Saturday, June 13, 2015

JANUARY MAKAMBA ALIVYOLITINGISHA JIJI LA MBEYA, AJIZOLEA WADHAMINI ZAIDI YA 2000

Mh January Makamba akiwapungia mkono wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Mbeya wakati akishuka kutoka garini, wananchi hao walifika hapo katika ofisi za CCM wila ya Mbeya Mjini kwa aijili ya kumdhamini.
Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakisalimiana na wananchi pamoja na wanachama wa CCM mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ofisi za CCM wila ya Mbeya Mjini.
Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakiwapungia mikono wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Mbeya  walipowasili katika viwanja vya ofisi za CCM wila ya Mbeya Mjini.
Mh January Makamba akiweka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi ya katibu wa CCM wilaya ya Mbeya Mjini mara baada ya kuwasili katika ofisihizo, kushoto ni mke wake Ramona Makamba. Mh January Makamba yupo mkoani mbeya katika ziara yake ya kusaka wadhamini ndani ya chama ambao watamuwezesha kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM.
Baadhi ya wanachama na wananchi wa mbeya walijitokeza kumdhamini  Mh January Makamba katika ofisi za chama cha mapinduzi wilayaya Mbeya Mjini. Idadi ya wadhamini ikiwa ni zaidi ya 2000
Katibu wa CCM wliaya ya Mbeya Mjini, Kulwa Milonge akizungumza na wanachama na wananchi wa mbeya walijitokeza kumdhamini  Mh January Makamba katika ofisi za chama hicho Mbeya mjini.
Katibu wa CCM wliaya ya Mbeya Mjini, Kulwa Milonge akimkabidhi Mh January Makamba fomu yenye majina na sahihi za wanachama wa CCM waliomdhamini huku idadi ya wadhamini ikiwa ni zaidi ya 2000.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Mjini, Alhaji Kundya akizungumza na wanachama na nanchi wa mbeya walijitokeza kumdhamini  Mh January Makamba katika ofisi za chama hicho Mbeya mjini.
Mh January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Mbeya  mara baada ya kabidhiwa fomu yenye sahihi za wanachama waliomdhamini. Idadi ya wadhamini ikiwa ni zaidi ya 2000. 
Picha zote na Suleiman Lyeme.

No comments:

Post a Comment