Thursday, November 17, 2016

BARAZA KUU YA UWT - IRINGA LAMPONGEZA MWENYEKITI WA CCM MKOA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA RAIS DKT MAGUFULIMbunge wa  viti maalum Mary  Chatanda  akisalimia katika kikao cha baraza  kuu la UWT mkoa wa Iringa 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu akifungua  baraza  kuu la  UWT  mkoa wa Iringa 
Marcelina Mkini mwenyekiti wa UWT  Mufindi  akitoa pongezi kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kulia  katikati ni mwenyekiti wa UWT mkoa  Zainab Mwamwindi na  kushoto ni mjumbe wa baraza hilo Hafsa Mtasiwa 
Wajumbe wa baraza kuu ya UWT  mkoa wa Iringa 
Msambatavangu  akiagana na wajumbe wa baraza   kuu la UWT mkoa  wa Iringa kutoka  kulia ni Mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini , mbunge wa  viti maalum  mkoa wa Iringa Ritta Kabati na Rose Tweve 
Wajumbe wa baraza  kuu la  UWT  mkoa wa Iringa  wakimpokea mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  wa tatu kushoto  akilakiwa na mbunge Rose Tweve  kushoto ni mwenyekiti wa UWT mkoa na mbunge wa  viti maalum Zainab Mwamwindi  na wa  pili  kulia ni mbunge Ritta kabati  akisalimiana na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina mkini  huku kulia ni katibu wa UWT mkoa 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu wa tatu  kushoto akiwa na viongozi  mbali mbali wa mkoa 
Mwenyekiti wa UWT  mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi akitoa salam za utangulizi
Na matukiodaimaBlog 
BARAZA  kuu  la  umoja  wa wanawake  mkoa  wa Iringa limempongeza mwenyekiti wa chama  cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa  kuwa  kiongozi  wa mfano ndani ya  mkoa na nje ya  mkoa wa Iringa na  hivyo  kumwomba  kugombea  tena nafasi  hiyo ya  uenyekiti mwakani 2017.
Akitoa pongezi  hizo  leo  wakati  akishukuru kwa niaba ya wajumbe wa baraza kuu la UWT  mkoa  lililokutana  kwenye  ukumbi wa CCM wilaya ya  Iringa mjini ,mwenyekiti wa  UWT wilaya ya  Mufindi Marcelina  Mkini ambae  pia ni mjumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM Taifa (NEC)  alisema  kuwa  ushindi mkubwa ambao CCM iliupata katika  uchaguzi mkuu mwaka jana  uchaguzi  uliomwezesha Rais  Dkt  John Magufuli  kushinda kwa  kishindo dhidi ya  wapinzani  wake ni pamoja na kazi  nzuri  iliyofanywa na Msambatavangu katika  kampeni  za uchaguzi mkuu .
Mkini  alisema  mkoa  wa Iringa kwenye  uchaguzi huo  uliweza  kufanya  vizuri kwa kushinda  majimbo 6 kata ya 7  yaliyopo ndani ya  mkoa  wa Iringa na kuwa  pamoja na kila  mmoja  kushiriki katika  kupigania ushindi  huo wa chama  ila  wao kama  wanawake  hawanabudi  kumpongeza mwanamke mwenzao ambae ndie mwenyekiti wa chama  mkoa kwa  kuonyesha Taifa  kuwa  wanawake  wanauwezo wa  kuongoza .
'' Naomba  kuchukua nafasi hii kwa niaba ya  wanawake  wenzangu  kukupongeza  sana mwenyekiti  wetu wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu  umeonyesha  mfano  mzuri kuwa unaweza kuongoza .......nakumbuka  wakati wa kampeni  wewe  ulisimama  kidete   kuhakikisha  chama kinashinda  kwa  kishindo  mbali ya figisu figisu zilizokuwa zikielekezwa kwao  ila hukuteteleka ''
Mbali ya mwenyekiti  kufanya  vema katika  kampeni  za 2015  ila  hajaacha  kuitumikia vema  jamii ya  mkoa wa Iringa ikumbukwe mkoa  umepata  misiba miwili mikubwa  ukiwemo wa  aliyekuwa mwenyekiti  mstaafu wa CCM  mkoa Tasili Mgoda na mwasisi wa maendeleo ya   wilaya ya  Mufindi Joseph  Mungai shughuli  zote  zimeratibiwa  vema na Msambatavangu tena  pasipo  ubaguzi  wowote .
'' Mwenyekiti   wetu  anafanya kazi  vizuri  ndani ya  mkoa  wetu  tena  pasipo ubaguzi wowote  na ni mtetezi  mzuri  sana kwa  wanawake  ndani ya  mkoa na hanaga unafiki kabisa  kwani  yeye  siku  zote  husema  kweli  tupu ''
Mkini  alisema   kuwa   kutokana na  utendaji  kazi wake mzuri  ndani ya  chama  wao  wanaona  bado  mwenyekiti huyo anauwezo  wa  kuwavusha wana CCM kwa miaka  mingine mitano ijayo  hivyo  kumshawishi  kuingia tena ulingoni  mwakani 2017 katika  uchaguzi  mkuu wa  viongozi ngazi mbali mbali za  chama.
Mwenyekiti  wa UWT  mkoa  wa  Iringa Zainab Mwamwindi akisoma tamko la  UWT  mkoa  wa Iringa kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt  Magufuli  alisema  kuwa   wao kama  wanawake wa CCM  wameendelea   kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt Magufuli na  kuwa  kubwa  zaidi  ni jinsi  Rais alivyoweza  kujibu maswali ya  watanzania  kupitia   mkutano wake  wahariri  wa  vyombo   mbali mbali  vya habari  hapa nchini.
.Kwa  upande wake  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa ,Msambatavangu  pamoja na  kupongeza  pongezi za baraza  hilo  dhidi yake  na  zile za Rais alisema atahakikisha pongezi za  wanawake hao zinamfikia Rais Dkt Magufuli  huku  akisisitiza  wanawake  kuendelea  kuongoza  nafasi zao kwa kujiamini  zaidi badala ya  kutanguliza  uoga usio  wa lazima .
Alisema  wakati  chama kinajiandaa kwa  chaguzi zake mwakani ni vizuri  wanawake  kuanza  kujipima ama  kuwapima  wale ambao wanaingia kuwania nafasi mbali mbali ili  kupata  viongozi wenye  uwezo wa kuwatumikia  wananchi hasa katika  kipindi   hichi  cha kujenga chama  chenye  nguvu na  uongozi wenye  uwezo wa kuendana na kauli  mbiu ya  Rais ya hapa Kazi  tu.
Kwani  alisema  wapo baadhi ya  watu  ndani ya  CCM kazi yao ni  kusubiri uchaguzi hadi  uchaguzi  kufanya kazi  za chama na kuwa  wanachama hao hawapo kwa  ajili ya  kuwatumikia  wananchi bali  wapo kwa ajili ya  kutumikia matumbo yao jambo ambalo halikubaliki  kwa uhai na  nguvu ya CCM .
Mwenyekiti   huyo  alisema   hivi  sasa  wananchi  wanauelewa mkubwa  juu ya siasa   na uongozi  hivyo ni lazima  wanaopewa nafasi za  kugombea  ni lazima  wawe wanakubalika katika  jamii  inayowazunguka   vinginevyo  chama  kinaweza  kuyumba iwapo  watu  wasio na sifa  watapewa nafasi za  kugombea hivyo  ni  vizuri  kuanza  kuwatafuta  watu  wanaofaa ambao hawapo  ndani ya  CCM kujiunga na CCM ili mbeleni  waje kugombea kupitia  CCM.
Kwani  alisema  hivi  sasa kote  duniani ni  vema  viwili  pekee  ndivyo vimebaki kuitwa  vyama tawala na  vyama  hivyo ni  nchini China na Tanzania pekee ila maeneo  mengine  yote  vyama  tawala  imeondolewa madarakani    kwa  kuwa CCM lengo lake ni  kuendelea  kuongoza ni  vizuri kila mwanachama na kila kiongozi  kuhakikisha anawajibika   vema kwa  wananchi kama ambavyo mwenyekiti wa chama Taifa Rais Dkt Magufuli anavyoliongoza Taifa kwa  faida ya  watanzania na  vizazi vijavyo.