Tuesday, February 1, 2011

WAZIRI MFUTAKAMBA ALISIFIA TAMASHA LA PASAKA.

Mkugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Alex Msama ambae ndio muaaandaaji wa tamasha la pasaka
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Dk. Athuman Mfutakamba

Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Dk. Athuman Mfutakamba amelisifia tamasha la Pasaka kwa kusema kwamba ni jambo jema zaidi kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mfutakamba alisema kwamba amefarijika mno na muamko wa Msama Promotions waandaaji wa tamasha hilo kwa kuangalia uwezekano wa kuwasaidia watoto yatima na wanawake wajane.
“Nimefarijika mno na muamko huu, kwakweli huu ni mfano wa kuigwa kwani ni watu wachache mno wanaoweza kuandaa matamasha kama haya na fedha zinazopatikana kuwasaidia watoto yatima na wajane,” alisema Mfutakamba.
Aidha Mtufakamba amesema kwamba kwa kiasi kikubwa tamasha hilo pia litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwani wengi hivi sasa wameamua kujikita katika muziki wa injili kwa ajili ya kumuimbia Mungu na kujipatia kipato.
“Unapokuwa na watu wenye uzalendo kama Msama Promotions kwa hakika kabisa vijana wengi watajitokeza na watahamasika kujiingiza katika muziki huu, kwani watakuwa na uhakika wa kujipatia kipato,” alisema Mfutakamba.
Tamasha kubwa la Pasaka linatarajiwa kufanyika Aprili 24 mwaka huu siku ya sikuu ya Pasaka katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na baadaye kufanyika mjini Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na jijini Mwanza Aprili 26, lengo lake kubwa mwaka huu ni kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasiaid mtaji wa bishara

No comments:

Post a Comment