Friday, June 19, 2015

SASA NI ZAMU YA KINONDONI CUP, MAKONDA KUGAWA VIFAA VYA MICHEZO LEO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda akionesha sehemu ya vifaa vya michezo atavyogawa leo Jumamosi kwa timu zitazojitokeza Leaders Club jijini Dar es salaam kushiriki ligi ya Kinondoni atayoizindua kukuza vipaji.

Na Mwandishi wetu
MH: PAUL MAKONDA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, anawaomba Wanakinondoni wote na wakazi wa DSM katika kuandaa maandalizi ya Team za Wilaya ya Kinondoni zitakazo kuwa na wachezaji watakao lipwa mshahara; katika:
1.Mpira wa miguu(Football).

2.Netball.

3.Basketball.

Kushirikiana nae katika uzinduzi wa ligi hizo kesho jumamosi, saa moja asubuhi Viwanja vya Leaders. Ambapo  atazikabidhi Team 138 vifaa vya michezo. SET 2  ZA JEZZY NA MIPIRA 2 KWA KILA TEAM.WATAKUWAPO WATAALAMU WAKUPIMA AFYA ZA WACHEZAJI NA WATU WENGINE, KUTAKUWA PIA NA ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU KWA ATAKAE PENDA. TEAM ZOTE ZIKISHACHEZA KWA PAMOJA BAADAE WASHINDI  WATAUNDA  TEAM ZA WILAYA....KWA MAELEZO ZAIDI FIKA VIWANJA VYA LEADERS MAPEMA LEO(JMOS TAR 20 JUNE/2015) .

KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO....AJIRA SI BOMU.BOMU NI KUTOTUMIA KIPAJI CHAKO. SERIKALI HAZIWEZI KUAJIRI WATU WOTE KATIKA AJIRA ZA OFISINI.AJIRA INAJUMUISHA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI.NJOONI TUJIAJIRI TUPUNGUZE UGUMU WA MAISHA.INAWEZEKANA...TUTIMIZE WAJIBU

No comments:

Post a Comment