Friday, June 19, 2015

TABORA WAMKUBALI MAKAMBA 100%

Mh anuary Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Tabora waliojitokeza katika viwanja vyaofisi ya CCM Wilaya wa Tabora. January yupo katika ziara yake ya kusaka wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM. Ambapo mkoani Tabora amejizolea wadhamini 9886 Mkoa wa Tabora

Mh January Makamba akipokea zawadi asali kutoka kwa mwenyekiti wa waendesha bodaboda mjini Tabora.

Mh January Makamba akipokea bahasha yenye fomu zilizowekwa sahihi na wanachama wa CCM mkoani Tabora waliomdhamini ambapo idadi ya wadhamini ni 9886.

Mh January Makamba na mkewe wakifurahia Shairi zuri lililosomwa mbele yao na mshairi kutoka Tabora, shairi hilo ni mahsusi kwa kumsifia na kumpongeza kwa uamuzi wake wa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama kugombea nafasi ya urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM

Mh January Makamba akisalimia wananchi na wanachama wa CCM Tabora Mjini mara baada ya kutambulishwa na Katibu wa CCM (hayupo pichani).

Mh January Makamba akiweka sahihi katika kitabu cha wageni cha Ofisi ya CCM Wilaya ya Tabora Mjini.

Mh January Makamba akizungumza jambo na vijana wanaofanya shughuli zao nje ya Jengo la ofisi za CCM Mkoa wa Tabora.

Mh January Makamba akiwa anatoka katika ofisi za CCM Mkoa wa Tabora huku akiwa ameambatana na viongozi wa CCM Mkoa.

Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakiwapungia mikono wananchi na wanachama wa CCM Mkoa wa Tabora

Baadhi ya waendesha Bodaboda waliojitokeza kumpokea Mh January Makamba wakiwa kwenye msafara wa kuelekea katika viwanja vya CCM Wilaya ya Tabora Mjini

No comments:

Post a Comment