Wednesday, July 31, 2013

IBRA WA 'WAKALI DANTA' AUAWA KWA KUCHOMWA KISU WAKIGOMBEA MWANAMKE


Marehemu Ibra enzi za uhai wake.
WAKATI Waislamu wakiwa ndani ya Mfungo wa Ramadhani, mapenzi yamemuua kijana Ibrahim Ibrahim ‘Ibra’ wa Kundi la Wakali Danta la Magomeni jijini Dar kwa kuchomwa visu.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 27, mwaka huu maeneo ya Magomeni Kagera ambapo ndugu wa Ibra, Ally Jumanne Sanane alidai kuwa, Ibra alichomwa kisu na kijana aliyefahamika kwa jina la Kelvin wakimgombea demu aitwaye Fatma Kiduku.
Mtoa habari huyo alidai: “Fatuma alikuwa ni mchumba wa Ibra lakini pia inaonekana alikuwa akitoka na Kelvin.
“Siku ya tukio Kelvin alikutana na Fatuma, akamuanzishia vurugu akimuuliza sababu ya kumuacha yeye ili aolewa na Ibra. Vurugu ilikuwa kubwa, Fatuma akaamua kumuita Ibra ili amsaidie.
“Ibra alipofika ndiyo akaanza kupigana na Kelvin, kuona amezidiwa Kelvin alitoa kisu na kumchoma cha kwanza kisha cha pili na ndiyo Ibra akaanguka chini na hakuamka tena,” alidai mtoa habari huyo.
Baada ya tukio hilo inadaiwa Kelvin na Fatuma walikimbia hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamepatikana. 
 Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 27, saa 9:30 eneo la Brazil Magomeni Kagera. 
Kamanda Wambura alisema kuwa Kelvin ambaye anahusika na mauaji hayo anasakwa na jeshi la polisi.
Mbali na Kelvin pia  mwanamke ambaye ndiye chanzo cha tukio hilo naye anasakwa.
Kesi hiyo imefunguliwa jalada namba MAG/IR/5600/ 2013 MAUAJI.
Uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea zaidi ili kuweza kuwakamata wahusika waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria
SOURCE-GPL

No comments:

Post a Comment