Sunday, September 30, 2012

CHEKA AMGARAGAZA KALAMA KWA K.O RAUNDI YA SITA

Bondia Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa
Fransic Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita
Mabondia Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya sita
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, September 25, 2012

KIDEDEA  WATAKA SANAA YENYE UJUMBE KWA JAMII.

Wasanii kikundi cha Chemchem Arts wakiigiza mchezo mfupi kuonyesha nguvu ya sanaa za maonyesho katika kufikisha ujumbe, kwenye Jukwaa la sanaa Jumatatu iliyopita.
Wasanii wa kikundi cha Chemchem Arts maarufu kama Kidedea, wakiwa jukwaani wakati wakionyesha mchezo wao uliokuwa na lelo la kuonyesha jinsi sanaa za jukwaani zinavyoweza kufikisha ujumbe.
**********************
Na Mwandishi Wetu
KIKUDI cha Chemchem Arts Group, maarufu kwa jina la Kidedea kimelezea umuhimu kwa wasanii hapa nchini kuandaa michezo ya kuigiza itakayokuwa na ujumbe mahsusi utakaoisadia jamii ya Tanzania kutafakari juu ya muskabali wa masuala mbalimbali  yanayoendelea hapa nchini.
Akitoa wasilisho katika Jukwaa la Sanaa Katibu wa Kikundi hicho Christian Kauzeni amesema moja kati ya mapungufu makubwa ya sanaa za hapa Tanzania ni kushindwa kufikisha ujumbe utakaoifanya jamii kupata hisia, kuamka na kuchukua hatua juu ya masuala mbalimbali yanayowakabili wanajamii.
Marta baada ya wasilisho lake lililoeleza changamoto na mafanikio ya kikundi hicho katika ufanyaji wa sanaa, kikundi hicho kilionyesha mchezo mfupi wa kuigiza  uliojadili pamoja na mambo mengine tabaka lililopo kati ya tajiri na masikini.
Mchezo huo ulionyesha jinsi wananchi walivyo na hasira ya kuhukumu na kuwauwa vibaka  na wezi wa kuku huku wakiwaacha mafisadi wanaolihumu taifa wakiendela kutamba na magari ya kifahari. Mchezo ulilenga katika kuwapa tafakari watazamaji juu ya namna ya kuchukua hatua katika kukabiliana na masuala mbalimbali yanayojitokeza katika maisha ya kila siku  hapa nchini.
Wakichangia mara baada ya wasilisho na mchezo huo, baadhi ya wadau wa masuala ya sanaa wameeleza umuhimu wa jamii kuamka na kuchukua hatua stahili juu ya masuala muhimu badala ya kuacha mambo makubwa kupita na kuisha kirahisi na badala yake wahoji kwa kina kwa viongozi waliowachagua.
Akijibu hoja za washiriki, Kauzeni alisema ni muhimu sana kwa watu kushiriki michakato mbalimbali ya maamuziki ikiwa ni pamoja na kuhudhuria vikao vya serikali za mitaa kwani huko ndiyo wananchi wanaweza kuanza kuleta mapunduzi ya kweli kwa kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa.

IMAGE PROFESIONAL YAANDAA MASHINDANO YA KUCHORA

Image Profession ikishirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa mara nyingine inatangaza kuanza kwa muhula mpya wa pili wa Shindano ya Uchoraji maalumu kwa Taasisi za elimu.
Shindano ambalo pia linajulikana Kama: Educational Drawing Competition au Image Profession Educational Drawing Competition, lina malengo ya kuibua vipaji katika fani ya uchoraji kwa kuzingatia uwekezaji kwa watoto na vijana.
Theme/Wazo kuu la mwaka huu: ART IMITATES LIFE au SANAA HUFUATISHA MAISHA
Makundi ya ushiriki
Chekechea, 
Elimu ya Msingi, 
Elimu ya Sekondari na  
Elimu  ya Juu 
Kwa maelezo na taratibu za Shindano tembelea Facebook Page/Group “ HYPERLINK "http://www.facebook.com/groups/340300676062057/" Tanzania Drawing Competition” au wasiliana na BASATA au 
DRAWING COMPETITION – IMAGE PROFESSION,
P O BOX 92 DAR ES SALAAM.
SIMU: +255 222 664 740 / +255 713 484 040
/ +255 714 676 217 / +255 716 430 084
EMAIL:  HYPERLINK "mailto:info@imageprofession.com" info@imageprofession.com


Monday, September 24, 2012

KIKUNDI CHA SHADA CHAFANYA KWELI TAMASHA LA BAGAMOYO JIONI HII

Wasanii wa Kikundi cha Shada, wakifanya onyesho la sarakasi katika ufunguzi wa tamasha la kimataifa la Sanaa Bagamoyo. Tamasha hilo limefunguuliwa rasmi Jumatatu na litaendelea kwa siku tano hadi Jumamosi ijayo
Wasanii wa kundi la Jeshi wakifanya onyesho la Mzingaombwe katika Tamasha la Sanaa la Bagamoyo.
 Picha kwa hisani ya CAJAtz

ASKOFU MOKIWA ANUSURIKA KIPIGO KUTOKA KWA WAUMINI, AOKOLEWA NA POLISI


Waumini wa Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga jana wakipiga kelele kupinga uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi. Picha zote na Mussa Mwangoka
Mmoja wa waumini wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote la mjini Sumbawanga akiwa na jazba wakati wa vurugu zilizoibuka jana mara baada ya kutolewa uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi.
Askofu Mkuu wa Angikana Tanzania, la Dk. Valentino Mkowa aliyevuliwa kofia ya kiaskofu akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia wakimtoa nje ya Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga baada ya kuzuka kwa vuguru kubwa jana.
Picha na habari zaidi nenda http://kajunason.blogspot.com/

MCHEZO WA ATALANTA KUTIKISHA TAMASHA LA BAGAMOYO


Na Mwandishi Wetu
KUNDI la Das Letzte Kleinod (PICHANI) kutoka Ujerumani kesho (Jumanne) litafanya onyesho la mchezo ya kuigiza  wa ATALANTA unaozungumzia masuala ya Utekaji nyara na uharamia  wa utekaji wa meli katika Pwani ya Somalia.
Mchezo huo ambao umelenga kualezea masuala mbalimbali ikiwemo madhara yatokanayo na uharamia huo unaofanyika katika Pwani ya Somalia kwa zaidi ya Miaka 20, utaonyeshowa katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo na baadaye utaonyeshwa kwenye ukumbi wa Goethe Institute jijini Dar es Salaam ijumaa.
Kwa mujibuwa Mratibu wa Kikundi hicho Juliane Lenssen, mchezo huo  wa ATALANTA umeandaliwa kutokana na ripoti iliyotokana na utafiti uliofanywa na mwandishi na muongozaji wa mchezo huo Jens-Erwin Siemssen katika pwani ya Somalia, na pwani za Afrika Masharki.
Amesema kundi hicho kimepata mwaliko wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuja Tanzania kuonyesha mchezo huo ambapo pia umshirikisha wasanii wawili kutoka Tanzania, mmoja kutoka Kenya na wengine kutoka Ujerumani.
Huu ni mchezo wa pili kwa kikundi hiki kutengeneza kuhusisna na masuala mbalimbali ya Afrika ambapo mwaka 2007, kikundi hiki kiliandaa mchezo wa Mkono wa Damu ambao ulikuwa ukizungumzia masuala mbalimbali ya utumwa  ambao ulionyesha katika nchi mbalimbali na kwa hapa Tanzania ulionyesha katika miji ya Bagamoyo na Zanzibar.
mwisho.

BONDIA THOMASI MASHALI ACHUKUA SEHEMU YA FEDHA YAKE KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MPAMBANO WAKEThomasi Mashali akiwa na mkanda wake wa Ubingwa wa Taifa unaotambulika na TPBO
Bondia Thomasi Mashali akitia saini ya kuchukua kiasi cha pesa kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake wa kugombania ubingwa wa Afrika Mashariki October 14
RAIS wa -TPBO YASSIN ABDALLAH -USTAADH 'kushoto' akimkabizi bondia Thomasi Mashali sehemu ya fedha kwa ajili ya malipo ya kujiandaa na mpambano wake wa ubingwa wa Afrika Mashariki dhini ya Med Sebyala kutoka Uganda mpambano utakaofanyika October 14.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Saturday, September 22, 2012

NEY WA MITEGO: HATA 'JB' NAMCHUKULIA KAMA WAIGIZAJI WA BONGO MOVIE TU!

Msanii wa muziki hapa nchini, Ney wa Mitego (pichani) amemuangushia bomu muigizaji wa filamu nchini, Jacob Steven aka JB kuwa hana tofauti na waigizaji wa Bongo Movies anaowachukulia kama vicheche.
Kauli hiyo ameitoa juzi (alhamisi) kwenye kipindi cha Ho
t Mix cha EATV baada ya kukwaruzana na JB jijini Mwanza walipokuwa kwenye ziara ya Fiesta. Inadaiwa kuwa Ney alimwita Wema kicheche jukwaani jambo lililomfanya muigizaji huyo kukwaruzana na Ney.
“JB alikuwa kama mtoto mdogo au ulifika time wacha tu niliongee hili,” alisema Ney.
Ilifika time nikasema JB simtofautishi na wale akina Aunty Ezekiel sijui akina Wema kwasababuunajua mtoto wa kike ni dhaifu unajua, mimi nilimsamehe Aunt Ezekiel na Wema pia, sababu Wema na Aunty Ezekiel ni watu waliotaka kugombana na mimi, niliwasamehe palepale.
Nachokisema sio kama nabahatisha, nakuwa na uhakika nacho.
 JB na Ray ilibidi waungane pamoja wanifuate, ‘bwana unajua mimi ni dogo kwao’ lakini labda tunashindana tu vitu fulani, ukubwa wa umri si tatizo.”
Uhusiano mbaya kati ya waigizaji wa filamu nchini na Ney ulianza baada ya rapper huyo kudai kwenye wimbo wake‘Nasema Nao’ kuwa makahaba wenye kiwango wapo kwenye Bongo movies.

Friday, September 21, 2012

SAKATA LA STUDIO YA JK LAIBUKA TENA

Sugu
Mwana FA
Amoss Makala
************************
Mwandishi Wetu

SIKU moja baada ya Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala kusema studio iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete ianze kufanya kazi katika nyumba ya kukuzia vipaji ya THT, Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amemshangaa na kudai kuwa hayo ni maeneno yake binafsi na sio ya Serikali.
Sugu alisema kuwa Makala hajamshangaza tu yeye hata wabunge wenzake wa CCM akiwamo mwenyekiti Kamati ya bunge, Jenister Muhagama.
"Nikiwa kama Waziri Kivuli nimemshangaa sana Makala yeye ndio alisema juzi kwenye bunge la bajeti kuwa studio imemchafua sana rais hivyo kuna utaratibu unafanyika ili irudishwe kwenye mikono ya Basata na itumiwe na wasanii wote," alisema Sugu.
Alisema,"alipigiwa makofi mengi sana Bungeni, kuna nakala alinionyesha za maofisa wa Wizara zilizoonyesha mlolongo mzima wa utoaji wa studio umegubikwa na utata mkubwa na aliniahidi kulivalia njuga kikamilifu mpaka Muhagama akamsifu na kusema Makala kiboko, naamini hata yeye kama amemsikia Makala akisema tena studio ni ya THT atamshangaa."
Kauli ya Sugu imekuja siku moja baada ya Naibu Waziri huyo wa Habari kutembelea ofisi za THT zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuhoji studio hizo mahali zilipo na kuambiwa zimehifadhiwa Masaki.
"Mwana Fa vyombo vya studio vipo wapi?," aliuliza waziri Makala.
Mwana Fa, "Vipo Masaki vimehifadhiwa kutokana na utata uliotokea wa kina Sugu"
Makala alisema, "Hivyo vyombo vifungeni vianze kufanya kazi haviwezi tu kukaa siku zote hizo, vifungeni mvitumie ni vya kwenu hivyo mmepewa nyinyi na Rais, haiwezekani Rais akatoa studio kwa wasanii wote, mmesikia ni vya kwenu hivyo."
Lakini jana Sugu alisema atahakikisha analivalia njuga suala hilo hadi vifaa hivyo virudishwe Basata ili vinufaishe wasanii wote na kuhoji kuwa kilichombadilisha Makala msimamo wake ni kipi hadi kugeuka matamshi yake aliyoyatoa kwenye bunge la bajeti  lililomalizika siku za karibuni.
Akizungumzia suala hilo  Katibu Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya (TUMA) Fredy Malik 'Mkoloni' alisema "Tunaamini alichokisema Makala ni kauli yake binafasi na si ya serikali hivyo haina mashiko, amesahau kabisa alichokizungumza bungeni, tunajipanga na kutoa tamko letu rasmi.

Thursday, September 20, 2012

FLAVIANA MATATA ANG'ARA KWENYE WIKI YA MITINDO JIJINI LONDON

Picha tofautitofauti za Flaviana Matata, akipita jukwaani wakati wa Onyesho la mitindo, jijini London, jana.

DJ NIJO KUTUA DAR KUPIGA SHOO KALI

The Hyped East Africa Show will be travelling to Dar es Salaam.  Hyped East Africa is the first ever travelling entertainment show that showcases the hottest clubs in Cities around East Africa.  The show introduces to us the hottest VJ’s and celebrities who rock those cities while showcasing the best music videos from across the world.
DJ Nijo will be travelling to Dar to showcase the hottest clubs in Dar es Salaam in the coming week.
· Friday 28th September 2012, Club Sun Ciro in Sinza
· Saturday 29th September 2012, Nyumbani Lounge, Kinondoni.

NJAA YA ASUBUHI NI NOMA, CHAI YA KIOFISI OFISI

Hapa mtu mzima 'Mtoto wa kitaa' nkipata kitu cha chai asubuhi hii hapa ofisini 'news room' kwetu. NJAA NOMAAAAA

Tuesday, September 18, 2012

SUPER D ASIKITIKA MASHINDANO YA NGUMI TAIFA KUKOSA WAFADHILI

KOCHA wa timu ya Ashanti na timu ya Mkoa wa ILala Kimichezo Rajabu Mhamila 'Super D' (pichani) amesikitishwa na kitendo cha mashindano ya taifa kutokuwa ata na mzamini mmoja ambapo mashindano hayo ndio dira ya maendeleo ya mchezo huo hapa Tanzania.
Akizungumza kwa uchungu wakati wa mashindano hayo yanayoshilikisha mikoa 18 iliyoanza siku ya jumatat amesema nasikitika sana mikoa karibia yote ya Tanzania bara hipo hapa inashiriki mashindano haya ya Taifa inakosa ata mzamini ambapo katika mkusanyiko huu watu wengi wanaweza kujitangaza karibia mikoa yote nchini kupitia mchezo huu.
Wadhamini wamekuwa wakigombania dhamini mchezo mmoja tu wa mpira wa miguu na kugombana kufaa jezi za mpinzani na mwingine kumwambia asivae jezi hizo lakini mbali na kupelekewa barua katika makampuni mbalimbali ya kuzamini mashindano makubwa ya mchezo huo mchini barua hizo zimekuwa zikiwekwa kapuni na kama Ufadhili basi upatikana mdogo ambao sio wa kutarajia nasikitika mpaka sasa mashindano yapoendelea akuna ata zawadi za mshindi ukiangalia mabondia wengi kutoka mikoani wamekuja kwa galama zao kwa kila kitu ikiwemo usafili maradhi na kazalika na kama timu hizo zikishinda awana kitu chochote cha kumbukumbu ya kuludi nayo mikoani mwao kwa ajili ya kuwaonesha wenzao waliokuwa wakiwaombea duwa kuwa mkoa wao ushindeInasikitisha sana nchi yenye lasilimali ya watu wengi wanashindwa kusaidia mchezo wa ngumi tena wa taifa bali wamekuwa wakitoa sapoti katika mambo mengine ambayo ayana ata mwelekeo ikiwemo michezo kazaa ambayo aina ata vyama ikiwemo mbio za Mbwa za mbuzi na kazalika michezo hiyo aina ata vyama inavyo visimamia lakini BFT walipepeka maombi mbalimbali ya kuwa kuna mashindano ya ngumi ya taifa makampuni yapatayo 30 na kukosa ufadhili wa aina yoyote ata maji ya kunywa akuna ambapo vijana wapandapo ulingoni utumia maji kila mwisho wa raundi.
Katibu Mkuu wa BFT Makore mashaga ambaye alijitolea kufatilia ufadhili katika makampuni 30 mbalimbali na kukosa ufadhili wa aina yoyote ile na kusababisha mashindano hayo kuendeshwa kwa ugumu.
Super D ambaye ni kocha wa timu ya mkoa wa kimichezo Ilala pamoja na viongozi wenzie wa mkoa uho wamekuwa wakiangaika uku na kule kutafuta ufadhili yapo mdogo kwa mabondia ukiwemo wa nauli za kujikimu kwa mabondia wa mkoa huo ambao unawakilishwa na mabondia watano wanaoishi sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam na kukosa ufadhili-- Super D Boxing Coach

Monday, September 17, 2012

WASANII WATAKAKIWA KUTUMIA MAWASILIANO KWA MANUFAA

Mkurugenzi wa Idara ya Utafidi, Mafunzo na Habari wa BASATA, Godfrey Lebejo, akizungumza katika Jukwaa la Sanaa jumatatu, kulia ni Katibu Mkuu wa CAJAtz, Hassan Bumbuli na kushoto ni Mtoa Mada, Benedict Chale kutoka TPDA.
************************
Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wametakuwa kuboresha namna ya utumiaji wa njia mbalimbali za mawasiliano zinazopatikana hapa nchini na katika maeneo yao ili kujitangaza na kutafuta masoko ya kazi zao.
Hayo yamesemwa katika Jukwaa la Sanaa, na Mkurugenzi wa Kituo cha Wakala wa Maendeleo ya Biashara  Tanzania (TPDA), Benedict Chale wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa Mawasiliano katika Sekta ya Sanaa hapa nchini.
“Tunatumia vipi fursa kubwa ya mawasiliano iliyopo katika shughuli zetu za sanaa? Hili ni swali la msingi, ukweli ni kwamba kumekuwa na tatizo la jinsi ya kutumia fursa hizi za mawasiliano kiufanisi. Ni muhimu sana wasanii wakaboresha namna ya kutumia haya mawasilinao katika kufanikisha kazi, kujenga mtandao, kutafuta na kuimarisha masoko na mambo mengine ya muhimu,” alisema Chale.
Alisema licha kuwepo kwa unafuu mkubwa katika mawasiliano kuanzia katika simu hadi intanet bado wasanii wanashindwa kutambua mbinu hasa za kutumia nafasi hiyo kufanya mawasilino yatakayowaletea manufaa zaidi na kuwataka kubadilika.
“Nawaomba wasanii washiriki pia katika maonyesho ya kazi mbalimbali za wasanii wengine na wajasiliamali,  kufanya hivyo ni kuongeza wigo wa mawasiliano, wengi wakiona ni maonyesho na picha basi mwigizaji haendi, basi isiwe hivyo, tenga muda nenda kunafaida fulani utaipata tu,” alisema.
Akihitimisha mjadala wa Jukwaa la Sanaa, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa BASATA Godfrey Lebejo, alitoa wito kwa wasanii kutumia pia fursa ya uwepo wa mawasiliano rahisi kujitafutia maarifa  na ujuzi kutoka katika mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na kujenga urafiki na wasanii katika maeneo mbalimbali Duniani.

Sunday, September 16, 2012

MSONDO NGOMA YAENDELEA KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE PANDE ZA ILALA

Waimbaji wa bendi ya Msondo Ngoma wakiimba wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kushoto ni Shabani Dede na Eddo Sanga
Wapiga Magitaa wa bendi ya Msondo Ngoma wakifulumusha burudani wakati wa bendi hiyo ilipotumbuiza katika ukum bi wa Max Bar Ilala Bungoni  kushoto ni Abdull Ridhiwani na Zahoro Bangwe 
Mpigas Drams wa msondo ngoma Saddy Ally akiwajibika katika onesho la bendi hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa max bar Ilala Bungoni.
Waimbaji wa Bendi ya Msondo wakitoa burudani kushoto ni Eddo San ga na Juma Katundu
Picha zote na www.burudan.blogspot.com

CUF WAFANYA HARAMBEE JANGWANI, WACHANGISHA MILIONI 62 CASH


PICHA hizi ni baadhi ya matukio pale katika viwnja vya jangwani.
Picha na www.mjengwablog.com

Tuesday, September 11, 2012

MASHINDANO YA NGUMI IA UBINGWA WA TAIFA 2012.


SHIRIKISHO LA NGUMI LA TAIFA (BFT)


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
          YAH:-MASHINDANO YA UBINGWA WA TAIFA 17-22/09/2012.
Shirikishi la ngumi Tanzania (BFT)limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2012 yatakayofanyika kuanzia jumatatu ya tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) kila siku kuanzia saa 9.00 alasiri.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15/09/2012 lakini kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya kimichezo ya ligi ya mpira wa kikapu,sasa mashindano hayo yataanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 17/09/2012.
Lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa ,itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara.ili kuanza maandalizi ya mapema na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola 2014,mashindano ya Afrika 2015,mashindano ya olimpiki 2016,ubingwa wa dunia na mashindano mbalimbali tutayopata mwaliko kwa ajili ya kuwakilisha taifa.
Hadi  leo jumla ya mikoa kumi na nane (18) imethibitisha kuja kushiriki katika mashindano hayo,mikoa hiyo ni mikoa ya kimichezo ya Temeke,Kinondoni  na Ilala.Mingine ni Ngome ya JWTZ,JKT,Magereza na Polisi.Mingine ni Pwani,Morogoro,Mbeya,Ruvuma,Dodoma,Kigoma,na Bukoba.mikoa mingine ni Tanga,Arusha ,Tabora na Mwanza.
Uongozi wa BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha mashindano haya,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu ya taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema.mashindano hayo yana takiwa kufanyika kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=).
Sasa Mabadiliko ya ratiba ya mashindano itakuwa kama ifuatavyo:-

TAREHE
MUDA
TUKIO
16/09/2012

Timu zote kuwasili dare s salaam.
17/09/20123
1.00-4.00 Asb
4.00-5.00 Asb
5.00-7.00 Mch
Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Zoezi la draw na bye na ratiba ya mashindano.
Semina kwa waamuzi,timu manaja,makocha kwa ajili ya kupatiwa kanuni na sheria za mashindano.
18/09/2012
1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Gwaride la ufunguzi na kuanza mashindano hatua ya mtoano
19/09/2012
1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea hatua ya mtoano
20/09/2012
1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea kwa hatua ya robo fainali
21/09/2012
1.00-2.00 Asb
2.30-8.45Mch
9.00-2.00 Usk
Kupima uzito
Mkutano mkuu  wa BFT(indoor stadium)
Mashindano kuendelea hatua ya nusu fainali
22/09/2012
1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk
Kupima uzito na afya.
Gwaride la kufunga na kuendelea kwa mashindano hatua ya fainali.
23/09/2012

Timu zote kuondoka

Aidha ajenda za mkutano mkuu wa wanachama wa bft ni mbili tuambazo ni kupitia na kupitisha rasmu ya katiba ya BFT na maandalizi ya uchaguzi wa BFT wa kuwapata viongozi makiniwa kuongoza BFT kwa kipindi cha miaka mine kuanzia marchi 2013 kwa mujibu wa katiba .

Monday, September 10, 2012

KOLABO LA UKWELI KUTOKA KENYA MPAKA BONGO

After a connection between Ezden The Rocker and Azma from Rock City, Tanzania with a female Emcee Laikkah, Orenge and General Maxima all from Nairobi, Kenya made on social networking sites specifically twitter landed to the idea of recording a collabo joint titled CONNECTION.
The beat/ Mixing were done in Tanzania by Tiddy Hotter, a producer from one music production houses in Mwanza called ONE LOVE FX. After the beat was done, it was sent to Nairobi for guys to jump on it then back to the Rock City again for the mixing process...and its now done!!!!
This joint is a special dedication to all the people residing in East Africa.

Sunday, September 9, 2012

KAMANDA NGURUMO AUNGURUMA NA MSONDO NGOMA NDANI YA MAX BAR USIKU HUU

Mwimbaji Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma Muhidini Gulumo kushoto akiimba sambamba na Hassani Moshi 'Tx Jr' wakati wa bendi hiyo ilipotumbuiza katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni Gulumo ni mwanamziki Mkongwe pekee aliyedumu katika Jukwaa kwa mda mrefu nchini ambapo hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na Maradhi yanayomkabili lakini kwa sasa karudi ulingoni kukonga mashabiki wa bendi hiyo msondo kila jumapili inatumbuiza katika ukumbi wa Max Bar
Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani wakati walipokuwa wakitumbuiza katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kutoka kushoto ni Muhidini Gulumo,Hassani Moshi na Shabani Dede.

NGOMA MPYA KUTOKA KWA ABASS KUBAF NA BENJAMINI WA MAMBOJAMBO

Tuesday, September 4, 2012

MB DOG SASA KUJITUPA KWENYE FILAMU

Mtu mzima Mbwana Mohamed a.k.a Mb Dog (pichani), ameamua kujitupia kunako tasnia ya uigizaji na kushiriki katika filamu inayokwenda kwa jina la Nankonda Wa Mikindani.
Katika filamu hiyo, Mb Dog, ameigiza akiwa mhusika mkuu huku akijinadi kuwafunika nyota waliopo katika tasnia ya filamu za Swahiliwood.
"Sanaa ipo katika damu, nilikuwa niingie katika filamu kipindi tu nyuma, lakini niliona nianze kwanza na muziki huku nikisoma mchezo wa filamu unaendaje," alisema.
"Kwasababu katika muziki ninafanya vizuri, sasa nakuja na katika filamu. Sina maneno mengi, watu wakae mkao wa kula kumwangalia Mb Dog."

Monday, September 3, 2012

JUKWAA LA SANAA LAMKUMBUKA MWANDISHI ALIYEUAWA IRINGA

Mwasilishaji wa mada katika jukwaa la Sanaa bwana Chediel Senzighe akisisitiza jambo wakati akitoa mada kwenye kongamano la Jukwaa la sanaa, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni Tanzania (CAJAtz) Hassan Bumbuli akizungumza katika Kongamano la Jukwaa la Sanaa hapo jana.kulia ni msanii Chediel Senzighe aliyekuwa muwasilishaji mada katika kongamano hilo.
************
Na Mwandishi Wetu
Kongamano la Jukwaa la Sanaa ambalo huendeshwa kila wiki, jana lilianza kwa kumkumbuka Mwandishi wa Habari na mwakilishi wa Kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi aliyefariki dunia juzi katika vurugu zilizotokea katika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa.
Kabla ya kuanza kwa kongamano hilo jana, Mwendeshaji wa kongamano hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni nchini, (CAJAtz) Hassan Bumbuli aliwataka  washiriki kusimama kwa dakika moja kumkumbuka mwandishi huyo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa.
Katika kongamano hilo ambalo jana lilijadili  mada ya Sanaa za jukwaani  na guvu yake katika kufikisha ujumbe kwa hadhira,  mwasilishaji wa mada hiyo Chediel Senzighe kutoka kundi la Jakaya Theatre, aliwakata wasanii kuandaa kazi kwa kuzingatia maadili  na kanuni ili kuepusha kuipotosha jamii.
“Sanaa ina nguvu sana katika kufikisha ujumbe, kama ni muuaji basi sanaa inauwezo wa kuua watu wengi kwa wakati mmoja, daktari akikosea katika upasuaji ataua mgonjwa mmoja, lakini maudhui ya kazi ya sanaa yakikosewa yanaathari kwa watu wengi na kwa wakati mmoja. Sasa ni vyema wasanii tukawa makini katika kuandaa kazi zetu na zaidi tufanye utafiti kabla hatujaamua kuandaa maudhui ya kazi zetu,” amesema Senzighe.
Wakichangia mada hiyo, washiriki wa kongamano hilo wamesema tatizo kubwa linalowakabili wasanii siku hizi ni uvivu wa kusoma na kujifunza na ndiyo maana wanaandaa kazi za kulipua huku akili zao zikiwaza fedha zaidi kuliko kufikiria wanachokipeleka kwa jamii kinaweza kuleta athari gani.
“Wasanii wetu lazima wabadilike sasa, wafanye utafiti kabla ya kuandaa sanaa  hasa sanaa za jukwaani au filamu hii itasaidia sana kuandaa maudhui mazuri ambayo pia yataisaidia jamii,” amesema Godfrey Lebejo Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, mafunzo na habari wa BASATA.
Awali wakati akifungua kongamano hilo, Katibu Mkuu wa CAJAtz, bwana Bumbuli, alieleza kusikitishwa na kifo cha kinyama kilichomtokea Mwandishi wa Channel Ten na kusema matumizi ya nguvu kupita kiasi ya jeshi la Polisi yanahitaji kukomeshwa mara moja hasa kwa kuwa yanagharimu maisha ya watu bila sababu za msingi.
“Inatusikitisha kama wanatsnia ya habari na kama Watanzania, nguvu za polisi zinaacha majereha makubwa kwa watu na sasa zinagharimu maisha ya watu, nguvu hizi hazina sababu na lazima zikemewe na kulaaniwa kwa nguvu zote,” amesema Bumbuli.

ILIVYOKUWA KWENYE VURUGU ZA POLISI NA WAFUASI WA CHADEMA MKOANI IRINGA JANA


Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

Daud Mwangosi (kulia, mwenye swta la rangi ya udongo) enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake, akichukuwa picha za video za tukio zima

Mwandishi wa Habari akijaribu kuchukuwa matukio

Askari polisi (FFU) akiondoka sehemu ya mlipuko
Askari wakimuinua mwenzao baada ya kujeruhiwa mguu
Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini

Mkazi mmoja aliyejeruhiwa akiwa ndani ya gari tayari kwa kupelekwa hospitali. 

*********************
Kwa hisani ya Vyombo vya habari mbalimbali
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo
Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari 
JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.
Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.
" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza
Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.
"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.
Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.
Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.

Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .
Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.
"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.
Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
MWISHO

Kwa habari zaidi tembelea