Thursday, June 18, 2015

JANUARI MAKAMBA ATINGISHA JIJI LA TANGA

Mh anuary Makamba akiwasili katika uwanja wa Ndege wa tanga tayari kwa mkutano na wanachama wa CCM mkoani Tanga kwa ajili ya kusaka udhamini wa wanachama hao ili kumuwezesha kupata ridhaa ya chama kugombea nafasi ya urais. January amejizolea wadhamini 15,043 mkoa wa Tanga.

MH. January Makamba akipunga mkono kwa wanachama wa CCM na wanchi wa mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ofisi ya CCM mkoa ambapo alizungumza na kuhutubia wananchi na wanachama hao waliojitokeza kumdhamini.

Mh January Makamba akisalimiana na wananchi pamoja na wanachama wa CCM mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ofisi za CCM mkoa wa Tanga.

MMoja wa wanachama wa CCM mkoa wa Tanga akikumbatiana kwa furaha na  Mh January Makamba.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' akisalimia wananchi wa Tanga ikiwa ni pamoja na kuwepo kwake katika kumuunga mkono Mh January Makamba (pembeni) katika ziara yake ya kusaka wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM.

Mh anuary Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Tanga waliojitokeza katika viwanja vya CCM Mkoa wa Tanga. January yupo katika ziara yake ya kusaka wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM. Ambapo mkoani Tanga amejizolea wadhamini 15,043 mkoa wa Tanga. 


No comments:

Post a Comment