Monday, February 28, 2011

MBIO ZA VODACOM FUN RUN ZANG’ARISHA KILI MARATHON

Baadhi ya washiriki wakitimua mbio za Vodacom 5KM Fun Run mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini Alhaj Musa Samizi kuanzisha mbio hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Dr Noman sigwa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa Vodacom 5KM Fun Run Kalis Stiven kitita cha shilingi 100,000 mara baada ya kuibuka mshindi wa mbio hizo,kulia Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Dr Noman Sigwa akimpatia zawadi Mtoto mlemavu Cornel Zagara aliyeshiriki mbio za Vodacom 5KM fun run zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro,katikati Meneja Udhamini wa Vodacom Rukia Mtingwa.

Mtoto mlemavu Cornel Zagara akishirikia katika mbio za Vodacom 5KM Fun Run zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanja.

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishangilia mara baada ya kumaliza mbio za Vodacom 5KM fun Run zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Saturday, February 19, 2011

Tamasha la Pasaka kusaidia wahanga wa mabomu Gongo la Mboto


 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka la
nyimbo za Injili, Alex Msama (kulia) akimkabidhi mtangazaji wa Radio Clouds, Anthonio Nugazi, magunia yenye vyakula
mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 3 ikiwa ni msaada kwa ajili ya walioathirika kwa mabomu ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Clouds,
Mikocheni, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka la
nyimbo za Injili, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kukabidhi msaada wenye thamani ya sh. milioni 3 kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Msama Promotions ambao ndio wanadaaji wa Tamasha kubwa la Pasaka, Alex Msama amesema kwamba kiasi cha fedha zikazopatikana katika tamasha hilo, zitatumika kuwasaidia waathirika(wahanga) wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Msama amesema hayo baada ya kuwakabidhi waathirika wa milipoko hiyo msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya ya shilingi mil 3.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ndiye aliyekabidhi msaada huo leo katika ofisi ya redio ya Clouds FM iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Vitu vilivyotolewa ni magunia manne ya mchele, kila moja likiwa na kilo 120, magunia mawili ya maharage, magunia 10 ya unga wa mahindi, mifuko miwili ya sukari, mifuko mitatu ya unga wa ngano yenye kilo 25 kila moja na ndoo mbili za mafuta ya kupikia.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Msama alisema wameguswa na waathirika hao, na pia wanafanya hivyo ikiwa ni kutimiza moja ya malengo ya tamasha hilo.
Msama alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za milipuko hiyo kwa Watanzania, na ndiyo maana wamejitolea kusaidia waathirika kwa misaada ya vyakula.
“Lengo kubwa la tamasha la Pasaka linaloratibiwa na Msama Promotions ni kusaidia watoto yatima na jamii kwa ujumla... hata hawa wenzetu walioathirika kwa kwa mabomu hatuna budi kuawasaidia.
"Natoa mwito kwa Watanzania wenzangu kuwa na moyo wa huruma na kuwasaidia waathirika hawa wa mabomu na pia nawa[pongeza Clouds FM kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha Watanzania kutoa misaada," alisema Msama.
Akipokea msaada huo, mtangazaji wa Clouds FM, Anthonio Nugazi anayeendesha kipindi cha Kambi Popote, alimshukuru Msama kwa kuonesha moyo wa kujitolea, na akatoa mwito kwa Watanzania wengine kuiga mfano.
Nugazi alisema Clouds 88.4 FM watawasilisha michango hiyo kwa wahusika katika kambi waliyoianzisha ya kutoa msaada Shule ya Msingi Mzambarauni iliyopo Ukonga, Mombasa, Dar es Salaam.
Tamasha la Pasaka la nyimbo za Injili za kumsifu Mungu, litafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Apili 24 mwaka huu na litashirikisha wasanii kutoka nchi sita za Afrika wakiwamo waimbiaji kutoka Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Lengo la tamasha la mwaka huu ni kupata fedha zitakazotumika kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wajane.
Milipuko hiyo iliyotokea katika kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha 511 KJ, iliyopo Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ilisababisha vifo vya watu 20 huku wengine zaidi ya 300 wakijeruhiwa.
Pia milipuko hiyo ilisababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi huku wengi wakipata hifadhi kwenye Uwanja wa Uhuru wakiwamo watoto wadogo waliopotezana na wazazi wao.

Friday, February 18, 2011

WAATHIRIKA WA MABOMU YA GONGO LA MBOTO WAENDELEA KULETWA UWANJA WA UHURU.Mama wa watoto wa tatu aliejitambulisha kwa jina la Zawadi Hassan akiwa na watoto wake wawili huku akihuzunika kwa kutokujua alipo mtoto wake mmoja wapo kutokana na kukimbia kwa kujinusuru na mabomu yaliyokuwa yakilipuka usiku wa kuamkia leo huko gongo la mboto.
Sehemu ya watoto waliookotwa huko Gongo la Mboto wakiwa ndani ya gati wakati wakiletwa ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar mchana huu.
wengine wakiendelea kuletwa hivi sasa.
Uandikishaji ukiendelea kwa wahanga wa mabomu ya huko Gongo la Mboto.
Wengine wakiwa wamejipumzisha kutokana na uchovu wa usiku kucha kwa hali iliyokuwa huko Gongo la Mboto kutokana na Milipuko ya mabomu katika moja ya maghala ya kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliopo huko Gongo la Mboto usiku wa kuamkia leo.
Wadau wa Msalaba Mwekundu wakiendelea kutengeneza mahema ya kuhifandhia wahanga wa mabomu yaliyoripuka usiku wa kuamkia leo na kusababisha watu wengi kupoteza makazi yao.
Mmoja wa wasamalia aliejutokeza uwanjani hapo akiwa pamoja na kijana wa Scout wakiwasaidia kuwanywesha maziwa watoto waliletwa uwanjani hapa kutokana na kupoteana na wazazi wao.
hali bado si shwari huko Gongo la Mboto kwani bado idadi kubwa ya watoto na wakazi wa maeneo hayo wanaendelea kuletwa uwanjani hapa.

Wednesday, February 16, 2011

HILI NDILO VARANGATI LA MABOMU YA GONGO LA MBOTO

Majeruhi wakifikishwa katika hospitali ya AMANA ilala usiku wa kuamkia leo mara baada ya milipuko ya mabomu Gongo la Mboto na kusikika kariobu kila kona ya jiji la Dar.
Daktari wa Amana akiwa anamhudumia mmoja wa majeruhi alifishwa hospitalini hapo.
Watoto wakiwa wanamuangalia mama yao aliejeruhiwa hospitalini hapo.
Majeruhi wa mlipuko wa mabomu wakiwa wamelala chini huku wakiwa wametundikiwa dripu katika hospitali ya amana
Deo Rweyunga wa redio one sterio akiongea na mtoto aliejeruhiwa na mlipuko wa mabomu.
Mmoja wa majeruhi akipata huduma.
Majeruhi mmoja mara baada ya kupata huduma ya kwanza katika hospitali ya amana.

MR. II aka SUGU KUUZINDUA MIX TAPE YA ANT VIRUS.


Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Mr II aka Sugu, siku ya tarehe 20 atakuwa pale Club Billicanskwaajili ya kuwashukuru wananchi pamoja na mashabiki wake ambao wako nae mpaka sasa. 

Sugu mbali na kuwashukuru ataizindua mixtape ya Anti Virus na atasindikizwa na wasanii wengine wakiwemoOrijino KomediSalu T na member wote wa 
Anti Virus.

Sitta, Mwanjelwa nao wajitosa Tamasha la Pasaka


WAZIRI wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo kupitia CCM, Samuel Sitta amempongeza Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama kwamba fedha zake zinazopatikana zinafanyiwa kazi zilizokusudiwa.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakalofanyika Aprili 24 lengo lake kubwa kwa mujibu wa Alex Msama ni kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.
Sita amesema kwamba jitihada zinazofanywa na Alex Msama ni mfano wa kuigwa kwa vijana wengi hapa nchini, kwani anaisaidia jamii kwa mapenzi kutoka moyoni.
“Kwa kweli kama wangejitokeza vijana wengine kama Msama naamini kabisa jamii yetu ingekuwa inapata misaada mingi, kwani jitihada anazozifanya ni za kumpongeza.”
Alisema ameshuhudia walemavu wakinunuliwa baiskeli, watoto yatima wakisomeshwa na wajane kusaidiwa mitaji ya biashara kupitia fedha alizozipata Msama kupitia matamasha pa Pasaka yaliyopoita.
Aliongeza kusema kwamba kwa kiasi kikubwa tamasha hilo pia litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwani wengi hivi sasa wameamua kujikita katika muziki wa injili kwa ajili ya kumuimbia Mungu na kujipatia kipato.
“Unapokuwa na watu wenye uzalendo kama Msama Promotions kwa hakika kabisa vijana wengi watajitokeza na watahamasika kujiingiza katika muziki huu, kwani watakuwa na uhakika wa kujipatia kipato,” alisema Sitta.
Wakati huo huo Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi mkoani Mbeya, Mary Mwanjela amejitokeza kumpongeza Msama kwa kuandaa Tamasha hilo.
Pia hivi karibuni aliyekuwa Waziri Bunge, Sera na Uratibu katika awamu ya kwanza ya rais Jakaya Kikwete, Phillip Marmo alilisifia tamasha la Pasaka kwa kusema kwamba malengo yake ni mazuri kwani linasaidia jamii.

NEW ALBUM COVER.....CHINI YA UVUNGU WA MOYO WANGU YA RAMA DEE.

NEW ALBUM COVER...CHINI YA UVUNGU WA MOYO WANGU  ya RAMA DEE ndio iko kidizaini hii na soon itakuwa kitaa. kaa tayari kupata madini ya kutosha kabisa katika albam hii!

WAANDAAJI MUZIKI WAILILIA BONGO FLEVA


Kulia ni Muandaaji chipukizi wa muziki wa kizazi kipya anayekuja kwa kasi nchini kutoka Studio za FishCrab,Lamar akiweka msisitizo kwenye mada iliyowasilishwa kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA. Pembeni yake ni Mtaalam wa Muziki John Ndumbaro kutoka mkoani Morogoro.
Muandaaji wa Muziki kutoka Studio za MJ, Joachim Kimario ‘Master J’ (Kulia) akichangia mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa, BASATA.Kulia kwake ni muandaaji mwenzake Allan Mapigo.

Na Mwandishi Wetu
Waandaaji mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Joachim Kimario (Master J), Lamar na Allan Mapigo wamedai kwamba,muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina la Bongo Flava umepoteza muelekeo na juhudi za makusudi zinahitajika katika kuurudisha kwenye mstari na kuupa utambulisho wa kitanzania.
Wakizungumza katika mjadala mkali kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa, waandaaji hao wa muziki walitupa lawama kwa watangazaji wa vituo vya redio na TV kwamba ndiyo chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa muziki huo kwa kile walichoeleza kwamba, hakuna utaratibu wa kuchuja nyimbo kabla ya kwenda hewani na baadhi hawana utaalam wa kazi zao.
Aidha, waliongeza kwamba pamoja na wao kujitahidi kuandaa midundo kwa kufyonza kutoka jamii za kitanzania, wasanii wa hapa nyumbani wamekuwa ni wa kuiga kila kitu wanapoingia studio na hawako tayari kubadilika wanapoelekezwa hali ambayo imeufanya muziki uhame kutoka kuwa wa jamii ya Tanzania na kuwa ule wenye kunakiri kila kitu kutoka nje hususan Marekani.
“Kwa sasa wasanii wanachokifanya ni kusikiliza muziki wa nje na kuja kuingiza kwenye muziki wao.Wamekuwa wakikopi kila kile msanii wa nje anachofanya kuanzia kuvaa na kuimba, wanataka wafanane na Jay Z hata wakija studio wanataka watengenezewe sound (midundo) kama ile ya nje” alisema Lamar kutoka Studio za FishCrab.
Kwa upande wake Master J ambaye ni mmiliki wa Studio za MJ alisema kwamba,siku hizi wanamuziki hawaangalii mazingira ya jamii za kitanzania tofauti na zamani, wamekuwa ni wa kuimba mambo yasiyofaa na yasiyopatikana katika jamii yetu bali ile ya Marekani hali ambayo imezidi kuutokomeza muziki wa kizazi kipya.
“Zamani tulikuwa na Hip Hop kama za akina 2 Proud ambaye kwa sasa anajiita Mr.Two (Sugu).Walikuwa wanaimba Hip Hop yenye kubeba matatizo halisi ya jamii ya Tanzania , Sugu aliimba nyimbo kama mikononi mwa polisi, miaka chini ya 18 na zote mbali ya kugusa matatizo yaliyopo ya jamii zilipendwa na kufanya vizuri tofauti na sasa” alisisitiza Master J
Aliongeza “Ujio wa redio na televisheni zisizozingatia utaalamu (professionalism) kwa watangazaji wake bali swaga (ujanja ujanja) na vipaji tu vya kuongea ni moja ya sababu ya kupoteza dira kwa muziki na hapo ndipo mambo yalianza kuharibika”.
Katika Jukwaa hilo la Sanaa pamoja na waandaaji wa muziki hao kutoa michango yao kuhusu mwenendo wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mtaalam wa muziki John Ndumbaro alitoa maelezo ya kina kuhusu sekta hiyo ya sanaa ambapo mada ilikuwa ni Changamoto Katika Kutengeneza Muziki wenye Utambulisho wa Tanzania.

Sunday, February 13, 2011

KESHO NDIO SIKU YA UTAMBULISHO WA ALBUM YA ATATAMANI 'LINAH'

 

LINAH FROM THT. ANAITAMBULISHA ALBUM YAKE YA ( ATATAMANI ) YENYE MASONGI YA MALAVIDAVI YAKUTOSHA.KABISA HUKU ATASINDIZWA NA DITTO, NASH, BEKA, MATALUMA, THT DANCER, NA WENGINE WENGI, NA PIA SHOW ITAKUA NI YA LIVE BAND. UKUMBI NI CLUB MAISHA SIKU VALENTINE DAY 14/02/2011 

KIINGILIO NI. COUPLE 15,000/= SINGLE 10,OOO/=

Thursday, February 10, 2011

WAJASIRIAMALI WA KITANZANIA

Mjasiria mali (FUNDI SEREMALA) akiwa kazini pande kitaa cha KAWE
Mjasiria mali (DEREVA TAX) akiwa kazin pande za ubungo buss terminal
Wajasiria mali (WAUZA MITUMBA) akiwa kazin pande za manzese darajani

HAPPY BIRTH DAY SHEIKH SULEIMAN HUSSEIN LYEME.

HAPA NI SULE JUNIOR (MTOTOWA KITAA) AKIWA NA BABA YAKE SHEIKH SULEIMAN LYEME
Hapa sheikh suleiman akiwa na wanae kuanzia kulia ni Hussein Suleiman, Hawa Suleiman, Mariam Suleiman, Sheikh Lyeme na Sule Junior

Wednesday, February 9, 2011

MPIGIE KURA AARON KWENYE TUZO ZA MUZIKI WA INJILI


Aaron muimbaji wa muziki wa kizazi kipya pamoja na injili ameingia kwenye tuzo za injili kwa kupitia ngoma mbili  ambazo ni NISAMEHE na JUU MBINGUNI 
Kategory alizoingia ni pamoja:-
           1- SINGO BORA  na ngoma aliziongia nazo ni NISAMEHE na JUU MBINGUNI
 2 - MSANII ANAECHIPUKIA
Aaron anaomba umpigie kura kwa kuandika neno TUZO kisha unaacha nafasi kisha AARON unaacha nafasi kisha kisha jina la wimbo NISAMEHE  / JUU MBINGUNI kisha unatuma kwenda namba 15522
Kwa upande wa anaechipukia utaandika TUZO kisha unaacha nafasi, kisha AARON unaacha nafasi kisha ANAECHIPUKIA halafgu unatuma kwenda 15522
Ngoma zenyewe nin:-
1 - JUU MBINGUNI ft BENJAMIMNI WA MAMBO JAMBO, KAPIPI &DULLY SYKES 
                             - STUDIO MZUKA  REC. PRODUCED BY AARON & BENJA
 2 - NISAMEHE          - STUDIO FLUKE PRO. LONDON - PRODUCED BY AARON & LUKE

KUMBUKUMBU:

Imekaribia ile siku ya kumkumbuka MAMA YANGU MZAZI! so kwa upendo wenuWADAU wa blog ya mtoto wa kitaa nawaomba tushrikiane wote kwa pamoja kumuombea dua mwenyezi mungu aendelee kumuweka mahali pema pepooni INANA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAAGJIUUN!

Monday, February 7, 2011

ARUSHA STREET VIBES - NJOO UONE TOFAUTI

SERIKALI YAOMBWA KUINGIZA RASMI SOMO LA SANAA KATIKA MITAALA YA ELIMU NCHINI.Mratibu wa Programu ya Jukwaa la Sanaa. Bw.Ruyembe (kulia) akifafanua jambo. Wengine kutoka kulia kwake ni Bw. Mayalla na Mpepo.
Mkufunzi wa Bendi ya Jeshi la Polisi, Damas Mpepo akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhusu Mchango wa Majeshi Katika Kuthamini Ajira za Sanaa.Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, Afisa wa Bendi ya Polisi Bw. Mayalla na Mratibu wa Jukwaa hilo, Ruyembe C.Mulimba.
Mmoja wa wadau wa Jukwaa la Sanaa akiuliza maswala mbalimbali kuhusu Mchango wa Majeshi Yetu kwenye tasnia ya Sanaa

Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeombwa kuliingiza rasmi somo la Sanaa kwenye mitaala ya elimu kutoka ngazi ya awali ili kujenga vipaji vya vijana katika tasnia hii na baadaye kuweza kujiajiri.
Ombi hilo limetolewa Jumatatu ya wiki hii na wadau wa sanaa wakati wakichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) iliyohusu Mchango wa Majeshi Katika Kukuza Ajira za Sanaa nchini iliyowasilishwa na Mkufunzi wa Bendi ya Polisi Damas Mpepo ambapo wengi walikunwa na jinsi majeshi yetu yanavyoenzi sanaa na kuwa mstari wa mbele kuiimarisha tasnia hii.
“Majeshi yetu yamekuwa yakifanya vizuri katika tasnia ya Sanaa kwa kuwa kuna elimu wanayoipata katika tasnia hii. Ni lazima Wizara ya Elimu iamke sasa na itambue kwamba tasnia ya sanaa ni kimbilio la vijana wengi kwa sasa hivyo lazima uwekwe utaratibu wa kujenga vipaji vya sanaa toka ngazi ya awali ili kukuza tasnia hii inayoajiri vijana wengi kwa sasa” alichangia mdau.
Hoja hii iliungwa mkono na Mkufunzi Mpepo wa Bendi ya Polisi ambapo aliweka wazi kwamba, wizara haina jinsi kwa sasa zaidi ya kuliingiza somo la sanaa kwenye mitaala ya elimu badala ya ilivyo sasa ambapo limekuwa halitahiniwi na vijana wengi mashuleni wamekuwa wanalikuta mitaani baada ya kumaliza shule.
“Sanaa inaajiri watu wengi sana, hata Jeshi la Polisi limeajiri wasanii karibu 500, tatizo lililopo sasa ni kwamba somo la Sanaa halifundishwi na hivyo ujuzi katika tasnia hii ni tatizo kubwa. Wizara ya Elimu lazima sasa ione haja ya kuliingiza somo la sanaa kwenye mitaala ya elimu toka ngazi ya awali na litahiniwe kwenye mitihani ya shule na taifa” alisisitiza Mpepo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji BASATA Ruyembe Mulimba alisema kwamba, hoja ya somo la sanaa kufundishwa toka ngazi ya awali ya elimu ilichukua muda mwingi kwenye Kikao cha Nane cha Sekta ya Utamaduni kilichomalizika hivi karibuni jijini Mwanza ambapo wadau walitoka na azimio la kushawishi somo hili kuanza kufundishwa na kutahiniwa kama masomo mengine.

“Kauli mbiu ya kikao cha nane cha sekta ya utamaduni ilikuwa ni Sanaa ni Ajira Tuithamini lakini wadau wengi walisikitishwa na somo la sanaa kutokufundishwa toka ngazi ya awali na walitaka wizara ya elimu kusikia kilio hicho kwani tasnia hii kwa sasa inaajiri vijana wengi sana wanaokadiliwa kufika milioni sita.
Katika kikao hicho cha Jukwaa la Sanaa, Jeshi la Polisi kupitia Bendi yake lilitoa taratibu za kuajiri wasanii na sifa zinazohitajika ambapo jumla ya wadau 157 waliohudhuria walipata wasaa wa kuelimishwa kazi mbalimbali za Bendi ya Jeshi la Polisi.

LISTENING SESION YA THE ELEMENT MIXPATE KUWAUNGANISHA WADAU

Tarehe 23 mwezi huu, itafanyika bonge la listening session ya THE ELEMENT MIXPATE pale mzalendo pub. Na baadhi ya wageni watakaofanya siku hiyo ikamilike ni pamoja na DJ PQ, Fid Q na wengine kibao ambao watatajwa kadiri siku inavyokwenda (ikikaribia). Nia ya Listening session hii si tu kwa ajili ya kusikiliza mixtape hii bali pia kama sehemu ya kuunganisha wadau na kubadilishana mawazo katika mambo tofauti tofauti. Pia kutakuwa na SHOWCASE ya djs wachanga kwa wale watakaotaka kuji expose katika industry, pia utaratibu wa namna hiyo hiyo kwa Young Producers kufanya showcasing inayoweza kuwaunganisha na wasanii wakubwa katika siku hiyo. kwa kufanikisha hili na pia kuchochea mwamko wa siku hiyo. basi tumeamua ku release track namba moja katika MIKS TAPE hii ukienda wka jina la HISIA.
Ni track pekee ambayo wahusika wakuu katika huu mzigo wameunganika pamoja, ni track inayozungumzia changamoto mbali mbali katika maisha yetu ndani ya jamii.... Verse I: Nikki anaelezea changamoto zinazokabiliwa kwenye game la music wetu.... Verse II: STEREO kajikita na changamoto za mtaani na mambo ya uswahilini, VERSE III: SUMA yeye kajitosa katika changamoto za utapeli wa mapenzi Verse IV: ONE THE INCREDIBLE yeye kaingia ndani ya familia zilizokosa mwelekeo.
Ni track ambayo haina chorus, 32 bars each, tunahisi inaweza isiwe ni user friend sana kwa media kwa sababu za itikadi za kibiashara (ni NYEUSI its not commercial) lakini ina ujumbe mkubwa ndani yake....bado tunaamini na ku project kuwa itakuwa na impact kubwa sana mtaani zaidi na kwenye net kuliko kwenye radio .
Hii track ni ruksa kuipiga kwa radio, kuisambaza thru NET na hata mtaani...lengo ni kufikisha ujumbe katika hadhira ya kitaani zaidi.
SIKILIZA WIMBO HUU KWENYE PLAY LIST HAPO KULIA KWAKO

Track: Hisia
Artist: Nikki Mbishi, Stereo, Suma & One
Produced by Duke
The Element mixtape
Music Lab 2011.

Patrick,
Artists & Studio manager,

Media Kings Tanzania Limited-Music Lab

CHEKI VIDEO MPYA YA YA BELLE 9 ft Mr BLUE - WE NI WANGU.

Sunday, February 6, 2011

GAZETI LA DIRA LIPO MTAANI LEO KAMA KAWAIDA YAKE

Leo kama kawaida ya gazeti hili kutoa habari zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na waandishi waliobobea katika habari za kiuchunguzi limtoka na jinsi mmiliki wa dowans alivyojipanga kuliteka bunge! unajua mmiliki huyo ni nani?, ana mipango gani? na ataliteka vipi? ....Usikose nakala yako ya DIRA YA MTANZANIAb kwa Tsh. 500/= tu

CHEKI VIDEO MPYA YA SIO KWELI - JAFARAI ft LADY JAY DEE.

Marmo alipa tano Tamasha la PasakaPhilip Marmo
Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Waziri wa Sera, na Uratibu waBunge katika awamu ya kwanza ya rais Jakaya Kikwete, Phillip Marmo amelisifia tamasha la Pasaka kwa kusema kwamba malengo yake ni mazuri kwani linasaidia jamii.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakalofanyika Aprili 24 lengo lake kubwa kwa mujibu wa Alex Msama ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ni kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Marmo alisema kwamba amefarijika mno na muamko wa Msama Promotions waandaaji wa tamasha hilo kwa kuangalia uwezekano wa kuwasaidia watoto yatima na wanawake wajane.
“Nimefarijika mno na muamko huu, kwakweli huu ni mfano wa kuigwa kwani ni watu wachache mno wanaoweza kuandaa matamasha kama haya na fedha zinazopatikana kuwasaidia watoto yatima na wajane,” alisema Marmo.
Aidha Marmo amesema kwamba kwa kiasi kikubwa tamasha hilo pia litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwani wengi hivi sasa wameamua kujikita katika muziki wa injili kwa ajili ya kumuimbia Mungu na kujipatia kipato.
“Unapokuwa na watu wenye uzalendo kama Msama Promotions kwa hakika kabisa vijana wengi watajitokeza na watahamasika kujiingiza katika muziki huu, kwani watakuwa na uhakika wa kujipatia kipato,” alisema Marmo.
Tamasha kubwa la Pasaka linatarajiwa kufanyika Aprili 24 mwaka huu siku ya sikuu ya Pasaka katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na baadaye kufanyika mjini Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na jijini Mwanza Aprili 26, lengo lake kubwa mwaka huu ni kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasiaid mtaji wa bishara wanawake wajane.