Friday, February 4, 2011

BREAKING NEWS.... FFU WAVAMIA OFISI ZA GLOBAL PUBLSHER!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Askari wa kutuliza ghasia (FFU) leo asubuhi badala ya kutuliza walikuwa chanzo cha fujo pale walipoingia kama wendawazimu katika ofisi za Kampuni ya Global Publishers na kuanza kupiga makofi na mabomu wafanyakazi.
Polisi hao walifika katika ofisi hizo ghafla huku wakiwa na bunduki na kuanza kufyatua mabomu ya machozi na baadaye polisi kadhaa waliingia ndani huku wakiwa wameshikilia bastola maalum ambapo kulikuwa na kikao cha kupitia magazeti kikiendelea, polisi mmoja  alitoka nje na mtumishi mmoja. Kifupi hali ilikuwa mbaya kutokana na kipigo cha polisi hao  kwa wafanyakazi wasiokuwa na hatia.
Kuona hali inazidi kuwa mbaya, Mhariri Mtendaji Manyota aliwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, (IGP) Saidi Mwema na kumueleza kila kitu kuhusiana na fujo za kikosi cha kutuliza ghasia ambapo kiongozi huyo alishtuka na kutoa pole huku akiahidi kushughulikia suala hilo.
PATA PICHA HALISI ZA TUKIO ZIMA!

Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakijaribu kumchukua mmoja wa wafanyakazi wa Global Publishers, Hassan Ally Daffa kwa madai kuwa ni mmoja wa wanafunzi walioandamana huku wafanyakazi wenzake wakimtetea.
PICHA kwa hisani ya global publisher.

No comments:

Post a Comment