Monday, March 31, 2014

RAIS KIKWETE AONGEA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA JANA USIKU


Rais Jakaya Kikwete akihutubia mamia ya Watanzania waishio Uingereza jana usiku alipokutana nao katika Ukumbi waSttavis Patida Center, Wimbley, London. Rais Kikwete yupo nchini Uingereza kwa ziara ya Kiserekali kwa siku tatu ikiwa ni mwaliko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Comeron.
Picha zote na IKULU

OFISA WA JWTZ AHUKUMIWA KIFUNGO JELA KWA KUGHUSHI


Na Mwandishi wetu
Mwanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Muhsin Kombo amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kughushi. 
Hakimu Mkazi Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, alitoa hukumu hiyo jana baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 19 na vielelezo vya upande wa Jamhuri pamoja na utetezi wa washitakiwa.
Kombo na mkewe Devotha Soko walikuwa wanakabiliwa na mashitaka sita ya kupanga njama, kughushi, kutoa taarifa za uongo na kujipatia Sh milioni 100 kwa njia ya udanganyifu.
Katika hukumu yake jana, Hakimu Lema alimuachia huru Devotha kwa kuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake na Kombo alitiwa hatiani kwa shitaka la kughushi.
Kombo ametiwa hatiani kwa mashitaka ya kughushi muhtasari wa kikao kilichofanyika Machi 25 mwaka 2008 akionesha kuwa, Devotha amechaguliwa na familia ya marehemu Awadh Ally kusimamia mirathi.
Katika mashitaka mengine ilidaiwa Mei 5 mwaka 2008 katika Mahakama  ya Mwanzo Sinza, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walitoa taarifa za uongo kwa Hakimu wa Mahakama.
Inadaiwa walitoa taarifa kwamba Ally alifariki mwaka 1986 na kuacha watoto wawili, jambo lililosababisha hakimu huyo kumteua Devotha kuwa msimamizi wa mirathi.
Aidha inadaiwa Januari 28 mwaka 2011, washitakiwa walijipatia Sh milioni 100 kutoka kwa Rukia Zidadu kwa madai ya kumuuzia nyumba yao iliyopo Kijitonyama katika kiwanja namba 281 block 46.

DK JOSE CHAMELEONE ANYANG'ANYWA GARI AINA YA ESCALADE KWA KUSHINDWA KULIPA KODI

Jose Chameleone amenyang’anywa gari yake aina ya Escalade na maofisa wa URA baada ya mamlaka hiyo kudai kwamba msanii huyo ameshindwa kulipa kodi yenye thamani ya shilingi milioni saba ya Uganda. 
Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la msanii huyo, maofisa wa URA waliikamata gari yake hiyo ya kifahari. 
Kwa mujibu wa mtandao wa Redpapper wa nchini Uganda,msanii huyo alijaribu kuwakatalia wasikuchukue gari lake akidai atakufa na mtu atakayeichukua lakini kauli hiyo haikufua dafu kwa mamlaka hiyo. “Hii ni gari yangu binafsi na nina haki yake, mtu yeyote akigusa Escalade yangu, nami tufe pamoja naye,” alidai Chameleone.
Hata hivyo Chameleone alidai kuwa hana tatizo lolote kulipa kodi lakini mamlaka hiyo haikutolea vigezo walivyotumia kupata jumla ya shilingi milioni 7 za Uganda ambazo ndizo pesa wanazomdai

Friday, March 28, 2014

KASEBA NA MASHALI WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO JUMAMOSI MARCH 29 PTA SABASABA


Bondia Japhert Kaseba akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Thomasi mashali kushoto mpambano utakaofanyika PTA Sabasaba kesho

Mabondia Thomasi Mashali kushoto na Japhert Kaseba wakiwa na mkanda ambao wataugombania katika ukumbi wa PTA sabasaba skesho

Promota wa mpambano huo Ally Mwazoa akizungumza mbele ya waandishi wa habari
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

COLONEL MUSTAPHA AWAOMBA RADHI WANAWAKE WA AFRIKA MASHARIKI BAADA YA KUPIGA PICHA ZISIZO NA MAADILI.

Baada ya Nyota Ndogo wiki iliyopita kufanya maandamano na wanawake wengine mjini Mombasa Kenya kupinga kile walichokiita ‘udhalilishaji dhidi yao’ uliofanywa na rapper Colonel Mustafa na kumtaka awaombe radhi, mkali huyo wa ‘Lenga Stress’ amekuwa mpole na kuomba radhi
Mustafa ameliambia gazeti la The Star la Kenya:
“Wana sababu za msingi kama wanawake. Nawaomba radhi wanawake wote wa Afrika Mashariki waliochukizwa na picha lakini ningependa kusema kuwa, wanawake kwenye picha hizo hawakulazimishwa kupose. Siku hizi uanamitindo umeingia kwenye kugeuza mwili kuwa sanaa.”
Picha zilizoleta utata ni zile alizopiga Huddah Monroe.

MMJKT MABINGWA WA NGUMI MKOA WA DAR ES SALAAM


Bondia Hamisi Mputeni kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Victor Njaiti wakati wa mpambano wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam juzi Njaiti alishinda kwa point.

Bondia Mohamed Chibumbuli kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Rashid  wakati wa mchezo wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam Chibumbuli alishinda kwa pointi mchezo huo juzi.
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu
TIMU ya MMJKT jana imeibuka mabigwa wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam baada ya kuvipiku vilabu nane vilivyoweza kujitokeza kushiliki mashindano hayo
na kutawazwa kuwa bingwa wa mkoa baadhi ya mabondia waliocheza fainal za mashindano hayo ni Hamisi Mrisho wa 'MMJKT' alisambalatishwa kwa pointi na bondia Oscar Richard wa 'Urafiki'   na Omari Mohamed wa urafiki akichezea kichapo kutoka kwa mwenzie John Mwambinga, na bondia anaekuja kwa kasi ya ali ya juu akitokea timu ya Ashanti ya ilala kwa sasa akichezea timu ya 'MMJKT' alifanikiwa kumpiga John Christian wa 'Mgulani' Saleh Abdallah wa mgulani alishindwa kutamba mbele ya  Undule Langson wa Magereza
nae Jacobo Agusteno wa 'mgulani' alishindwa kufulukuta mbele ya Bosco Bakari wa 'MMJKT' katika mpambano mwingine uliowakutaniasha Festo Ngabo wa Magereza alishindwa kutamba mbele ya Victor Njaiti wa 'mmjkt' nae bondia Mohamedi Chibumbuli wa magereza alimsambalatisha vibaya bondia Said Saleh wa 'mavituzi'
 akizungumzia maandalizi ya mabondia wa mkoa wa Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam 'DABA' Akaroli Godfrey amesema
kwa sasa mabondia wa timu ya mkoa wa Dar es salaam wapo kambini wakijiandaa na mashindano ya majiji yatakayoanza Kampala Uganda April 2 mwaka huu 
timu hiyo ambayo ipo na makocha wazoefu wakiongozwa na David Yombayomba ,Ferdnand Nyagawa mazoezi yanayofanyika kila siku mgulani JKT, wakisaidiwa na Mazimbo Ally na Kameda Antony 
timu hiyo ina maitaji mbalimbalio ikiwemo kambi pamoja na kupeleka timu Uganda ambayo itagalimu milioni 16 kwa ajili ya kwenda kwenye mashindano
hayo ambapo mpaka sasa wamenda sehemu mbalimbali ikiwemo makampuni na kwa watu binafsi
ata hivyo akuna mafanikio yoyote hivyo kuwaomba wadau wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kusaidia timu hiyo ambayo inakabiliwa na mashindano ya majiji 

Thursday, March 27, 2014

BATULI WA BONGO MUVI AFUNGUKA, WANOFANYA UFUSKA BONGO MUVI WANATUHARIBIA

Msanii wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuph  ‘Batuli’.

MSANII wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuph  ‘Batuli’ amesema tabia mbaya za baadhi ya wasanii wenzao ndizo zinazowaharibia na kuwafanya wote waonekane hawana maadili.

Akiteta na safu hii, Batuli alisema amekuwa akipata malalamiko kuwa hawatumii katika filamu zake za watoto Jenifer na Jamila waliokuwa wakifanya kazi na marehemu Steven Kanumba, jambo ambalo amelikanusha.

“Siwezi kuwanyima watoto nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, sema watu hawajui kilichopo nyuma ya pazia. Nimeshawahi kuwaita lakini wazazi wao wakawazuia kwa madai siku hizi bongo muvi ni ufuska tu na hakuna kazi kama zamani. Ilibidi nimchukue yule mtoto mwingine mvulana Patrick.

“Fikiri nafasi ya msichana inalazimishwa hadi anacheza mvulana ni tatizo. Wasichokijua watu ni kwamba, wazazi wao wanawazuia wakiogopa wataharibika. Wasanii tubadilikeni jamani,” alisema Batuli.

Chanzo: Kandili yetu blog.  

Wednesday, March 19, 2014

MGOMOWA BASI YA ABIRIA 'DALA DALA' WAENDELEA MKOANI MOROGORO


Hali si shwari mjini Morogoro leo hii ambapo madereva daladala wamegoma kutoa huduma kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kupinga faini kubwa wanazotozwa na mamlaka za usalama barabarani mkoani humo.Mwakilishi wetu mkoani Morogoro ataendelea kutuweka karibu na tukio hili kwa kadiri litakavyokuwa likiendelea. Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa updates za mara kwa mara.

Pichani ni baadhi ya wakazi wa Morogoro ambao leo asubuhi walilazimika kutumia usafiri wa vyombo visivyo rasmi kusafirisha abiria, ili kuwahi makazini


SOURCE: JUKWAA HURU  MEDIA PAGE

Monday, March 17, 2014

MALORI MAWILI YALIGONGANA MLIMA KITONGA NA KUFUNGA NJIA JANA


Lori likiwa limetumbukia kwenye korongo mlimani kitonga

Baadhi ya abiria wa kutoka sehemu mabalimbali wakisubiri lori lililoziba barabara kuondolewa baada ya kupata ajali ya kugongana na lori jingine kwenye mlima Kitongo.

Magari yakiwa yamesimama baada ya ajali hiyo ya malori kuziba barabara. Ajali hiyo ilisababisha magari mengi kuweka kambi kwa muda wa zaidi ya saa nne.

BONDIA MANNY CHUGA AJIANDAA KUMKABILI SELEMANI MOTTO MARCH 23


Kocha wa mchezo wa ngumi Kwame Mkuluma kushoto  akimwelekeza bondia Amani Bariki 'Manny Chuga' jinsi ya kupiga ngumi kwa shabaha wakati wa mazoezi yake yaliyofanyika katika klabu ya Biafra Mburahati kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Motto utakaofanyika March 23 katika ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam

Kocha wa mchezo wa ngumi Waziri Chara kushoto  akimwelekeza bondia Amani Bariki 'Manny Chuga'  jinsi ya kupiga beg wakati wa mazoezi yake yaliyofanyika katika klabu ya Biafra Mburahati kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Motto utakaofanyika March 23 katika ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam

Kocha wa mchezo wa ngumi Kwame Mkuluma kushoto  akimwelekeza bondia Amani Bariki 'Manny Chuga' jinsi ya kupiga ngumi kwa shabaha wakati wa mazoezi yake yaliyofanyika katika klabu ya Biafra Mburahati kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Motto utakaofanyika March 23 katika ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam.
 picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, March 12, 2014

"NEW AUDIO" UKWELI HALISI - NOVIC

Novic anayewakilisha Vyema Arusha katika Muziki wa Gospel ya Kisasa ana release ngoma kwa jina "Ukweli Halisi" ikiwa ni mkono juu ya beat ya Marekani na vocals pande za Noizmekah Production studios chini ya defxtro, bofya HAPA kuisikiliza/Kudownload

Tuesday, March 11, 2014

AJIRA MPYA ZA WALIMU KUTANGAZWA RASMI TAREHE 15.03.2014


Na Mwandhishi Wetu
Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).

Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.

Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.
Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira.

Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo. Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. 

Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.
Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.

IMETOLEWA NA
JUMANNE A. SAGINI
KATIBU MKUU

OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI

KUMRADHIII

Kutokana na usumbufu uliojitokeza kwa wasomaji wetu wa blog hii ya MTOTO WA KITAA kutokuwa hewani kwa muda tangu juzi ikiwa ni mwingiliano wa link nyingine tofauti, hivyo kusababisha usumbufu.
Timu nzima ya blog ya Mtoto wa Kitaa inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza
….Endelea kupata habari na burudika na blog ya matukio tofauti kutoka mtaani.
-- Team SULE'S INC & ENTERTAINMENT

Sunday, March 9, 2014

ILIVYOKUWA KWENYE NDOA YA BW. HAMZA KHAMIS NA BI MRIAM

Bw. Hamza alipokuwa akifungishwa ndoa
Bw. Hamza na Bi. Mariam mara baada ya kufunga ndoa
Baadhi ya ndugu wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi.
Sule Junior na Bw. Issah Miraji pia tulikuwepo katika kusababisha mpango mzima.
Picha na Sule junior na Alex Nyaganilwa