Wednesday, June 10, 2015

JANUARY MAKAMBA AMALIZA KAZI DODOMA, ASEMA HAKUJA KUJARIBU ANANIA THABITI YA KUIJENGA TANZANIA MPYA

Katibu mkuu mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba akizungumza na baadhi ya wadau waliofika kusapoti Mh Januari Makamba nje ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma kabla ya January kuchukua Fomu.
 Mh. January Makamba na Mkewe wakisalimiana na wanachama waliokuja kumuunga mkono katika harakati ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea urais kupitia chama cha mapinduzi. 
Mh. January Makamba na Mkewe wakionesha mkoba waliokabidhiwa na seif Khatib (kushoto) kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidiwa fomu hizo.

Mh. January Makamba akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma. Pembeni yake ni mkewe.
Katibu mkuu mstaafu wa chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba na mkewe wakifuatilia mazungumzo ya Mh. January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa makao makuu ya CCM mjini Dodoma mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea nafai ya urais.
 Mh. January Makamba na Mkewe wakitoka katika ukumbi wa makao makuu ya CCM mkoani dodoma mara baada ya kuchuka fomu ya komba ridhaa ya kugombea urais kupitia Chama hicho.
Mh January Makamba akiwasili katika viwanja vya Ofisi za CCM dodoma mjini kwa ajili ya kuzungumza na wanachama wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kumdhamini.
 Mh. January Makamba akizungumza na Mwanachama wa CCM mjini Dodoma mwenye ulemavu katika viwanja vya CCM Dodoma Mjini.
Mh. January Makamba na mkewe wakipeana mikono na baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini katika ofisi za CCM Chamwino.
Mh. January Makamba na mkewe wakitazama baadhi ya wadhamini wao wakiweka sahihi katika kitabu cha wadhamni.
mh. January Makamba Katikati) akizungumza na mtoto Salua Salum (4) aliyejitokeza kumsapoti katia ofisi za CCM dodoma.
Mwenyekiti wa CCM dodoma mjini, Paulo Luhano akishereha jambo wakati mh January Makamba alipowasili ofisini hapo kwa ajili ya kukusanya sahihi za wadhamini wa chama hicho ili kumuwezesha kupitishwa kuwania nafasi ya urais kupitia CCM. January Makamba alijizolea wadhamini 1200 ikiwa ni idadi ya chamwino pamja na Dodoma mjini. 
Mh. January Makamba na Mkewe wakiweka sahihi katika kitabu cha wageni na kitabu cha wadhamini katika ofisi za Dodoma mjini.
Mh. January Makamba akiweka sahihi katika kitabucha wageni katika ofisi za CCM Dodoma Mjini.
January Makamba akizungumza na mtoto Saluwa Salum. Mtoto huyu ana kadi ya chipukizi ya CCM.
Baadhi ywa wanachama wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma wakiwa katika ofisi za ccm chamwino. January Makamba amevunja rekodi kwa kupata wadhamini wengi Mjini Dodoma akiwa na jumla ya wadhamini 1200 kwa Chamwino (500) na Dodoma mjini (700).
 Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

No comments:

Post a Comment