Thursday, August 18, 2011

FLORAAH MVUNGI: BONGO MOVIES INA RUSHWA YA NGONO!!

MSANII wa filamu Flora Mvungi, amefunguka live na kutoa siri nzito ilikuwa moyoni mwake ya kuombwa rushwa ya ngono kinyume na maumbile kutoka kwa wasanii wakubwa na watu maarufu kwa lengo la kumpa nafasi (scripti) zaidi ya kucheza kazi zao.
kitendo hicho cha kuombwa rushwa ya ngono tena ya kinyume na maumbile kilimpa wakati ngumu kwa kuwa hana tabia hiyo chafu ya udhalilishaji wa kijinsia.
Masharti haya mazito alipewa ili aweze kuonekana kwenye filamu zao
"Kwa kweli nilikuwa katika wakati mgumu unajua wengi walidhani mimi ni mwanamke ambaye naweza kujitoa kama wao wanadhani na ilifika kipindi walinipa hadi masharti ya kucheza kwenye filamu zao," aliongeza.

No comments:

Post a Comment