Monday, September 27, 2010

KAA TAYARI KWA SHOW KABAMBE YA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010

Kampuni ya Unique Entertainment inatarajia kufanya show bab-kubwa ya mitindo nchini Tanzania iitwayo Giraffe unique model 2010 itakayojumisha shindano la wanamitindo kumi bora wa kike ambapo vigezo vya wanamitindo hao vitatajwa hivi karibuni.
    Lengo la shindano hili ni kuinua sanaa ya mitindo nchini Tanzania ambapo inaweza kutoa ajira kwa vijana kama kazi zingine kwa muda wote,hii ni tofauti sana na mashindano mengine kwani washiriki wote kumi watakuwa na nafasi ya kuwajibika katika jamii na binafsi kwa kumuingizia kipato mwanamitindo tofauti na mashindano mengine kwa mwaka mzima.
  ITADHAMINIWA Na : Graffe ocen view hotel,Tanga beach resort hotel, Truworths,uniqueentertz blog na wadhamini wengine wataendelea kutajwa.  STAY TUNED

KAMA KAWA GAZETI LAKO PENDWA LA DIRA YA MTANZANIA LIPO MTAANI LEO.


Gazeti mahiri kwa habari za uchambuzi wa mambo ya siasa,michezo burudani na mengineyo linalochapishwa na Kampuni ya Dira Media Group lipo mitaani kwa mara nyingine tena,kama ada yake huwa limesheheni habari kibao za kusisimua.! Usikose jipatie nakala yako mapema kwa shilingi 400/= tu kwa kila kopi.

WATUMIAJI WA VODACOM SASA KUCHATI BURE.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.
Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.
Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.
“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.
Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.
Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Moderm.

Saturday, September 25, 2010

FLEVA ZA KITAA!

Yuda Skills akitoa burudani kwa watu wake wa kitaa
Hapa mtoto wa kitaa *The DON* nikishow lavu na warembo Marry na Lucy huku nikiwa na Mr Kitime na DJ Kinyonga

Hapa Mr Kitime akishow lavu na DJ Kinyonga (kushoto) na DJ SB (kulia)..

KAMA kawa mashindano yetu ya kitaa ya mpango mzima wa kudansi bado yanaendelea palepale!

TUWASAIDIE WATOTO HAWA WA MITAANI WA NEW HPOE FAMILY STREET CHILDREN.

KITUO cha kulea watoto waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu na Hatarishi cha ‘New Hope Family Street Children’ cha jijini Dar es Salaam kimewaomba wafadhili kujitokeza kwa wingi ilikuwasaidia misaada ya haraka ikiwemo chakula na mahitaji mengine ya muhimu ya kila siku.
Walisema hayo jana wakati wakipokea msaada huo wa vyombo vya ndani vilivyotolewa na Uongozi wa Vijana kupitia Pasta Freddie Kyara na 'Madam Nuru' wa Kanisa la St. Columbus la Upanga jijini Dar es Salaam, katika makazi ya watoto hao kilichopo Ungindoni Kigamboni.
Vitu hivyo vilikabidhiwa na Mratibu wa na Afisa uhusiano wa kituo hicho Andrew Chale kwa niaba ya uongozi huo wa vijana wa St.columbus Youth, kwa watoto hao, Andrew aliwashukuru wasamalia kwa kujitokeza na kutoa msaada wao ambao umeweza kuonyesha tija na faraja kwa watoto hao.
"Tunashukuru sana kwa msadaa wa vitu hivi ambavyo ni chachu kubwa sana kituo hichi tunaomba wadau wengine kujitokeza ilikufanikisha zoezi la kuwasaidia watoto hawa' alisema Andrew.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo hicho Omary Rajabu alisema kuwa watahakikisha wanavitunza na kuvitumia kwa matumizi sahihi yaliyokusudiwa na kituo hicho. “Tunafarijika kwa msaada wa vitu hivi tunahakika vitakuwa faraja kwetu na kuvitunza ilikufanikisha kazi shughuli za kituo” alisema Omary.
Kanisa hilo kupitia vijana wake (St. Columbus Youth) walichangia vyombo mbalimbali vya kupikia ikiwemo; taa za chemri,masufulia,vikombe,sahanai,jiko,na ndoo za maji na vifaa sabuni na miswaki.
Watoto hao kwa pamoja waliomba jamii iliyo na uwezo kujitokeza kuwasidia misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula na maswala ya elimu. “Tunaomba msaada wa chakula ilikitusaidie kwa miloo kamili tulivyokuwa navyo havitoshelezi” walisema watoto hao.
Kituo hicho kwa siku kinatumia chakula kilo 25, kiwango ambacho kwa hali ya kituo chao akikidhi hivyo waliomba wadau walio na uwezo kujitokeza na kuwasaidia vitu kama Mchele, Unga, Maharage ,mafuta na vyote vya kula.

Friday, September 24, 2010

KITUO CHA KAZI KIPO HEWANI.

Huyu ndio mkubwa wa kituo cha kazi Henri Mdimu
Hii ndi logo (nembo) ya kipindi chenyewe.

Kama kawa kama dawa kipindi chenu cha burudani cha KITUO CHA KAZI sasa kipo hewani huku kikiongozwa na kuratibiwa na kaka mkubwa Henri Mdimu a.k.a Zee la Nyeti huku akipewa sapoti na mtu mzima Mwana FA a.k.a Binamu na Fid Q wakati mitamboni akisimama Maliki a.k.a Mkoloni
Kipindi hiki kitakuletea mambo mengi tu ya burudani ikiwa ni pamoja na habari za hapa na pale huku wakichambua pia habari za michezo. Pia kita kukutanisha na wadau mbalimbali wa burudani hapa nchini. kipindi ni kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa Radio Times, ..100.5 FM kuanzia saa tatu asubuhi mpaka sita mchana!

Wednesday, September 22, 2010

MUSIC LAB YATOA OFA KWA WASANII WACHANGA.

Kama kawa studio ya Music Lab ndio imetoa ofa ya dizain hiyo ambayo imepewa jina la underground campaigne huku mpango mzima ukisimamiwa na mtu mzima DUKE amabe nio producer wa studio hiyo. Hivyo ukiwa kama msanii mchanga na unajua kama unakipaji basi fika pande zile ili uweze kuinua kipaji chako!

KCB TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA VITABU VITABU SHULE YA KINONDONI MUSLIM.

Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, Rajabu Mruma msaada wa vitabu vya masomo na samani  za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili  pamoja na kuinua kiwango cha elimu. Kushoto ni Kaimu mkuu wa shule hiyo, Mohammed Songo
 
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akiwaeleza jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim Tiba Kalufya na Mayasa Hemed mara baada ya kuikabidhi shule hiyo msaada wa vitabu vya masomo na samani  za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili  pamoja na kuinua kiwango cha elimu. Kulia ni mkuu wa idara ya masoko na mahusiano wa benki hiyo Christina Manyenye.
 
Wanafunzi wa  Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim wakijisomea vitabu vilivyotolewa na benki ya KCB Tanzania mara baada ya hafla ya makabidhiano ya msaada wa vitabu vya masomo na samani  za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili  pamoja na kuinua kiwango cha elimu iliyofanyika jana (leo) jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akiwapa vitabu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, mara baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo na samani  za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili  pamoja na kuinua kiwango cha elimu
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, mara baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo na samani  za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili  pamoja na kuinua kiwango cha elimu iliyofanyika shuleni hapo

Monday, September 20, 2010

GAZETI LAKO LA DIRA LIPO MTAANI SASA. GET YO COPY TODAY.

K
L
  
Na huo ndio muonekano mzima wa gazeti la dira ikiwa ni mwanzo kati na mwisho.

Friday, September 17, 2010

BASATA LATOA DARASA KWA VIONGOZI WA WASANII.

Mmoja wa viongozi wa baraza la sanaa tanzania (BASAT) aiktoa muongozo kwa baadhi ya viongozi wa wasanii.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka viongozi wa mashirikisho ya wasanii kuhakikisha wanakuwa imara na thabiti ili kuleta ufanisi kwenye mashirikisho ya wasanii nchini yaliyoundwa na kupata viongozi wake hivi karibuni.
Hayo yamesisitizwa na Wakufunzi kutoka BASATA wakati wakitoa semina kwa viongozi wa mashirikisho ya wasanii nchini iliyofanyika wiki hii kwenye ukumbi wa Baraza hilo na kuhudhuriwa na viongozi wote wa mashirikisho ya wasanii na wajumbe wao.
Mashirikisho yaliyohusika kwenye semina hiyo ni pamoja na lile la Sanaa ya Muziki, Maonyesho,Ufundi na Filamu ambapo mada mbili zilizotolewa kwa viongozi hao ambazo ni Wajibu na Maadili ya Uongozi wa Mashirikisho ya Sanaa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji wa BASATA,Bw.Ruyembe Mulimba na na ile ya Mchakato wa Kuandaa Mpango Mkakati wa Shirikisho iliyowasilishwa na Mwalimu Rashid Masimbi kutoka Kituo cha Sanaa za Maonyesho Tanzania.
Akizungumza kwenye semina hiyo,Ruyembe alisema kwamba, viongozi wa mashirikisho ya wasanii hawana budi kuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wasanii,kuwa na mwenendo mwema, kuzingatia maadili ya uongozi, kuzingatia dhana ya kutangulia na kuelekeza huku mtangulizi akiwa anafahamu anakowapeleka watu anaowaongoza.
“Kiongozi mzuri lazima aelewe majukumu na mwenendo mwema katika kazi ya kusimamia watu ambao wanahusika na utendaji wa shughuli husika kwa ushirikiano na kwa pamoja kulingana na Katiba iliyopo” alisisitiza Ruyembe.
Aliongeza kwamba, historia inaonesha vyama vingi na shirika za wasanii zimekuwa kwenye migogoro isiyoisha kutokana na viongozi kutokuwa na utashi wa kuongoza., kutanguliza maslahi binafsi na kushindwa kabisa kuwa na maono ya kutekeleza mikakati inayokuwa imewekwa.
Alizidi kufafanua kwamba, wasanii wanakumbwa na changamoto nyingi sana zikiwemo za wao kuibiwa kazi zao, kunyonywa kupitia mikataba, kulipwa malipo kidogo na ukosefu wa masoko hivyo viongozi wa mashirikisho hawana budi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto hizo zinawekewa mikakati ya kupunguzwa kama si kumalizwa kabisa.
Naye Mwalimu Rashid Masimbi alisema kwamba, moja ya kazi ya viongozi hao wa mashirikisho ya wasanii ni kuhakikisha wanakuja na Mpango Mkakati wa muda mfupi na mrefu ambao utalenga kujenga dira ya utendaji na mafanikio ya mashirikisho.
Aliongeza kwamba, viongozi hawana budi kuwa na mpango mkakati ambao utaeleza nini kitafanyika,nani atakifanya, kwa namna gani na kwa muda gani.
“Mpango Mkakati ndiyo dira, dhamira, malengo, shughuli na matokeo ya utendaji wa shirikisho lolote hivyo lazima nyinyi viongozi mtuoneshe ni kwa jinsi gani tutayafikia haya” alisisitiza.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria semina hiyo waliishukuru BASATA kwa mpango huo na kusisitiza kwamba, semina kama hizo ziandaliwe mara kwa mara ili kujenga ufanisi wa mashirikisho ya wasanii na sekta ya sanaa kwa ujumla.

SLAA ATINGA VIWANJA VYA NYUMBANI KWA KISHINDO.

Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu leo.
Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea wa ubunge katika jimbo la Karatu kupitia chama hicho, ambaye ni mridhi wake, Mchungaji Israel Natse, wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu jana.
Dk. Willibrod Slaa, akizungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni zake kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Bariadi juzi.
  
Baadhi ya wanachma na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakishangilia hotuba ya mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wakati akihutubia mkutano wa kampeni zake, kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu leo.

JAMANI KUBAMBIA KUNA RAHA!


Kama kawaida mshikaji wa ukweli kabisa 'Magese' ambae ndio mmliki wa blog ya UNIQUE ENTERTAINMENT ambayo inajihusisha zaidi na masuala ya urembo akiwa amembambia mrembo mmoja anaejulikana kwa jina la Prsca

WATUMIAJI WA VODACOM SASA WAPATA AHUENI.

Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake katika huduma ya kupiga simu, ambapo wateja wa Vodacom wataweza kupiga simu kwenda mitandao mingine nchini kwa punguzo la zaidi ya asilimia 50.Hii ni katika jitihada za kampuni hii kuhakikisha kuwa mawasiliano yanapatikana kwa gharama nafuu, nchi nzima.
Gharama hizi mpya zitamruhusu mteja wa Vodacom kuweza kupiga kwenda mitandao mingine kwa kiasi kidogo cha shilingi tatu tu za kitanzania kwa sekunde, wakati hapo awali gharama ya kupiga simu kwenda mitandao mingine ilikuwa shilingi sita na nusu.
Huduma hii imekuja miezi michache tu baada ya Vodacom kuzindua huduma nyingine ya shilingi moja kwa sekunde , maarufu kama HABARI NDIO HII.
Ikiwa na wateja milioni nane nchini, kampuni ya Vodacom imeendelea kutoa bidhaa na huduma kwa wateja wake,na kuwawezesha kupata mawasiliano kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacon Tanzania, Mwamvita Makamba alisema jana kwamba kuwa gharama hizi mpya zimeleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano ya simu nchini.
“Kama tulivyozindua huduma ya Habari Ndio Hii, tumejikita kuhakikisha kuwa mtandao wetu unatoa bidhaa na huduma bora kwa wateja wetu ili kuwajenga kiuchumi.”
Kampuni ya Vodacom imekuwa nchini kwa miaka kumi sasa na inatabiri kukua zaidi katika sekta hii mwaka huu na miaka mingine ijayo.
“Tutamatumaini makubwa juu ya utendaji wetu hapo mbeleni na tunashauku kubwa kuweza kutoa huduma zetu zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.”
Huduma zingine za Vodacom kama Vodajamaa na Cheka Time zitabaki kama zilivyo.
“Vodacom inawahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu hapo mbeleni” Bi Pendaeli alihitimisha kusema.

Wednesday, September 15, 2010

SUGU AANDAA TAMASHA KWA AJILI YA WATU WAKE WA MBEYA MJINI.

Sugu akiwa kwenye kombati ya CHADEMA huku ameshika kipaza akiongea na watu wake katika moja ya kampeni zake za kuomba kura kwa wananchi

Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Ijumaa hii ataweka kando gwanda maalum ambalo ni sare ya chama chake, na kulipa kisogo jukwaa la siasa, na atashika kipaza sauti ‘MIC’ na kudondosha shoo kali ya Hip Hop kama ilivyokawaida yake. Sugu, anatarajia kutoa shoo kwa kushirikiana na mastaa wengine wa muziki wa kizazi kipya kwenye Ukumbi wa Mtenda Sunset uliopo Mbeya. Wasanii ambao wametajwa kupanda jukwaa moja na Sugu siku hiyo (Septemba 17) ni Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, Ferouz Mrisho Rehani, Abbas Hamis Kinzasa ’20 Percent’, Danny Msimamo, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Gerald Mwanjoka ‘G Solo’, Mapacha ‘Maujanja’ na Isanga Family’. Akifafanua kuhusu kupanda jukwaani na kuvua kombati ya CHADEMA, Sugu alisema atafanya hivyo kama sehemu ya harambee ya kukusanya fedha za kumaliza kazi ya kulitwaa Jimbo hilo. “Wala siyo utani kaka, Ijumaa navua gwanda, navaa jeans. Nitakuwa na saa nzima ya kutoa shoo ya muziki kwa watu watakaohudhuria onesho hilo. Nataka niwaoneshe watu wangu wa Mbeya kile ambacho huwa nafanya. “Kuna watu wanasikia tu lakini hawajawahi kuona shughuli yangu jukwaani. Nitawaonesha. Wanakuja wakali kama Ferouz, Afande Sele, 20 Percent, Mkoloni, Msimamo, G Solo, Mapacha, Isanga Familiy na wengineo,” alisema Sugu na kuongeza: “Ni shoo maalum ya kuchangia kampeni. Tumegawa kadi maalum ambapo kuna maeneo zinanunuliwa kama njugu. Kila kadi tunauza shilingi 10,000. Tunapiga hatua kubwa na naamini tutafika kwa sababu tunapata sapoti ya kutosha kutoka kwa watu wangu kama ambavyo unaona wanamuziki wanaacha kazi zao wanakuja kushirikiana na mimi kaka yao kukusanya michango ili kuniwezesha.” Kuhusu maendeleo ya kampeni zake, Sugu alisema kuwa tumaini la ushindi linaongezeka kila siku kiasi ambacho haoni wapi ambapo anaweza kukosea na kutoa nafasi kwa mpinzani wake kupenya. Alisema, juzi alifanya mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mbeya kwenye Uwanja wa Mbembela uliopo Kata ya Nzovwe, Iyunga na kuvunja rekodi ya mahudhuria ya ule wa uzinduzi wake uliochukua nafasi Uwanja wa Ruanda Nzovwe, Kwamama John. Kuhusu afya ya mshirika wake, Mkoloni aliyelishwa sumu, Sugu alisema: “Kwanza namshukuru Mungu anaendelea vizuri, leo (juzi) alikwenda tena hospitali kuangalia macho. Anaendelea vizuri, pengine waliompa sumu walitaka kummaliza ila yote tunayaacha apone kwanza, muhimu ni kwamba Ijumaa tutakuwa naye hapa kufanya shoo.
TUMUUNGE MKONO MWANA HARAKATI HUYU KATIKA KULILETEA MAENDELEO JIMBO LA MBEYA MJINI.

Monday, September 13, 2010

DIRA YA MTANZANIA YAMTOLEA UVIVU SHEIKH YAHYA NA IKULU.

Hili ndio gazeti la Dira ya mtanzania linavyoonekana kwa mbele.
Na huu ndio ukurasa wa pili unavyioonekana.

Na huu ndio mpango mzima kuhusu sakata lenyewe. Lipo ukurasa wa 8 na 9 a.k.a center.

CHADEMA YAFUNIKA BUNDA.

Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ),Dk.Willibrod Slaa,akiwahutubia maelfu ya Wananchi wa mji wa Bunda,Kwenye uwanja wa Sabasaba katika mfululizo wa kampeni zake jana

Grand Malt yakusanya maelfu Coco beach

Mfalme wa Rymes afande Sele akiwa jukwaani huku akipagawisha mashabiki waliofurika katika fukwe ya coco beach jijini dar, jana j'pili katika bonanza la Grand Malt.
  
Washereheshaji wa shughuli a.k.a Wasema chochote au MC's wa bonanza la Grand Malt wakienda sambamba na mmoja wa vijana waliopanda jukwaani kuonyesha vipavi vyao.
  
Hahahahahahah! Pia mambo ya taarabu yalionyeshwa na vijana wa kike katika bonanza la Grand Malt lililofanyika jana katika fukwe ya coco beach jijini dar.
 
 Hapa Temba, pale Chege kiujumla ni TMK Family wakifanya vitu vyao katika bonanza la Grand Malt lililofanyika jana katika fukwe ya cocobeach jijini dar.
  
Na hili ndio nyomi lililokuwepo pande zile kuliokokuwa kukifanyika bonanza la Grand Malt jana pale katika fukwe ya coco beach

Thursday, September 9, 2010

TUMUUNGE MKONO SUGU KATIKA HARAKATI ZA KULIKOMBOA JOMBO LA MBEYA MJINI.

Tuungane kiukeli katika kufanikisha huu ushindi kama kweli wewe unahitaji maendeleo basi ni lazima utatakiwa kuchagua wanaharakati kama huyu (JOSEPH MBILINYI)
TUMUUNGE MKONO MWANAHARAKATI HUYU KATIKA KULIKOMBOA JIMBO LA MBEYA MJINI.

EID MUBARAK

 
Hii ni picha inayoonyesha eneo la alqa-aba ambapo ni sehemu takatifu waislamu wanayoielekea wakati wa kuswali
Huyu ndio mtoto wa kitaa akiwa katika vazi la kanzu bana.

Mtoto wa kitaa kama kawa anawatakia watazamaji / watembeleaji wote wa blog hii Kheri ya sikukuu ya eid el-fitri.

HAWA NDIO WASHIRIKI WOTE WA VODACOM MISS TANZANIA 2010.

Wednesday, September 8, 2010

ALLIANCE FRANCEE WATANGAZA MICHONGO KWA WASANII

Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Utamaduni cha Ufaransa, Didier Martin (Katikati) akiwasilisha mada yake iliyohusu Mchango wa Asasi kama yake Kwenye kukuza Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania.Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego na Ruyembe Mulimba
Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Alliance Francee, Didier Martin muda mfupi baada ya kuliahirisha Jukwaa la Sanaa hadi Jumatatu ijayo ambapo Mada kuhusu Changamoto za Sanaa ya Unenguaji Itawasilishwa.
  
Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Hussein Jumbe yeye alitaka aelezwe ni kwa Jinsi gani ataweza kushiriki Tamasha la Sauti za Busara ambalo limekuwa likidhaminiwa pia na kituo hicho.
Msanii wa Kizazi kipya Symon John aka Gheto King akichangia hoja kwenye Jukwaa la Sanaa
 Sehemu ya wadau wa Jukwaa la Sanaa wakifuatilia kwa makini wasilisho la Mkurugenzi wa Alliance Francee, Didier Martin


========= ======== =======


ALLIANCE FRANCEE WATANGAZA MICHONGO KWA WASANII
Kituo cha Kimataifa cha Utamaduni cha Ufaransa (Alliance Francee) kimewataka wasanii wa Bongo kutumia programu yake ya Barazani katika kutangaza kazi zao na kuzifanya zitambulike na kupata soko kimataifa.

Barazani ni programu ya ‘pafomansi’ za kisanaa ambayo imekuwa ikiwahusisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na imekuwa ikifanyika kwa mwezi mara moja kwenye kituo hicho cha utamaduni.Mwezi huu itafanyika Tarehe 15.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwa kuandaliwa na BASATA likishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz),Mkurugenzi wa Kituo hicho BW.Didier Martin alisema kwamba, wasanii hawana budi kulitumia jukwaa hilo katika kuuza na kutambulisha kazi zao kwani limekuwa likihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani.
Alisema kwamba, ushiriki wa wasanii kwenye jukwaa hilo uko wazi kinachotakiwa ni wasanii wenyewe kuchangamkia fursa hiyo kwa kufika kwenye kituo hicho na kujiandikisha.

Aidha, alisema kwamba, kwa sasa kituo hicho kinatoa mafunzo ya lugha ya Kifaransa kwa watu mbalimbali na kuongeza kwamba, gharama za malipo zimepunguzwa kwa wasanii hadi kwa zaidi ya asilimia hamsini hivyo ni fursa pekee kwa wasanii kujifuna lugha hiyo ya kigeni.

Kuhusu nyimbo za wasanii wa muziki kusikika redioni,alisema kwamba, Ufaransa imefungua kituo cha redio ambacho kitarusha matangazo kwa lugha ya Kiswahili na kuongeza kwamba, mwezi ujao wanatazamia kuanzisha dawati la Kiswahili.Bila shaka wasanii wanaobanwa kwenye ‘ea taim’ watumie fursa hiyo.

Masuala ya msingi yaliyojadiliwa kwenye jukwa la sanaa Jumatatu hii na wadau wengi ni pamoja na haja ya kituo cha Alliance Francee kupenya hadi vijijini, kusaidia kuhamasisha wawekezaji wa Kifaransa kujenga studio za kurekodia nchini, kusaidia usambazaji wa kazi za wasanii,kutoa msaada wa kifedha kwa wasanii nchin, kuzitangaza kazi za wasanii wa ndani nje ya miapaka nk.

Akijibu masuala hayo, Mkurugenzi Martin alisema kwamba, kwa sasa kituo chake kinatoa msaada wa fedha kwa wasanii wanaofanya sanaa zenye uasili wa Tanzania na kusisitiza kwamba, wasanii wa Tanzania lazima waachane na dhana ya kunakiri kazi kutoka nje bali wajikite kwenye kutengeneza kazi za sanaa za asili.

Aliongeza kwamba, tatizo la masoko ya kazi za Sanaa ni kubwa lakini akasisitiza kwamba, wasanii wanapaswa kujikita kwenye ubunifu wa kazi zilizo bora na zenye kubeba asili ya Tanzania ili kuzifanya kuwa tofauti na zile zinazotolewa sehemu zingine duniani.


Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonce Materego alisema kwamba, Baraza lake litaendelea na utaratibu wa kuwapa wasanii fursa mbalimbali za kukutana na wadau wa sanaa wa ndani na nje hata hivyo naye akakumbusha kitu ambacho ambacho muda wote amekuwa akikisisitiza cha wasanii wetu kubuni kazi zenye asili ya kwetu.

Alisema kwamba, kunakiri kila kitu kutoka nje maana yake ni kudumaza sanaa yetu na hivyo kuwafanya wasanii kushindwa kushindana kwenye masoko kutokana na kutengezeza kazi zinazopatikana kwingineko duniani.
Picha/ Habari na Afisa Habari wa BASATA, Alistide Kwizela

Monday, September 6, 2010

TUWAEPUEKE SANA VIONGOZI WA DIZAINI HII.

Kama kiongozi anaweza kutumia fedha nyingi kuliko zile atakazoenda kulipwa kama posho kule mjengonui (Bungeni) wewe unadhani ataweza kukuletea maendeleo kweli!? hapa ni lazima ataanza kurudisha kwanza zile alizozitumia ndio kama itawezekana awakumbuke baadae na hapo muda utakuwa umekwisha. Kupata katuni kama hizi tembelea ww.sidymic.blogspot.com
TUMIA VIZURI KURA YAKO

HALIMA MDEE ATEMA CHECHE JIMBO LA KAWE.

Kamama kawa kama dawa mtoto wa kitaa jumapili huwa nakuwa nimetulia tu kitaani kwangu. nikiwa katika misele ya hapa na pale kitaani kwangu si ndio nikasikia sauti kama za mziki hivi zikisikika si ndio nikasema ngoja nijisogeze nicheki kuna kitu gani kinaendelea kitaani kwangu kwa maana siku zote za wiki mtoto wa kitaa nipo na pilika za ujenzi wa hili taifa letu. Kusogea si ndio nikamgumia mdada makini kabisa ambae nkitaaluma ni mwanasheria na kutokana na uwezo wake wa kaza aliweza kulitingisha bunge lililopita akiwa katika vit maalum. Na sasa yupo kikazi zaidi akiwa ndio mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la kawe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHDEMA). Halima Mdee kwa sasa anaendelea na mikutano yake ya kampeni katika jimbo lake ila jana alikuwa kitaani kwetu katika kitongoji cha kawe mzimuni akizungumza na wananchi wa pande zile ambao ndio wapiga kura wake!
Mdee aliongea mambo mengi sana lakini cha misngi alikua anomba tu kura! kauli mbiu yake ni
VIJANA WA KAWE TUAMKE, TUSIDANGANYIKE!

Hapa Halima Mdee akiwa anamwaga sera zake jukwaani.
Hawa ndio baadhi ya wadau waliofika kwenye mkutano huo.
  
Ilifika hatua ya kumtambulisha mama yake mzazi kwa wapiga kura wakena Halima Mdee alifanya kama anavyoonekana
Huyu ndio mama mzazi wa Halima Mdee
Baada ya kuteremka jukwaani alikutana na mwandishi wa habari na aliulizwa maswali mawili matatu na aliyajibui kikamilifu!