b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, August 23, 2011

BASATA YAHIMIZA MSHIKAMANO WA WASANII

Katibu wa Shirikisho la Filamu (TAFF) Wilson Makubi akizungumza na wadau wa Jukwaa la Sanaa kuhusu uzoefu wake katika Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyowasilishwa hivi karibuni. Wengine kulia kwake ni Katibu wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Dennis Mango na Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufunfi, Adrian Nyangamale

Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Kassim Mapili akieleza jinsi viongozi wa mashirikisho ya sanaa nchini walivyopata fursa ya kuongea na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kuhusu umuhimu wa sekta ya sanaa wakati walipomtembelea bungeni Dodoma hivi karibuni.
Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakiwa wamesimama kumkumbuka Msanii Mahadiya Ally aliyefariki Dunia Usiku wa kuamkia Jumapili na kuzikwa Jumatatu wiki hii Mkoani Tanga.
Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kujenga ushirikiano kupitia vyama na mashirikisho yao ili kuhakikisha kunakuwa na mfumo rasmi na unaoeleweka wa uendeshaji wa tasnia ya sanaa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego wakati akiliahirisha Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ambapo alisema kwamba,wasanii wamekuwa walalamishi tu pasipokuchukua hatua na kuleta mabadiliko ndani ya tasnia.
“Wasanii turudi nyuma katika vyama vyetu, tujiulize kama vyama vyetu viko hai na sisi tuko ndani. Tumekuwa tukilalamika sana, malalamiko mengine ni sahihi na mengine si sahihi. Wakati umefika  wa kuleta mabadiliko” alisema Materego.
Aliongeza kwamba,uwepo wa wasanii wengi hapa nchini pasipokuwa na mfumo unaowaunganisha na kuwaweka pamoja hakutakuwa na maana yoyote hivyo kuna kila sababu ya wasanii wenyewe kuamka na kuujenga mfumo huo.
“Hebu hapa tujiulize ni wasanii wangapi wako katika vyama? Sasa ni kwa vipi sauti yako itasikika wakati hauko katika umoja? Ni lazima turudi nyuma na tujipange katika vyama vyetu na kuyapa nguvu mashirikisho. Tusizungumzie mfumo wakati sisi wenyewe tuko nje ya mfumo” alitoa rai Materego.
Alizidi kueleza kwamba, BASATA katika mwaka huu wa fedha imejipanga kuendesha chaguzi za mashirikisho yote ya sanaa nchini na kuwataka wasanii kujipanga katika vyama vyao na kuhakikisha vinakuwa hai kwa ajili ya kujenga mfumo utakaoleta mageuzi ya maendeleo katika tasnia hii.
Aidha,alisikitishwa na tabia ya wasanii kutokuwa katika vyama na badala yake kukaa pembeni na kutupa lawama au kukosoa mwenendo wa tasnia pasipokuzingatia kwamba wao wanapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko na kupaza sauti zao wakiwa ndani ya mfumo.
“Tuanze kujiuliza sauti zetu zinasikika katika vyama vyetu? Kama hauko katika chama wewe ndiye unayekwamisha ujenzi wa mfumo. Wakati umefika tusiwe watu wa kulalamika bali kuleta mabadiliko ya kweli tukiwa katika umoja wetu” alihitimisha Materego.
Awali katika program ya wiki hii,Viongozi wa mashirikisho ya wasanii nchini walipata fursa ya kuwasilisha uzoefu wao kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyosomwa bungeni hivi karibuni.
 
Picha/Habari na mdau Alistide Kwizela, Afisa Habari wa BASATA

Monday, August 22, 2011

HEPY BIRTHDAYDRAVIC MOUDY

Hongera mwanah kwa kufikiaha miaka ........

Sunday, August 21, 2011

HEPY BIRTHDAY JEROME RISASI

Leo ni siku ya kuzaliwa kwa kaka mkubwa Jerome Risasi. Uongozi wa kampuni ya Sule's Inc. & Entertainment na blog ya Mtoto Wa Kitaa kwa pamoa wanamtakia kheri ya sikukuu ya kuzaliwa

Katibu Mtendaji wa BASATA akimkabidhi bendera Miss Universe 2010

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Bw.Ghonche Materego akimkabidhi Bendera ya Taifa mshindi wa shindano la Miss Universe 2010 Nelly Kamwelu anayeelekea Sao Paulo Brazil kuiwakilisha Tanzania kwenye fainali za shindano hilo.
Miss Universe Nelly Kamwelu akionesha bendera aliyokabidhiwa.Ameahidi kurudi na taji nchini.

Thursday, August 18, 2011

FLORAAH MVUNGI: BONGO MOVIES INA RUSHWA YA NGONO!!

MSANII wa filamu Flora Mvungi, amefunguka live na kutoa siri nzito ilikuwa moyoni mwake ya kuombwa rushwa ya ngono kinyume na maumbile kutoka kwa wasanii wakubwa na watu maarufu kwa lengo la kumpa nafasi (scripti) zaidi ya kucheza kazi zao.
kitendo hicho cha kuombwa rushwa ya ngono tena ya kinyume na maumbile kilimpa wakati ngumu kwa kuwa hana tabia hiyo chafu ya udhalilishaji wa kijinsia.
Masharti haya mazito alipewa ili aweze kuonekana kwenye filamu zao
"Kwa kweli nilikuwa katika wakati mgumu unajua wengi walidhani mimi ni mwanamke ambaye naweza kujitoa kama wao wanadhani na ilifika kipindi walinipa hadi masharti ya kucheza kwenye filamu zao," aliongeza.

Wednesday, August 17, 2011

PETER MSUCHU AFANYA ZIARA KATIKA SHULE ALIYOSOMEA

Msechu akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Nia Njema akiwahamasisha umuhimu wa kuifahamu lugha ya kiingereza.
 
Msechu akiwa na baadhi ya marafiki zake aliosoma nao shuleni hapo ambao walimsindikiza katika ziara hiyo.
Msechu akiwa na baadhi ya walimu wa NIa Njema High School
Na Mwandishi Wetu
MMOJA kati ya  washindi wa shindano la Tusker  la Tusker All Stars 2011 Mtanzania Peter Msechu amewaasa wanafunzi nchini kutilia mkazo wa lugha ya Kiingereza kwani inasaidia katika kupata mafanikio. 
Msechu amesema hayo leo jumatano wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nia Njema iliyopo mjini Bagamoyo ambayo aliwahi kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne. 
Alisema kufahamu lugha hiyo ni kitu muhimu kwani kumemsaidia kwa kiasi kikubwa kutwaa taji hilo ambalo litamuwezesha kufanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa duniani.
“Napenda niwaambie lugha ya kiingereza ni mkuhimu katika kusaka mafanikio ya kitu…mimi nilipokuwa nasoma hapa niliona kama mwalimu wangu ananionea baada ya kuniadhibu kutokana na kutoifahamu vema, lakini sasa nimeona hawakuwa wakikosea,”Alisema. 
Aliongeza kuwa, tangu alipoanza mchakato wa kushiriki shindano hilo kwa mara ya kwanza alikutana na changamoto ya lugha hali iliyomfanya aombe msaada wa kufunzwa zaidi na walimu wake hali iliyomsaidia kuchanja mbuga. 
“Asikwambie mtu kiingereza ndiyo kila kitu kwani bila hivyo ningeona aibu kujifunza na kuishia njiani…nawasihi wadogo zangu kuitilia mkazo lugha hii,”Aliongeza.
 Aidha, Msechu aliwashuku walimu wa shule hiyo kwani ndiyo chachu ya mafanikio yake kutokana na shule hiyo kutilia mkazo lugha hiyo kama lugha kuu ya mawasiliano shuleni hapo.
Naye mkuu wa shule hiyo, Anthony Nyenshile alimpongeza msanii huyo kwa kukiendeleza kipaji chake sambamba na kujibidiisha hali ambayo imemfikisha hapo alipo.
“Kwa kweli kijana huyu alikuwa mchapakazi na anayependa sana sanaa…tunakupongeza kwa hatua uliyofikia hivyo tunakutakia kila lka heri katika harakati zako za kimuziki,”Alisema.
 Msechu, pamoja na wenzake wawili Alfa wa Burundi  na  Davis wa Uganda walitwaa ushindi wa shindano hilo lililofikia tamati mwishoni mwa wiki iliyopita huko Nairobi, Kenya.
 Kwa ushindi huo wasanii hao watapata fursa ya kupanda jukwaani na wasanii mbalimbali wakubwa toka nchini Marekani ambao wanatarajiwa kwenda nchini Kenya.

Baby J AACHIA NGOMA MPYA - "FURAHA YANGU"


Wimbo mpya kutoka kwa Baby J msanii wa Zenzi Fleva anayewakilisha ipasavyo kila atoapo wimbo. Hivi sasa ameamua kuja na wimbo mwingine aliupa jina la FURAHA YANGU uliotengenezwa katika studio ya Akhenaton chini ya Producer Lil Gheto. 
Usikilize halafu unipe maoni yako mwanadada amerudi vipi kwa wimbo huu mpya. 

Download and listen for promo ONLY

WASANII WAASWA KUTOUZA HAKIMILIKI ZAO


 Mshauri wa masuala ya Biashara na Mjasiriamali Bw.Alitenus Millinga (Katikati) akiongea na wasanii kuhusu masuala mbalimbali ya kuboresha masoko ya kazi zao kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.Kulia ni Kaimu Mratibu wa Jukwaa Bw.Alistide Kwizela na Mwenyekiti wa program,Bw.Godfrey L. Mngereza
 Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuuza hakimiliki ya kazi wanazobuni kwani kwa kufanya hivyo wanapoteza haki ya umiliki wa kazi zao kwa miaka yote ya maisha yao na miaka hamsini baada ya kifo.
Akizungumza wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu katika Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Mshauri wa masuala ya biashara na mjasiriamali Bw.Alitenus Millinga alisema kwamba, kumekuwa na taarifa za wasanii kuuza haki ya umiliki wa kazi za ubunifu kutokana na kusaka fedha za haraka pasi na kuzingatia athari zake.
“Uthamani wa kazi ya ubunifu huanza na msanii kumiliki haki za ubunifu.Tatizo la wasanii wetu wamekuwa hawathamini hakimiliki na wamekuwa wakiuza bila kuangalia kesho.Wanaangalia leo-leo tu.Hii ni changamoto kubwa” alisema Bw.Millinga.
Aliongeza kwamba,haki za msanii kumiliki ubunifu wake kwa mujibu wa sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki hudumu kwa miaka yote ya uhai wa msanii na miaka 50 baada ya kifo chake hivyo hulka yoyote ya wasanii kuuza hakimiliki kwa kutazama leo tu inawakosesha haki na mapato mengi.
Hata hivyo,alikosoa vikali tabia ya baadhi ya wasanii kunakili kazi za wengine hali inayoifanya tasnia ya sanaa nchini ikose utambulisho wa Taifa letu na kuzifanya kazi hizo sishuke thamani na kudumu kwa muda mfupi.
“Wasanii ndiyo msingi wa ubunifu na ubunifu ni chanzo cha kutatua matatizo na kuleta mambo mapya.Tukiwa na wasanii wa kunakili kila kitu basi maana yake hata taifa lenyewe linakosa utambulisho pia ubunifu” alisisitiza Millinga.
Alizidi kueleza kwamba,ili msanii aweze kufaidi kazi za sanaa lazima azingatie thamani ya ubunifu wake ikiwa ni pamoja na kuzalisha kazi zenye ubora na kulenga soko,kuzingatia mikataba ya masoko,kupanga bei zenye kuzingatia wanunuzi na kuzisambaza kikamilifu.
Aliyataja masuala kama uuzaji wa hakimiliki, kutozingatia mikataba,uharamia  na kupanga bei pasipokuzingatia hali ya uchumi kama changamoto zinazowakabili wasanii katika kupata mafanikio ya kazi zao.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Sanaa, Bw.Godfrey L. Mngereza alisema kwamba,somo lililotolewa na Bw.Millinga kwa wasanii ni kubwa sana na wanapaswa kulifanyia kazi ili kuweza kupiga hatua.

Tuesday, August 16, 2011

DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI ZIPO MTAANI

BONGOUK UPCOMING EVENTS IN LONDON AND MILTON KEYNES

JAY Z AIBUKA KINARA KWENYE TOP 20 YA WASANII WA HIP HOP WENYE MSHIKO MREFU

  1. JAY Z - $37 MILLION
 2. P DIDDY - $35 MILLION
 3. KANYE WEST - $ 16 MILLION
 
 4. LIL WAYNE - $ 15 MILLION
 5. BIRDMAN - $15 MILLION
 6. DR. DRE - $14 MILLION
 7. SNOOP DOGG - $14 MILLION
 8. EMINEM - $14 MILLION
 9. AKON -$13 MILLION
10. LUDACRIS - $12 MILLION
11.WIZ KHALIFA - $11 MILLION

12. DRAKE - $11 MILLION

13. PHARELL WILLIAMS - $10 MILLION
14. TIMBALAND - $7 MILLION

15. SWIZZ BEATZ - $6.5 MILLION

16. NICKI MINAJ - $6.5 MILLION

17. RICK ROSS - $6 MILLION
18. 50 CENT - $6 MILLION

19. PITBULL - $6 MILLION

20. T-PAIN - $5 MILLION

Sunday, August 14, 2011

ANTiVIRUS VOLUME ONE PART II....NI COLORLESS....!

ANTiVIRUS VOLUME ONE PART II....NI COLORLESS....! IKO NJIANI GET READY KUJUA UKWELI ZAIDI

LIGHTNESS: MODEL WA KWANZA KUINGIA UNIQUE TZ TEAM

lightness ni model,muigizaji na muimbaji anafanya kazi za mitindo kwa ujumla,wasiliana na Unique Tz blog unapotaka kufanya kazi na model huyu.

WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KUYEYUSHA VYUMA CHAKAVU(scrapers) IRON STEEL WAKUTANA KUJADILI HATMA YAO

Baadhi ya wafanyakazi wa  kiwanda cha kuyeyusha chuma chakavu (scrapers) Iron steel  wakiangalia makabrasha mbalimbali kabla ya kuanza kwa kikao chao cha kujadili kufukuzwa kazi kwa kudai nyongeza ya mshaara ambapo wafanyakazi 207 wamefukuzwa bila kufata taratibu zakazi.
Mwenyekiti  wa wafanyakazi wa  kiwanda cha kuyeyusha chuma chakavu (scrapers) Iron steel. Bw. Raina Mwanyamba akizungumza wakati wa mkutano wao wa kujadili kufukuzwa kazi kwa kudai nyongeza ya mshaara ambapo wafanyakazi 207 wamefukuzwa bila kufata taratibu zakazi.
Mmoja ya Wafanyakazi wa kiwanda cha kuyeyusha chuma chakavu (scrapers) Iron steel Omari Salumuakizungumza katika kikao chao cha kujadili kufukuzwa kazi kwa kudai nyongeza ya mshaara ambapo wafanyakazi 207 wamefukuzwa bila kufata taratibu zakazi.(PIcha na Mpigapicha Wetu)
kwa maelezo zaidi:-
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times

MABONDIA WANAWAKE KUAMASISHA NGUMI IDI PILI MORO

MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika siku ya Idd pili katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa katika raundi 10 uzito wa Kg 72 huku likisimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa (PST).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku likiwa katika uzito wa kg 52 ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.
"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.
Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia anaendelea kujifua katika gym yake tayari kwa kusubiri siku hiyo ambapo maandalizi yanaendelea.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo hapo uwanjani na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi

Thursday, August 11, 2011

MTOTO WA KITAA KAZINI (TUNAANDAA VIPINDI VYA TV)


Sule Junior (kulia) akisimamia mpango mzima huku akiwa na kameraman pembeni
Mwanadada Mina akifanya mahojiano mafupi na wadau wa burudani
SULE’S INC.& ENTERTAINMENT kwa kushirikiana na mtoto wakitaa inaandaa kipindi / vipindi vya burdani ambacho muda sio mrefu kitakuwa hewani!
Wadau wote wa burudani na hasa wa huu muziki wa bongo mnaombwa make katika mkao wa kula!

Monday, August 8, 2011

WATCH A VIDEO OF CHAMPY (SHOW ME THAT MOVE)

Champy ni msanii kutoka Mzuka Record ambayo ipo chini ya Art In Tanzania huku producer wake akiwa ni Benjamini wa mambojambo ambaye ameifanya ngoma hii kuanzia audio mpaka video.

KAMA IPO - PROF. JAY

Saturday, August 6, 2011

SUPER D AACHIA DVD TATU ZA KIMATAIFA KUFUNZIA NGUMI

Super D Boxing Coach

Na Mwandishi Wetu

Kocha maarufu wa mchezo wa ngumi nchini, Rajabu Mhamila 'SUPER D' aliyeamua kutumia njia ya DVD kuwafundisha watu mbalimbali kujua na kutambua sheria za mchezo huo ameachia kazi nyingine tatu mpya.
Kazi hizo tatu zinausisha mapambano kadhjaaa ya nyota na mabingwa wa ngumi za kulipwa Duniani, ziliachiwa sokoni zaidi ya wiki moja sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari Super D, alisema tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa 'clips' za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.
Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.
''katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tatu tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition '' alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti  pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza 'live' chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana mbalimbali

ENZI HIZO (1978 TOP TANZANIA'S SPORTSMEN)

FROM LEFT: Filbert Bayi ( World 1500m Champion) ; Gidamis Shahanga ( Commonwealth Marathon Champion) ; Emmanuel Mlundwa ( Africa Flyweight Champion) ; Lucas Msomba ( Africa Light Welterweight Champion ) ; Suleiman Nyambui ( Africa 10,000m Champion ).picha na SUPER D.