Friday, November 30, 2012

NGOMA MPYA KUTOKA OVER CLASIC MUSIC


ARTIST -      DON MAKOLELA
SONG   -     NITAUMIA (HABIBT)
STUDIO -     OVER-CLASSIC MUSIC
PROD   -      EIZER

Wednesday, November 28, 2012

WASANII WAMLILIA SHARO MILIONEA KWA WIMBO MMOJA - KAZA MOYO

Video ya kumuenzi marehemu HUSSEIN a.k.a Sharo Milionea huu wimbo umeimbwa na Shetta, Dayna Nyange, shilole mohamed, Cannal Top, Rich Mavoko, Shadoo, Amazon, Barnabas Elias, Stamina, Dan rock, Suma Mnazaleti, Eric Mlindima, Muba c, Seif

BONGO ALL STARS together we canAudio producer ni C9Kanjenje 
Video directed by Msafiri under KWETU studio
R.I.P Sharo Milionea tutakukumbuka daima milele 

Tuesday, November 27, 2012

TAMADUNI MUZIKI KUZINDUA SANTURI NNE KWA PAMOJA


2NDA MAN, RAYMOND WATOA WIMBO WA MAOMBOLEZO YA SHARO MILIONER (R.I.P SHARO MILIONEA) PRODUCED BY MANECKY

SHARO MILIONEA KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAO LUSANGA, LUSHOTO.

Sharo milionea - enzi ya uhai wake

MSIBA wa msanii nyota wa uchekeshaji hapa nchini, Hussein Mkiety, maarufu kama 'Sharomilionea' umegusa hisia za wengi, huku King Majuto akikimbizwa Hospitali baada ya kushikwa na presha, hivyo kutishia usalama wake.
Mtoto wa King Majuto, Hamza Majuto, aliimbia HANDENI KWETU kuwa hali ya baba yake inaendelea vizuri kutokana na kuumizwa zaidi na msiba wa Sharomlionea anayetamba katika ulingo wa filamu na muziki hapa nchini.
Msanii huyo alikufa jana saa mbili za usiku Maguzoni, kilimita chache na kijijini kwao Lusanga, wilayani Muheza mkoani Tanga, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria lenye namba za usajili T478 BVR Toyota Harrier kupinduka na kusababisha kifo chake.  
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Masawe, alikiri kutokea kwa msiba huo na kusema kuwa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Teule, Muheza, mkoani Tanga kwa taratibu za mazishi zinazopangwa na familia yake.
“Marehemu alikufa majira ya saa mbili za usiku kwenye barabara ya Segera alipokuwa anatoka Dar es Salaam kwenda Muheza, hivyo mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Teule, huku gari lake likihifadhiwa pia kwasababu haliwezi kutembea,” alisema Masawe.
Taarifa za kifo cha msanii huyo aliyeibukia hivi karibuni na kufanya vema katika ulingo huo zilianza kuzagaa saa tatu za usiku, ikiwa ni dakika chache baada ya kufariki katika ajali hiyo ya kusikitisha kwa nyota huyo.
Katika mitandao yote ya kijamii kuanzia saa tatu za usiku zilizagaa habari zake, huku kila mmoja kiwa na hisia tofauti zilizotokana na madai ya kifo cha msanii huyo, ambaye baadaye jeshi la Polisi lilithibitisha kwa kupitia Kamanda wake, Masawe.
Sharomilionea ameshacheza filamu nyingi za uchekeshaji na kujipatia sifa kubwa, ikiwamo ile ya Sharo Millionea, Imekula Kwako, Jini Mahaba, Porojo na nyinginezo zinazofanya vyema katika tasnia ya filamu nchini.
Katika filamu ya Jini Mahaba, Sharomillionea anayetamba pia kwa msemo wake wa ‘Umebug Men’, anacheza kama mtu maarufu anayekwenda kujitambulisha kwa wake zake (Kingwendu) na kushangazwa na hali zao za maisha.
Sharomillionea anamshangaa mama yake mkwe anavyochambua mboga za majani wakati yeye sio utaratibu katika maisha yake. “Huyu ndio mama yako Men? Mbona anachambua majani,” aliuliza huku anakunja mdomo wake na kujifuta uso.
Maneno hayo yanamuumiza mama yake mkwe na kuamua kumuita mume wake (Kingwendu) na kuja kushangaa Sharobalo alivyokuwa katika mueneko wa super Star na kujikuta akipagawa alipoanza kukejeliwa na mkwe wake.
Mbali na filamu hiyo ya Jini Mahaba, mkali huyo pia ametamba katika filamu nyingi pamoja na nyimbo mbili alizorekodi, huku pia akililiwa na wasanii wenzake kutokana na ushirikiano wake, mara baada ya kuibuka kisanii.
Wasanii wengi waliozungumzia kifo cha Sharomillionea wakiongozwa na Steve Nyerere, walionyeshwa kuchanganyikiwa kwa msiba wa msanii aliyeanza kutokea peupe na kutamba mno katika sanaa ya uchekeshaji.
Sharomillionea aliyetokea katika ubavu wa nguli wa vichekesho nchini, King Majuto, anazikwa kesho Jumatano, kijijini kwao Lusanga, huku wasanii wengi wakitarajia kuhudhuria msiba na mazishi ya nyota huyo aliyeipenda pia nyumbani kwao Muheza.
Habari kwa Hisani ya Kambi Mbwana, Dar es Salaam

Monday, November 26, 2012

MSANII SHARO MILIONEA AFARIKI KWA AJALI YA GARI

Sharo Milionea - Enzi ya Uhai wake
Mwili wa Sharo Milionea baada ya ajali

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Sharobaro, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza majira ya saa mbili usiku (usiku huu). 

Kampuni ya SULE'S INC. & ENTERTAINMENT NA Menejment nzima ya blog ya MTOTO WA KITAA tunatoa pole kwa familia ya sharo milionea, baraza la sanaa tanzania (BASATA) na wasanii wote kwa ujumla.

TAMADUNI MUZIKI YANDELEA KUSHIKA KASI

DUKE akiongea na wadau waliofika pale New Msasani klab juzi.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mchakato.
Ma MC wakionyesha uwezo kwenye TAMADUNI MUZIKI.

MWIGIZAJI JOHN STEPHANO KUZIKWA JUMANNE MAKABURI YA KINONDONI


JOHN STEPHANO- Enzi ya uhai wake

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwao Mwananyamala 'A'  jirani na Kopakabana Bar  jijini Dar es Salaam.

Marehemu John anaetarajiwa kuzikwa kesho siku ya jumanne Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam, 
John alianza kujiingiza katika Sanaa ya Uigizaji mwaka 2001 chini ya wasanii wenzake, Thea na Deo Shija na ilipofika mwaka 2008 alianza kuigiza filamu na hadi mauti yanamfika alikuwa njiani kutoa Filamu yake.
Pia Mtanzania yeyote atakae guswa na Msiba huu anaweza kutuma Rambi Rambi zake kupitia Namba ya Tigo Pesa za 0715541714 au 0718951355

Sunday, November 25, 2012

PATA MASAHIRI (LYRICS) YA WIMBO WA SIHITAJI MARAFIKI KUTOKA KWA FID Q.


SIHITAJI MARAFIKI
VERSE 1

Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani/
haijalishi ulikua na wangapi bali wangapi uko nao..
washkaji ambao... 
kosa lako lao wakati hauna mafa
wanaokufikiria wewe muda ambao
wenzao walionao wanafikiria wengine ndo wanao
now kupata washkaji ukiwa na pesa... ni rahisi
kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi mie sikufichi sihitaji urafiki na usupastaa
ukihit ndo unang'aa.. 
upishwe useat kwenye bar
upewe beat na lamar kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground
sikuhizi mabinti wanaomiss ni walionidiss mie sio mdau
wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mmwanza
ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za kwanza
U-N-I-T na prof Ludi walionifunza kukaza...
kwetu mbali.. sijui lini nitarudi? (C) Lokua kanza
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea
aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

VERSE 2
Na usupastaa huwa ni feki.. utakung'arisha ukiwa na Market
utakupatia senti,utapita juu ya red carpet
utageuka young & restless, utakupa wanawake
utakupa mafake brethrenz.. kisha utaenda zake
kwahiyo power its not permanent.. huwa ipo kwa muda tu
respect ur own conglomorete... fikiri kikubwa tu
masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru
wanazusha najiskia.. so im my own best friend
sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man
naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention, lakini sio tajiri wakuafford kuua true friendship
tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga/na hizi falsafa double double ajabu sio kinywa cha mjomba
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

VERSE 3

Rafiki wa kweli yukoje.. ni mkimya au anayechonga
yule aliyekupa jina? au pengine anayekuponda? anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?
au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?/ hakuna adui mbaya ka rafiki yako mwenyewe ambaye hajui.. ka yupo nawe.. au yupo kinyume na wewe/bora adui.. kama hachachawi utaenda muomba akuelewe
ka buibui.. naweka tandu mtaenda kando mzingue?
kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo
Inabidi tu uwaache wakuwatch kwenye kideo/unakula nao happy leo.. kesho wanamtaka mkeo/urafiki sitaki.. hauletagi maendeleo..
nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama nature
wachache niliowafanya wakang'aa wanayaweka maisha yangu in danger
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

Wednesday, November 21, 2012

MTOTO WA KITAA NASHOO LAV NA MAJEMBE YA UKWELI

Wanangu wa ukweli kuanzia kushoto ni Issah Habib (graphic designer wa mwanaanchi communication Ltd), Sule Junior (Mtoto wa kitaa) na Jerome Risasi (Producer wa vipindi wa Clouds Tv & Radio)

Tuesday, November 20, 2012

WASHINDI WA USAILI WA KATIKA SHINDANO LA UNIQUE MODEL SEASON II.

Wanamitindo 12 chipukizi walipita katika ussail wa shindano la Unique Model Season II, usaili huo ulifanyika juzi jumapili katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada. Picha na Mpigapicha wetu

Monday, November 19, 2012

SUPER D AENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MCHEZO WA MASUMBWI BURE KWA VIJANA


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi kupiga ngumi za tumbo huku akiwa ameingia ndani kwa mashambulizi zaidi wakati wa mazoezi.
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi ya kupiga ngumi uku akiwa amejikinga kwa kutumia bega uku ngumi yake ikiwa imenyooka wakati wa mazoezi yaliyofanyika ufukwe wa GYKHANA Dar es salaam jana
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza katika mazoezi ya ngumi ufukwe wa GYKHANA Dar es salaam jana.
Picha zote kwa hisni ya www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, November 16, 2012

MAISHA PLASS: WASHIRIKI KUMI KIKAANGONI


Na Julieth Kulangwa
BAADA ya wiki iliyopita kuhsuhudia washiriki wawili, Bereniki na Justin wakitolewa katika 'fake eviction', waliobaki walipendekezana na kujikuta kumi kati yao wakiingia kikaangoni.
Justin na Bereniki baada ya 'kula bata' walirejeshwa kijijini bila wenzao kuwa na taarifa hiyo, wengi walionekana machoni kuwafurahia wenzao waliporejea lakini mioyoni huenda walikuwa tofauti.
Kwani Bereniki ambaye alijiapiza kuwa atahakikisha mwaka huu mwanamke anachukua ushindi, hata baada ya kurejea aliendeleza maneno hayo huku akisisitiza kuwa harakati zinaendelea.
Haina ubishi kuwa Justin na Bereniki ni kati ya washiriki wenye nguvu kwa maana hiyo kurudi kwao kutakuwa kumewashtua wale ambao waliamini kuwa kikwazo kimeondoka.
Lakini kumbuka wiki hii pia itakuwa tofauti na wiki tatu za mwanzo ambapo washiriki wawili walikuwa wakiaga mashindano kwani safari hii watatu na wa mwisho wataondoka kijijini.
Washiriki waliongia kikaangoni ni pamoja na Rashid Ndunduke, Bahati Kisula, Dora Mhando, Swaumu Shaaban, Magret Msechu, Tatu Masoud, Saad Mohames, Gabriel Lwinga, Hidaya Abdallah na Jonathan Joachim.
Baada ya mtoano huu washiriki kumi nane watabaki na hakutakuwepo mwingine mpaka shindano hili litakapofikia tamati mwezi ujao.
Shindano lilianza likiwa na washiriki 26, mpaka sasa washiriki wanne walitolewa moja kwa moja na wengine wawili walitolewa na kurudishwa katika fake eviction wiki iliyopita.
Mshindi atakuwa mmoja tu ambaye atajishindia kitita cha shilingi za Tanzania milioni 20. Huyu atapatikana kwa kupigiwa kura nyingi na watazamaji.

Mashabiki kujishindia zawadi.......
'Fans'  wanaweza kujishindia zawadi nyingi zikiwemo fedha taslimu, kompyuta aina ya laptop na fursa adimu ya kutembelea kijiji cha Maisha Plus..
 Kushiriki, andika neno MAISHA kisha tuma kwenda namba 15678 na baada ya hapo yatakujia maswali rahisi kuhusu MAISHA PLUS, JIBU maswali yote. -- Unaweza kuwa mmoja kati ya washindi.

NGOMA MPYA KUTOKA KWA STIVE RnB Ft OMMY DIMPOZ - RADIO

SIKILIZA NA PAKUWA KWA AJILI YA PROMO TU

SIKU CHACHE BAADA YA NEY KUKANA KUWA NA UHUSIANO NA NISHA, PICHA ZA KIMAHABA ZABAMBWA MTANDAONI.

Ney wa mitego akiwa kwenye pozi za kimahaba na msanii wa bongo muvi, Nisha!
Ney alikana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo wa bongo muvi. Pia Ney aliwaponda wasanii wa bongo muvi hasa wa kike kwa kusema kuwa "ukitaka makahaba wenye viwango nenda bongo muvi"

ASIA DACHI (UNIQUE MODEL 2012) AWAASA MODELS KUJITOKEZA SIKU YA JUMAPILI KATIKA USAILI WA UNIQUE MODEL 2012

Asia dachi ambae ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji hilo baada kuvikwa mwaka 2010 ametoa wito kwa wasichana wenye vipaji vya uanamitindo kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili hii kwaajili ya usaili wa kujiunga na shindano hilo.
  Pia nawaomba wabunifu wa mitindo ya nguo kujitokeza kuwavalisha wanamitindo watakaokuwa wamechaguliwa kwani kwakufanya hivyo mtapata nafasi ya kujitangaza na kuunga mkono harakati za ukuaji wa sanaa ya mitindo nchini Tanzania. Ushirikiano mzuri umeonyeshwa na wabunifu nguli Asia Idarus na Gabriel Molel kwa kujitokeza na kuunga mkono harakati hizi za unique model 2012 ambapo inategemewa kuwa chombo pekee cha kukuza sanaa ya wanamitindo wachanga nchini Tanzania. Usaili huo utafanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada iliyopo msimbazi center kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa saba mchana.

Thursday, November 15, 2012

NASSIBU RAMADHANI NA FRANSIC MIYAYUSHO KUGOMBANIA UBINGWA WA WBF DESEMBA 9


Mwandaji wa mpambano wa ubingwa wa WBF Mohamed Bawazir katikati akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Fransic Miyayusho kulia wengine kulia ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo na Kushoto ni Mratibu Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi
Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho mpambano utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Bawazir
Amesema amewakutanisha mabondia hawo kutaka kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa hivyo amewataka watanzania kujitokeza kuwapa sapoti hususani kudhamini mchezo huo wa masumbwi ata kwa bondia mmoja mmoja kuwagea changamoto mbalimbali mabondia hawa vijana wana uwezo mkubwa wa kutangaza biashara mbalimbali kupitia mchezo wao wa masumbwi kwani makampuni mengi yamekuwa yakiupiga danadana mchezo huu ni mchezo kama michezo mingine nashangaa sana kuona tunakosa Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema atuhusiki na mchezo huo Wengine wanasema kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi awapewi kipaumbele kabisaa amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza siku ta 9 Desemba kuja kuangalia ngumi ili zisonge mbele watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni :-
Fadhili Majia VS Juma Fundi
Moh'd Rashid Matumla VS Doi Miyayusho
Ibrahimu Class 'King Class Mawe' VS Said Mundi wa Tanga
Fred Sayuni VS Deo Samweli
Hassani Kidebe VS Baina Mazola
Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri .
Mpambano huo umedhaminiwa na JB BELMONT HOTEL gazeti la Jmbo Leo, Times FM, Na wengine wameobwa kujitokeza katika udhamini huo kwa mawasiliano zaidi 
0716 332933
0784 426542
KWA AJILI YA KUTOA SAPOTI YA AINA YOYOTE PAMOJA NA USHAULI KATIKA MPAMBANO HUU

Monday, November 12, 2012

LORD EYES: NIMEJIPANGA KUIKABILI KESI ILIYOPO MBELE YANGU

Mweusi toka A- City, Lord Eyez amekutana na waandishi wa habari akiwa na wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa vifaa vya gari ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa zilizopita.
Lord eyez amesema yeye kwa sasa anaiachia mahakama ambayo ndiyo itaweza kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama hakuhusika katika wizi huo wa vifaa vya gari.
Wakili wa msanii huyo anayejulikana kwa jina la Peter Kibatala amesema kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiye mhusika wa wizi wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza mahakama ndiyo itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.
Hizi kauli za mweusi huyu na wakili wake zinaonekana zimepimwa na ruler ya kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi ambayo iko mahakamani (commenting on a pending case).
Weusi nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma zinazomkabili member huyo na kwamba tukio hili limewaathili hasa pale wanapokutana na watu mbalimbali na kusikia story toka kwa watu kwamba wote watakuwa wanahusika katika tukio hilo wakati ni story ambazo sio za kweli.
Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa katika mahakama ya mwanzo jijini Dar es Salaam tarehe 13, 14 na 15 mwezi huu wa Novemba.
Hata hivyo the N2N soldier amesema kwa sasa anachotaka kufanya ni kudondonsha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya ‘surprise’ kwa mashabiki wake katika industry ya muziki wa Bongo.
Lord eyez alituhumiwa na msanii mwenzake Ommy Dimpoz kuwa alishirikiana na wenzake kumuibia vifaa vya gari lake na tuhuma hizo nzito ambazo ni pigo kwa kundi la weusi kiujumla zilipelekea Lord Eyez kukamatwa na kushikiliwa kwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa na baadae kufunguliwa kesi mahakamani ambapo alipewa dhamana.

SHARO MILIONEA AFUNGUKA, USHAROBARO MGUMU

KOMEDIAN aliyejitosa katika muziki wa Bongofleva, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefunguka kuwa hakuna kitu kigumu kama kuishi kisharobaro kwani kunahitaji gharama kubwa.
Akizungumza na ‘kachala’ wa Wikienda Staa Shopping aliponaswa hivi karibuni akifanya manunuzi ya nguo katika duka la Robby One lililopo Kinondoni jijini alisema ili uwe sharobaro wa ukweli inabidi usiwe mbahili katika kununua nguo kila mara ili uendane na staili hiyo ya usharobaro.“Kweli kabisa ndugu yangu hutakiwi kuwa mbahili kwani ukiwa na tabia hiyo wavimba macho mitaani watakutungia jina la sharobaro mchafu,” alisema Sharo Milionea.Komedian huyo alifanya shopping ya kununua vitu dukani hapo iliyogharimu kiasi cha shilingi laki mbili na ushee.

BENDI YA MSONDO NGOMA YAKABIDHIWA VYOMBO VYA MUZIKINa Mwandishi Wetu 
BENDI kongwe nchini ya Msondo Ngoma music band  imekabidhiwa vifaa vya muziki na kampuni ya Konyagi Dar es Salaam 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Konyagi nchini, David Mgwasa alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania na kuifanya msondo kuwa imara katika kutoa burudani kwa watanzania.
"Msondo ni bendi kongwe tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 imesimama imara katika kutoa burudani ya uhakika kwa watanzania sanjari na kutumia nyimbo zake katika kuelimisha, kufunza jamii ya watanzania walio wengi," alisema Mgwasa.
Alisema watu wengi kwa kuwepo bedndi ya msondo wamewezakupata mafunzo mengio kupitia nyimbo zao ambazo nyingi zimekuwa zikitoa mafunzo kwa watanzania.
Hivyo alisema kuwa kwa kuwapatia vifaa hivyo, Msondo itakuwa moto wa kuotea mbali katika kutoa burudani ya uhakika hali itakayofanya bendi nyingine kwa wasindikizaji katika tasnia ya muziki wa dansi nc?hini.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Maalim Gurumo alisema kuwa kwa sasa wanadeni kwa Watanzania na kampuni ya Konyagi katika kutoa burudani ya uhakika baada ya kupatiwa vifaa hivyo.
"Tunaamini baada ya leo kupata vifaa hivyo tutatoa burudani ya uhakika sanjari na kukijenga vyema kikosi chetu kwa lengo la kukiimarisha," alisema Gurumo.
Kiongozi wa bendi hiyo Said Mabela alitoa shukrani wa kampuni ya konyagi kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kutoa burudani safi kwa Watanzania na Afrika kwa ujumla.
"Tunashukuru kampuni ya Konyagi kutupatia vifaa vya muziki ambavyo kwetu ilikuwa ni vigumu kwa kipindi hiki kuvipata, hivyo tunaamini tutafanya tutaendela kuwa vinara katika kutoa burudani nchini," alisema Mabela.
Ofisa Habari wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa amefurahishwa na kampuni hiyo kutoa vifaa hivyo akiamini kuwa vijana wake watafanya vizuri zaidi katika ushindanio wa muziki huo nchini.
Pia aliwaomba wadau wengine wa muziki nchini kujitokeza  kuisaidia Msondo ili kuijengea uimara katika ushindi wa muziki huo nchini ili kuendelea kuwa bendi bora na ya kuigwa nchini. 

Sunday, November 11, 2012

HAPPY B'DAY TO MY YOUNG SISTER, MARIAM SULEIMA LYEME

Hope leo ni siku nyingine tena ya furaha kwa mdogo wangu huyu kipenzi (Mariam). Mungu akupe maisha marefu yenye Afya, yaliyo bora na yenye mafanikio! 
HEPIBESDEI!

Thursday, November 8, 2012

TANZANIA NA ZAMBIA SASA KUPAMBANA KWENYE MASUMBWI


WAPENZI WA MCHEZO WA MASUMBWI MNATAHALIFIWA KUWA KUTAKUWA NA MCHEZO WA NGUMI WA KIMATAIFA KATI YA ZAMBIA NA TIMU YA TAIFA YA BOXING YA TANZANIA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI YA TAREHE 10,11,2010 KATIKA UKUMBI WA DDC KARIAKOO KUANZIA SAA KUMI KAMILI  NJOO UBURUDIKE NA NGUMI SAFI KUTOKA KATIKA MATAIFA MAWILI TOFAUTI MPAMBAO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA KINGILIO MLANGONI ITAKUWA NI 5000 KWA KILA MTU MPAMBANO SI WAKUKOSA KWANI UMEANDALIWA VEMA NA ULIKUWA UKISUBILIWA KWA HAMU HIVYO SHIME WATANZANIA KUJITOKEZA KUIPA SAPOTI TIMU YA NGUMI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KUHAKIKISHA  MABONDIA WA TANZANIA WANAFANYA VIZURI KWA KUJA KUTOA MCHANGO WAKO WA KUJA KUWASHANGILIA MGENI RASMI SIKU HIYO NI MBUNGE WA KINONDONI IDDI AZANI AMBAYE KWA SASA YUPO BEGA KWA BEGA NA TIMU HIYO KUAKIKISHA INAFANYA VIZURI  KATIKA MCHEZO WA NDONDI MASUMBWI MAWE

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali
 

DIAMOND, I-VEW MEDIA WADAIWA KUWATAPELI MODELS WALIOWACHEZESHA KWENYE VIDEO

Katika Kipindi cha XXL cha Clouds FM Segment You-Heard Amepigiwa Simu Model mmoja wapo Ambae alichaguliwa katika ule mchakato uliofanywa na Diamond pale Nyumbani Lounge wa kuchagua Models watakao shiriki katika Video ya Nataka Kulewa ambayo ilifanyika Jana ..Model huyu Amesema toka wachaguliwe wamekuwa wakienda ofisi za I-View ambapo ndio wahusika wa video hiyo Bila kupewa chochote na kushinda na Njaa, Mbaya zaidi ni Hapo Jana ambapo video ilifanyika na kuambulia Kupewa Shilingi Elfu kumi Kila Mmoja ...Nadhani Hapa Diamond ana Tuhuma Za kujibu ili awake mambo sawa ..Binti Alie Ongea na Clouds Fm ameongea kwa Uchungu Sana....

MANECKY AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI KUHUSU BEAT YA "DIAMOND" "NA PASHA"

Wakati wimbo wa Diamond ‘nataka kulewa’ ukitengeneza topic kwenye media kibao TZ na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wengi wanasema beat hiyo inafanana asilimia 100 na ile ya beat ya wimbo wa Pasha alomshirikisha Tunda Man ‘Mtoto Amekua’, Manecky wa AM records ambae ndiye aliyetengeneza ‘nataka kulewa’ amesema beat ya wimbo huo ni tofauti kabisa na ile ya wimbo wa Pasha. 
Producer huyo ambae ndiye mshindi wa kili music awards 2011 kama producer bora wa mwaka alifunguka kwa msisitizo kwenye XXL cha Clouds fm kuwa hakusample beat sehemu yeyote ile na hiyo beat aliifanya kwa mawazo yake mwenyewe kuanzia mwanzo kabisa.
Alipoulizwa maoni yake kama beat hizo mbili zinafanana au hazifanani, alisema “kwa kitu ambacho mimi nimeweza kusikiliza hizi ni beat mbili tofauti, sema kuna idea ya lead sound ambayo inaweza kuwa na mfanano flani, ndio maana nikarudia kusema palepale, mimi ni mtu ambae nasikiliza muziki kila siku, na ni binadamu na sio computer sio kitu flani ambacho kinasema ni kitu flani kifanye hivi…!”
Manecky amesema hata Tunda Man aliisikiliza ‘beat ya Nataka kulewa’ mara nyingi tu lakini hakuweza kuifananisha kabisa na ile ya wimbo wa Pasha ambao yeye mwenyewe kaweka vocal yake kwenye beat ileile inayofananishwa, lakini inaonekana alipousikia watu wanasema zinafanana ndipo na yeye akashtukia kuwa inawezekana iko hivyo.Duuuh..!
Kweli tunatofautiana kushtukia copy, wengine wakisikia hata kinanda cha kwanza tu wanashtukia ila Tunda Man yeye ameshtuka baadae sana pamoja na kuitumia beat hiyo.
Wimbo wa Diamond umepata challenge kubwa sana tangu au-release rasmi, muda mchache baada ya kuonekana beat inafanana na ya wimbo wa Pasha ft. Tunda Man ‘nataka kulewa’, H-Baba alijitokeza na kumtuhumu Diamond kwa kumuibia idea ya wimbo huo tena kwa makusudi huku akiweka hadharani vielelezo vya demo ya wimbo wake ‘nataka kulewa’ akiwa na Q-Chillah.

Wednesday, November 7, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AENDA KUMPA POLE KATIBU WA MUFT Z'BAR BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga ambaye amelazwa katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhiombili kufuatia majeraha ya usoni na kifuani yaliyotokana na  kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe mjini Unguja juzi. Rais ambaye amerejea  leo Jumanne Novemba 6, 2012 akitokea katika ziara ya kikazi ya  takriban juma moja katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu ya haraka.

Tuesday, November 6, 2012

TEJO-SQUAD WAACHIA NGOMA MPYA - UNYAMA NDANI YA GIZA

Tejo-Squad, kundi la muziki wa hiphop lenye maskani yake Olmatejoo "A" baada ya "simsms imara" toka Grandmaster Records sasa wanadrop na ngoma yao mpya kabisa ikiwa ni mdundo toka Mwanza "RockCity" kwa producer Yusuf wa Mkoko ikiwa ni pini "unyama ndani ya giza" 

Monday, November 5, 2012

RUGE: RAY C AMEANZA MATIBABU, ATAKUA FITI MUDA SIO MREFU


“Alishaanza hatua ya kwanza ya matibabu, anafanya bidii kwenda kwenye hatua ya pili ya matibabu, kweli kabisa anafanya bidii na kuhusu taarifa kwamba amepelekwa Iringa kupata matibabu ya kuacha utumiaji wa dawa za kulevya hakuna ukweli wowote, kuna taarifa nyingi za kupotosha ambazo mimi nilikua naomba watu wangeacha kuzisambaza kwa sababu hazisaidii mtu yeyote yule na vilevile zinaendelea kulikuza tatizo”

Sunday, November 4, 2012

MSONDO NGOMA WAPAGAWISHA WAKAZI WA ILALA USIKU WA HUU.

http://3.bp.blogspot.com/-dmujf-3taP8/UJatnGGRdDI/AAAAAAAAKq4/nLrDWRPNXdw/s1600/IMG_9484.JPG 
Waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma kutoka kushoto ni Eddo Sanga Sahani Dede na Juma Katunduwakitoa burudani usiku huu Katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni.http://3.bp.blogspot.com/-Z_e5r-05SwI/UJatZEqlPSI/AAAAAAAAKqw/ldeJK1_5mz0/s1600/IMG_9483.JPG 
Mpiga gila la Ridhim Wa msondo ngoma Zahoro Bangwe akizikung'uta nyuzi wakati wa onesho la bendi hiyo lililofanyika jumapili katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni http://4.bp.blogspot.com/-Lr9rLNikqms/UJax0sMsOoI/AAAAAAAAKrg/UG6ViEv5UKo/s1600/IMG_9491.JPG 
Wasanii wa bendi ya Msondo ngoma wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Max Bar Ilala bungoni kutoka kushoto ni Shabani Lendi,Hamisi Mnyupe na Romani Mng'ande wakipuliza ara za mziki picha na www.burudan.blogspot.com

KAMANDA MPINGA AFUNGA MAFUNZO YA WAENDESHA PIKIPIKI CHUO CHA UFUNDI STADI VETA – CHANG’OMBE JIJINI DAR‏


Kamanda Mpinga akiongea na wahitimu, L to R ACP Missime RPC Temeke, Yakub Rajab TDA, Mkurugenzi manispaa temeke,M/kiti Bodi ya ushauri, Mkuu wa chuo cha VETA, ACP Kahatano Traffic Kuu.

Mgeni rasmi,Kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani  Tanzania,SACP Mohamed Mpinga akikmkabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu ya mafunzo ya waendesha piki piki yaliyofanyika chuo cha ufundi stadi-VETA Chang'ombe jijini jana.Vijana wapatao 301 kutoka Temeke walipewa vyeti
 
Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Mama Nyalile  akiwaasa bodaboda, L to R kamanda Mpinga, M/kiti wa  wa bodi ya ushauri ya chuo Nd. Marealle, Mkuu wa chuo cha VETA Nd. Ng'andu.
Onyesho la Mishikaki ambapo waendesha piki piki hap wameapa kutopakia abiria zaidi ya mmoja.

Wahitimu wa mafunzo ya uendeshaji boda boda wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo.

Waendesha piki piki wakila kiapo cha utii.

 Wahitimu hao wakifurahi kwa kucheza muziki
(Picha zote kwa hisani ya SACP Mpinga - CO Traffic)