langu na Ni matumaini yangu ya kuiona Iringa kwa jicho la Mwenyezi Mungu yaani Iringa ambayo Mungu anataka Iwe Kama alivyoikusudia na Kila Mmoja aweze kuridhika nayo.

Inawezekana Kila Mmoja Akitimiza wajibu wake, Mjenga Nchi ni Mwananchi.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Iringa, Mungu akiwa Upande Wetu Ni Nani aliye juu yetu??? Tujipe moyo Tutashinda Pamoja. 

Addo November Mwasongwe,
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania,
Wakili na Kada wa CCM
P.O.BOX 1215 Iringa Tanzania.
 0754/0713396367