Wednesday, July 31, 2013

IBRA WA 'WAKALI DANTA' AUAWA KWA KUCHOMWA KISU WAKIGOMBEA MWANAMKE


Marehemu Ibra enzi za uhai wake.
WAKATI Waislamu wakiwa ndani ya Mfungo wa Ramadhani, mapenzi yamemuua kijana Ibrahim Ibrahim ‘Ibra’ wa Kundi la Wakali Danta la Magomeni jijini Dar kwa kuchomwa visu.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 27, mwaka huu maeneo ya Magomeni Kagera ambapo ndugu wa Ibra, Ally Jumanne Sanane alidai kuwa, Ibra alichomwa kisu na kijana aliyefahamika kwa jina la Kelvin wakimgombea demu aitwaye Fatma Kiduku.
Mtoa habari huyo alidai: “Fatuma alikuwa ni mchumba wa Ibra lakini pia inaonekana alikuwa akitoka na Kelvin.
“Siku ya tukio Kelvin alikutana na Fatuma, akamuanzishia vurugu akimuuliza sababu ya kumuacha yeye ili aolewa na Ibra. Vurugu ilikuwa kubwa, Fatuma akaamua kumuita Ibra ili amsaidie.
“Ibra alipofika ndiyo akaanza kupigana na Kelvin, kuona amezidiwa Kelvin alitoa kisu na kumchoma cha kwanza kisha cha pili na ndiyo Ibra akaanguka chini na hakuamka tena,” alidai mtoa habari huyo.
Baada ya tukio hilo inadaiwa Kelvin na Fatuma walikimbia hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamepatikana. 
 Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 27, saa 9:30 eneo la Brazil Magomeni Kagera. 
Kamanda Wambura alisema kuwa Kelvin ambaye anahusika na mauaji hayo anasakwa na jeshi la polisi.
Mbali na Kelvin pia  mwanamke ambaye ndiye chanzo cha tukio hilo naye anasakwa.
Kesi hiyo imefunguliwa jalada namba MAG/IR/5600/ 2013 MAUAJI.
Uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea zaidi ili kuweza kuwakamata wahusika waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria
SOURCE-GPL

MONALISA: SINA MPANGO WA KUOLEWA TENA

Msanii mkongwe  kwenye  soko  la  filamu  Tanzania,Yvonne Cherry "Monalisa"  amesema  hatarajii  kuolewa  tena  baada  ya  kuvunjika  kwa  ndoa  zake  kadhaa  ikiwemo  ile  ya  producer  Tyson....
Akisimulia  mikasa  ya  maisha  yake  mbele  ya   mwandishi  wetu,Monalisa  aliema  kuna  siku  walipokuwa  kwenye  kikao  cha  sendoff  ya  mama  yake, alitania  na  kusema  ataolewa  disemba  lakini  hakuwa  serious....
"Sina  mpango  wa  kuolewa  kabisa,kwanza  sina  mchumba, ntaolewaje?
"Siku  ile  nilikuwa  natania  tu kwa  sababu  sipo  tayari  kuolewa  na  kuachika  tena"..Alisema  Monalisa

BONDIA MTANZANIA OMARI KIMWERI ALIVYO MGALAGAZA EKKALAK SAENCAN WA THAILAND KWA KO


Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake baada ya kumtwanga  Ekkalak Saenchan  wa Thailand kwa KO raundi ya kwanza.

Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa akimsukumia makonde mazito mfululizi bondia Ekkalak Saenchan  wa Thailand na kufanikiwa kumtwanga kwa kwa KO raundi ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita.
PICHA NA kwa hisani ya www.superdboxingcoach.blogspot.com

Monday, July 29, 2013

MBUNGE WA KINONDONI AJISALIMISHA POLISI KWA TUHUMA ZA KUFADHILI BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.
Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.
"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike  na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan kwa njia ya simu
"Mimi sipo juu ya sheria ,  itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza:
 "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao," alinukuliwa Mbunge huyo.

MAUTI YAWAKUTA WAKIFANYA NGONO

Kwa Mujibu wa Ripoti iliyotolewa na wakazi wa eneo husika, inasemekana kwamba Bw. Mathias Nwoko (45), na Binamu yake Angela Ihuoma walifikwa na Umauti wakati wakiwa katika tendo la ndoa. 
Wawili hao ambao asubuhi kabla ya kufariki walionekana pamoja wakicheza kwa furaha katika sherehe za kumkaribisha Padri Mpya katika Jimbo lao, Mathias ambaye ameelezwa alikuwa ndani ya ndoa kwa kipindi cha miaka 13 bila ya kupata mtoto alirudi na binamu yake usiku wakitokea kusikojulikana na kumkuta mkewe akiwa anaangalia T.V nyumbani kwake.
Mathias alimwambia mkewe atangulie kulala kwasababu yeye anachukua tochi amsindikize binamu yake huyo kwao. Mama mzazi wa Angela alipoona usiku unazidi na mwanawe hajarudi alimtafuta kupitia simu yake ya mkononi ambayo alipokelewa na Mathias akimwambia wapo pamoja.
Mpaka asubuhi, Si Mathias wala Angela Aliyerudi kwao na ndipo familia zote mbili zilipoingiwa na wasiwasi, Mke wa Mathias alienda katika nyumba yao ya pembeni asubuhi hiyo na ndipo alipowakuta wawili hao, mwanamke akiwa juu ya mwanaume.
Aliganda kwa muda asiamini anachokiona,hasa kuona wawili hao hawashtuki japo kawaona na ndipo alipogundua ya kwamba wamefariki Dunia. Ilibidi kutoa taarifa kwa familia ya Angela ambapo alikuja mama yake mzazi ambaye alipigwa na butwaa kutokana na picha iliyokuwa mbele yake.
Miili yao ilitenganiswa na kupelekwa hospitali huko Ogbor Nguru, jimbo la Aboh Mbaise.

Thursday, July 25, 2013

NGOMA MPYA KUTOKA KWA DADY DADYZ (SOLO 2 & A2) FT TASH


MSONDO NGOMA MUSIC YAINGIA STUDIO NA KUTANGAZA RATIBA YA IDDI


Msemaji wa kundi la Msondo, Super D

Na Mwandishi Wetu

BENDI Kongwe ya Mziki wa dansi nchini Msondo Ngoma imeingia Studio kurekodi nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika Albam moja akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Bendi Hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa bendi yake kwa sasa imeingia studio kukamilisha kurekodi nyimbo zao mpya
Alizitaja nyimbo hizo kuwa li Suluhu uliotungwa na Shabani Dede,Lipi Jema na Baba Kibebe wa Eddo Sanga,Nadhili ya mapenzi wa Juma Katundu,Kwa momba akuna Uridhi ,Machimbo nyimbo zote hizo zikikamilika zitawekwa kwenye albam moja kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wao wawapo majumbani
Super D aliongeza kuwa bendi hiyo kwa sasa imesimamisha maonesho yake lakini watakapoanza sikukuu ya Idi mosi watatoa burudani katika ukumbi wa DDC Kariakoo idi pili watakua TTC Chang'ombe na idi tatu watavuka bahari kuelekea visiwa vya karafuu na kufanya onesho lao Zanzibar
Bondi hiyo kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbalimbali wameweka nia ya kukonga mashabiki wa bendi hiyo kwa kupiga nyimbo mpya na zazamani ili kila mtu apate burudani unajua bendi yetu kongwe lazima tutoe burudani za aina tofauta aliongeza Super D
Bendi hiyo iliyopata umarufu mkubwa miaka ya nyuma imewahakikishia wapenzi wake kurudi katika ubora ule ule kama ilivyokuwa awari


Tuesday, July 23, 2013

ISERE SPORTS YATOA JEZI KWA TIMU YA KILWA MASOKO


Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Isere Sports inayoshuhulika na uagizaji na uuzaji wa vifaa vya michezo,Abbas Isere (kulia) akimkabidhi jezi Katibu Mipango wa timu ya Fresh Niga ya Kilwa Masoko ,Maulid Mtika maarufu Milulu zenye thamani ya Sh. 350,000.


Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Vifaa vya michezo, Isere Sports imetoa jezi seti moja yenye thamani ya sh. 350,000 kwa timu ya Fresh Niga ya Kilwa Masoko inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu wilaya ya Kilwa.
Katibu Mipango wa timu ya Fresh Niga, Maulid Mtika akipokea jezi hizo jana alisema msaada huo ni mfano wa kuigwa na wafanyabiashara wengine wenye uwezo wa kusaidia kuibua vipaji vya vijana kwenye soka.
Mtika ambaye ni maarufu kwa jina la Milulu alisema imefika wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litafute njia ili lishuke mpaka ngazi ya wilaya kujua matatizo yanawakabili timu ili kutafuta vipaji vya wachezaji watakaochukua nafasi ya waliopo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
'Tunao vijana wenye vipaji vya kucheza soka kufikia ngazi ya timu ya taifa, kinachowanyima nafasi ya kuonekana ni vifaa vya michezo tunaomba TFF ishuke mpaka ngazi ya wilaya kuwasaidia vijana kukuza vipaji.
Alitoa wito kwa wadau wa michezo kujitokeza kusaidia timu ambazo hazina wafadhili lakini kuna vijana ambao wako tayari kuonesha vipaji vyao
Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema jana kuwa msaada huo ameutoa ili kukuza vipaji vya soka katika wilaya hiyo ambao wanahitaji misaada kama hiyo ili kuendeleza vipaji.

Friday, July 19, 2013

MREMBO WA MIS TZ APIGA PICHA ZA UTUPU, NI FATHIYA


WakatI maelfu ha waumini wa dini la Kiislam duniani wakiwa ndani ya mfungo mtukufu huku wengi wao wakitumia kipindi hiki kupunguza maovu yao kwa mola kwa kufanya ibada,Hali imekuwa tofauti aliyekuwa mshiriki wa shindano la kumtafuta Miss Utalii Taifa Faithiya Madoud amepiga picha chafu za kujidhalilisha pamoja na kumdhalilisha mwanamke wa kitanzania.
Picha hizo chafu kwa mara ya kwanza zilinaswa na Xdeejayz toka kwa chanzo chetu cha habari ambapo inadaiwa msichana huyo ambae ameanza kuonja radha ya ustaa kufuatia kufanya vyema kwenye filamu za Mrembo wa Facebook na Nimpende Nani ambapo filamu zote hizo amecheza kama staa.
Habari za uhakika toka kwa chanzo chetu klichofikisha cd nzima ya picha hizo mezani kwa mtandao huu hatari kwa kunasa matukio magumu kilisema kuwa msichana huyo ambae mapema mwaka huu alishiriki shindano hilo la Miss Utalii Taifa yaliyofanyika Mkoani Tanga. Lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kushika nafasi za chini lakini alichaguliwa kuwa balozi wa Hotel zote za Kitalii nchini Tanzania pamoja na Kule Zanzibar
Hata hivyo habari zaidi ziliendelea kusema kuwa bint huyo kabla ya kuingia kwenye umiss alikuwa ni msanii maigizo na ametamba sana kwenye filamu hizo kiasi cha kujizolea umaarufu mkubwa nchini.
Aicha chanzo hicho kilisema picha hizo ambazo nyingine ni mbaya sana ambapo blog hii imeshindwa kuzitundika zote kwa kuzingatia maadili kwa wasomaji wetu lakini ilidaiwa kuwa picha hizo alikuwa anapigwa na mwanamke mwenzake na ilionekana walikuwa Hotel na haikufahamika walifika kufata nini kwenye nyumba hiyo ya wageni.
Baada ya kupata picha hizo xdeejayz ilivuta waya moja kwa moja hadi kwa staa huyo mtarajiwa na kwa bahati nzuri simu yake ilipokelewa na yeye mwenyewe na haya ni mahojiano kati ya mwandishi wa Xdeejayz na mrembo huyo " Xdeejayz habari yako dada bila shaka naongea na Fathiya? " Ndiyo habari yako nani mwenzangu?"
Xdeejayz" 
Hapa ni ofisi za DTV kupitia blog ya Xdeejayz" Fathiya" Ndiyo nikusaidieni nini DTV?" 
"Xdeejayz ahsante sana Fathiya ofisi yetu imenasa picha zako za utupu hivyo tulitaka ufike ofisini kwetu ili kuzitambua kama inawezekana au thubitisha kama uliwahi kupiga picha na namna hiyo"
"Fathiya umesema wewe nani?
"Xdeejayz ofisi za DTV kupitia blog ya xdeejayz"
"Fathiya sasa kwani nani kawaletea hizo picha? mimi hizo picha nilipiga kwa matumizi yangu binafsi sasa nyie inawahusu nini lakini mbona waandishi wa Tanzania mnapenda kufatilia maisha ya watu? Sitaki kabisa mtoe picha zangu kwenye Tv yenu au gazeti la sivyo nitakufa na mtu sipendi kabisa ****** zenu" Alimalizia na tusi Fathiya kisha akaata simu.
Hata hivyo juhusi za kumtafuta Rais wa Miss Utalii Tanzania Gedion Chipungahelo hazikufanikiwa baadaya namba yake ya simu kushindwa kupokelewa.
XDEEJAYZ ina laani vikari tabia za mabint wenye tabia chafu kama hizi za kujipiga picha za kujidhalilisha bila sababu za msingi.
FROM:XDEEJAYZ

Thursday, July 18, 2013

HAPPY B'DAY TO MY HOMIE 'INOCENT MUJWAHUKI'

MUJWAHUKI ni mmoja kati ya maprojuza katika studio za M-Lab, Pia ni mahiri sana katika upigaji wa KINANDA 'Keyboards Player'

Wednesday, July 17, 2013

WAZEE WA TABORA WAKOMALIA MCHEZO WA BAO


Juma Shoka Salumu Dilunga Kushoto akicheza mchezo wa bao na Salumu Dilunga wakati walipokuwa maeneo ya Changamoto Mkoa wa Tabora jana mchezo huo uliozoeleka kuchezwa mikoa ya pwani imeleta chachu kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Tabora.
Picha kwa hisani ya  blog ya SUPER D

DUA KUTOKA KWA ZAHIR RASHID (Official Video)

Friday, July 5, 2013