b..

B1

Wynem

animation

Friday, February 14, 2014

JHIKOMAN AWASHA MOTO SAUTI ZA BUSARA 2014...

  

Na Andrew Chale, Zanzibar.
MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro rege, Jhikoman Manyika   jana usiku Februari 13,  aliwasha moto  kwa kupiga shoo ya nguvu iliyodumu kwa lisaa limoja na kukonga nyoyo umati mkubwa uliojitokeza kwenye tamasha hilo la 11,la Sauti za Busara mwaka huu 2014. Jhikoman alipanda jukwaani majira ya saa tatu usiku  sambamba na bendi yake ya Afikabisa na kupiga vionjo mbalimbali vya nyimbo zake za sasa na za nyuma.

Jhikoman aliweza kuwasha moto huo kwa kupiga nyimbo zake zilizopo kwenye albamu yake ya Chikonda na nyingine hali iliyokonga wadau hao wa muziki wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali na watanzania waliojumukika kwenye tamasha hilo.

Hata hivyo, Jhikoman alisema baada ya shoo hiyo anatarajia kupiga shoo zingine kwenye nchi mbalimbali kwa kufanya ziara maalum ikiwemo mataifa ya Ulaya. Mbali na Jhikoman wasanii wengine ni pmoja na kundi la Seven Survivor wanopiga muziki wa mchiriku, huku kundi la Baladna taarabu wao walikonga nyoyo kwa muziki wa mwambao na taarabu asili. Wengine ni kundi la Pongwa kutoka visiwani Zanzibar,  Tritonik (Motius), na nyingine nyingi.

Awali tamasha hilo lilifunguliwa kwa paredi iliyokusanya wanamuziki mbalimbali kutoka mataifa yote na kwa kila mmoja kuonyesha muziki wake mitaani na kasha kumalizikia kwenye viunga vya Ngome Kongwe. Aidha tamasha hilo la siku nne, linatarajiwa kuwa na wanamuziki mbalimbali vikiwemo vikundi 32, vyenye jumla ya wasanii 200, ambao watapiga shoo kwenye jukwaa hilo la Kimataifa. Hadi sasa mji wa Zanzibr umebarikiwa kuwa na wageni mbalimbali wakiwemo waliofika maalum kwa ajili ya shoo na wale wanaokuja kupumzika kwenye kisiwa hiki cha marashi ya karafuu.Aidha, tayari idadi ya wageni imeongezeka  huku baadhi ya hoteli zikiwa zimefurika  na biashara za kitalii zikiwa zinanunuliwa kwa wingi.

Kwa upande wake, David Ojoy ambaye ni msaidizi wa masuala ya habari wa tamasha hilo, anasema kuwa  hali ya wageni imekuwa kubwa kufika kwenye tamasha hilo ikiwemo kupata habari mbali mbali zinazoptikana kwenye mtandao maalum wa tamasha hilo pamoja vyombo vya habari. "Tunavipongeza vyombo  vya habari kwa kutupa sapoti na tunaomba tuendelee hivyo hivyo ilikukuza muziki wetu wa kiafrika na kujenga tamaduni imara hapa afrika na tamasha hili liendelee kuwa la kimataifa zaidi" alisema Ojay.

"VIDEO" KITIFA FT. LINEX - MAISHA YA MJINI


Thursday, February 6, 2014

NGUMI ZA NELSON MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP ZAFUNGULIWA KAWE


Bondia Rashidi Samvu kutoka Kigoma  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela  yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam
Bondia Part Kimweri kutoka Tanga  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Saidi Jabir wa Ngome Dar, wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela  yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Kimweri alishinda mpambano huo kwa pointi

Bondia Fabian Gaudence kushoto akipambana na Hussein Mnimbo  wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela  yabayofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Gaudence alishinda mpambano huo kwa pointi
Mgeni wa heshima katikati Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete akiwa na viongozi wa Shilikisho la mchezo wa ngumi za Ridhaa nchini kulia ni Rais wa shilikisho hilo Mutta Rwakatare  makamu wa rais Lukelo Willilo na
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis


mjumbe wa bft antony mwangonda akiwa na makamu wa rais Lukelo Willilo
picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu   
MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayokwenda kwa jina la Nelsoni Mandela Open ChampionShip  yameanza kutimua vumbi katika
Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam


akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa ali ya juu Makamu wa Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo Willilo 'amesema mashindano hayo kwa sasa yameboleshwa kwa kufuata taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia kwa sasa mabondia awavai kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo wapenzi wa ngumi weje waone mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa ndio ambazo ni msingi wa maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini;'
zamani mabondia walikuwa wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko sasa awavai kofia wanapigana vichwa wazi  ambapo kwa kuanzia tumeamua kuweka mashindano haya kwenye viwanja vya wazi na ni bule tu akuna kingilio ili kila mtu ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo yanayo husisha mikoa mbalimbali nchini
mashindano haya yatakuwa ya siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na ngumi zinanza kupigwa saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku ngumi ndio zitakuwa zikisha
Katika ufunguzi huo bondia Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele ya Said Jabir wa ngome na Rashidi Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi na Hafidhi Kassimu wakati Fabian Gaudence  akimsambalatisha Hussein Mnimbo

Sunday, February 2, 2014

"AUDIO" Vatoloco Gangz - Deadliest Men

Vatoloco Gangz wakiwa katika mchakato wa kumalizia mixtape wanadrop ngoma ya "Deadliest Men" ikiwa ni HipHop style ya Grime iliyo maarufu zaidi Uingereza, kusikiliza/Kudownload click HAPA