b..

B1

Wynem

animation

Monday, March 27, 2017

KIWANDA CHA SARUJI MOSHI CHAFUNGWA KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba alipotembelea kiwanda cha saruji cha Moshi. Kiwanda hicho kimefungiwa baada ya kutotekeleza maagizo waliyopewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Katikati ni Mwakilishi wa Kiwanda hicho Bi. Sophia na kushoto ni Dkt. Menan Jangu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kaskazini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ziara ya kikazi.
 Mtambo wa kudhibiti vumbi katika kiwanda cha saruji cha Moshi ambao haufanyi kazi ipasavyo, kumekua na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya uchavuzi wa hewa ufanywao na kiwanda hicho. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya Kaskazini ilitoa maelekezo ambayo hayakutekelezwa kikamilifu,  hivyo kiwanda hicho kimefungwa hii leo.


 Na Lulu Mussa, Moshi 
Ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba hii leo ametembelea Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Rombo. Akiwa Wilayani hapo Waziri Makamba ametembelea Kiwanda cha Saruji cha Moshi kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya uchafuzi wa hewa itokanayo na vumbi katika shughuli za uzalishaji.
Akitoa maelezo wa awali, Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo amesema kuwa Kiwanda hicho kimeendesha shughuli za uzalishaji wa sementi kwa kutofuata sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mfumo mzuri wa kudhibiti uchafuzi wa vumbi kiwandani hapo.
kwa upande mwingine Dkt. Menan Jangu Mratibu wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kaskazini amesema kuwa Ofisi yake awali ilitembelea kiwanda hicho na kutoa muongozo na taratibu zinazotokiwa kufuatwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
"Tuliwaelekeza kufanya yafuatayo, kujenga fensi kuzunguka eneo lote la kiwanda, kujenga "pevements" na kuweka mashine maalumu ya kuzuia vumbi kusambaa kwa wingi angani, vitu ambavyo havijafanyiwa kazi." Alisisitiza Dkt. Jangu
Mwakilishi wa Kiwanda hicho raia wa China aliyefahamika kwa jina moja tu Bi. Sophia, amesema kuwa suala la kuzungusha uzio eneo lote litatekelezwa pindi hati miliki ya ardhi ya eneo hilo itakapopatikana.
Waziri Makamba aliagiza NEMC kukifunga kiwanda hicho mpaka mapendekezo yaliyotolewa na Baraza yatakapokamilika. "Kiwanda hiki kisitishe shughuli za uzalishaji mpaka pale vigezo vya Sheria ya Mazingira vitakapokamili"
Katika hatua nyingine Waziri Makamba ametembelea Ziwa Chala na kuwataka wadau wa mazingira kuongeza jitihada katika kulihifadhi  kwa kuwa ni muhimu kwa ikolojia na historia yake. " Kina cha ziwa hili kinashuka kwa kasi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na sisi kama Serikali tutahakikisha tunawekeza nguvu zetu katika kunusuru kina cha ziwa hili kisiendelee kushuka" Alisisitiza Makamba.
Waziri Makamba ameahidi kuzungumza na Serikali ya Kenya ili kuwa na mikakati ya pamoja ya kuhifadhi ziwa hilo kwa kukuwa lipo pande zote za nchi hizi. Ziwa Chala ni chanzo kikubwa cha utalii na limetokana na mlipuko wa Volcano likiwa halitoi wala kuingiza maji kutoka vyanzo mbalimbali.
Waziri Makamba amemaliza ziara yake Mkoani Kilimanjaro na hii leo amewasili Mkoani Arusha. 

Friday, March 24, 2017

Prof Mbarawa alivyopamba sherehe za miaka 100 za benki Standard Chartered

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 100 ya shughuli za Benki ya Standard Chartered nchini, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa juu wa benki hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na wateja wakiwamo wafanyabiashara wakubwa nchini.
 WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (pichani kushoto) akishiriki hafla ya  maadhimisho ya miaka 100 ya shughuli za Benki ya Standard Chartered nchini, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa juu wa benki hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na wateja wakiwamo wafanyabiashara wakubwa nchini. 
Baadhi ya viongozi wa juu wa benki Standard Chartered nchini kutoka sehemu mbalimbali Duniani pamoja na wateja wakiwamo wafanyabiashara wakubwa nchini wakifuatilia yaliyokijiri ukumbini humo.Baadhi ya viongozi wa juu wa benki Standard Chartered nchini kutoka sehemu mbalimbali Duniani pamoja na wateja wakiwamo wafanyabiashara wakubwa nchini wakifuatilia yaliyokijiri ukumbini humo.
Wageni waalikwa mbalimbali Baadhi ya viongozi wa juu wa benki Standard Chartered nchini kutoka sehemu mbalimbali Duniani pamoja na wateja wakiwamo wafanyabiashara wakubwa nchini wakifuatilia yaliyokijiri ukumbini humo.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza  Mshauri wa  Uchumi wa Ubalozi  wa Ufaransa  Bi. Beatrice Alperte, Ikulu jijini Dar es salaam. alipokuwa akifanua jambo mapema leo , Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Balozi wa  Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak  alipokuwa akifanya mazungumzo nae mapema leo, Ikulu jijini Dar es salaam.

WANA CCM ZAIDI YA 400 WAJITOKEZA KATIKA OFISI ZA CCM LUMUMBA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI


Thursday, March 23, 2017

NAPE NNAUYE AKUTANA NA VIKWAZO KATIKA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI

Mfanyakazi wa hoteli ya Protea, Suleiman Kapase akizungumza na waandihishi wa habari mara baada ya kutangaza kuwa mkutano wa Nape Nauye na waandishi hautokuwepo hotelini hapo na kuwataka waandishi kusambaa
Mh. Nape Nnauye akuzungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli ya Protea mara baada ya kuwasili hotilini hapo na kuzuiwa kuingia katika hoteli hiyo kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari.
Gari la kamanda wa polisi wa Kinondoni likiwa limeblok gari la Mh. Nape Nnauye asiondoke eneo la tukio

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadaam, Hellen Kijo Bisimba (kushoto) akishuhudia kinachoendelea kwenye mkutano wa Mh. Nape Nnauye.
Mh. Nape Nnauye akuzungumza na kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni (yupo garini) baada kamanda huyo kufika katika mkutano huo kwa ajili ya kuzui Nape asizungumze na wanahabari.
Mh. Nape Nnauye akirudi kwenye gari lake mara baada ya kumaliza kuzungumza na kamanda wa mkoa wa kipolisi Kinondoni.

Picha zote na Suleima Salum.