Wednesday, September 30, 2015

TIMU NIMESTUKA WATOA SALAMU KWA WAKAZI WA IGUNGA


Msanii Inspector Haarun akiwa ameongozana na Kasala wakiingia eneo la mkutano mjini Igunga.
Msanii Kupa akiwa amembeba msanii wa vichekesho, Tausi huku Msanii Ndede akipunga mkono kuwasilimia wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini hapo kwa shuguli za Kampeni.
Msanii Kajala akitoa ishara ya Gole Gumba kama alama ya CCM kwa wakazi wa mji wa Igunga alipoitwa jukwaani kuwasalimia wana Igunga.
Msanii Ray Kigosi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Sehemu ya baadhi ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo.
Msanii Aunt Ezekiel akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii wa vichekesho, Mr Kupa akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Wasanii wa Bongo Muvi, kuanzia kushoto ni Stan Bakora, Aunt Ezekiel na Kajala wakifuatilia mkutano wa kampeni ulifanyika mjini Igunga.
Msanii wa Bongo Muvi, Sajent akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii Kitale akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii Kitale akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii Kajala akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii vichekesho, Mboto akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii vichekesho, Mboto akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.

Msanii Ndende akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.

Msanii vichekesho, Tausi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.

Mboto akiwaaga wana Igunga mara baada ya mkutano kumalizika.
Picha zote na Sule Junior

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MWANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA IKULU DAR, AAGANA NA BALOZI WA MALAWI TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (wa tatu kulia kwake) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, (katikati yao) wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Sept 30, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuwasili nchini. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 alipofika kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi. Picha na OMR

Tuesday, September 29, 2015

WASANII WA TIMU NIMES'TUKA WAAGA MWILI WA MAREHEMU MAMA CELINA KOMBANI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO

Wasanii wa Timu NIMES'TUKA wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Morogoro kuuga mwili wa marehemu Celina Kombani
Wakipata maelekezo
Wakisalimiana na mbunge wa Morogoro Mjini, Mh Abood
Mboto, Juma Nature na Rich One wakipita kutoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Celina Kombani
Ndende, Stan Bakora na Saguda wakipita kutoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa mama Celina Kombani
Kupa akiwa amembeba msanii Tausi wakipita kutoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Celina Kombani
Ray Kigosi (kushoto), Sajent (katikati) na Kitale wakipita kutoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Celina Kombani
Aunt Ezekiel na Kajala wakipita kutoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Celina Kombani.
Picha Zote Na Sule Junior

Monday, September 28, 2015

BASATA KUINUA MUZIKI WA REGGAETIMU 'NIMESTUKA' ILIVYOFANYA MAMBO DODOMA MJINI

Juma nature na Inspekta Haarun na wasanii wengine wakiwa wanaingia katika viwanja vya Mnadani mjini dodoma.

Baadhi ya wasanii waliokuwa ukawa na kurudi Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mji wa Dodoma wakiwastua wanadodoma kustuka kuwa ukawa hakuna sera hivyo ndiomaana wameamua kurudi ccm.
Wasanii hao wanaunda timu waliyoipa jina la NIMESTUKA wanafanya kampeni za kuwastua watu katika baadhi ya mikoa ya tanzania.

Msanii Stan Bakora akisalimiana na mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini, Antony Mavunde mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Ray Kigosi akiwa na msanii mwenzake wakisalimia wananchi wa dodoma mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Juma nature na Inspekta Haarun na Rich One wakikamua katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Msanii Kitale, Ndede na Mboto wakisalimia wananchi wa dodoma mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Aunt Ezekiel akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Dodoma mjini katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma

Stan Bakora na Mr. Kupa wakifanya yao katika viwanja vya Mnadani Mjini Dodoma. Picha zote na Suleiman Lyeme

Thursday, September 24, 2015

Airtel yazindua kifurushi cha “Yatosha Nyts” bila kikomo

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki wakionyesha bango kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kama ishara ya kuzindua huduma mpya ya kifurushi cha ‘Yatosha Nyts’ itakayomwezesha mteja kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo pamoja na kupata kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.


Na Mwandishi Wetu
Wateja kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi bila kikomo· Piga simu bure kila siku kuanzia saa 5 usiku mpaka 12 asubuhi.

 Kwa shilingi 300 tu. Dar es Salaam,Jumatano 23 Septemba 2015, Kampuni ya simu za mikononi Airtel imewapa sababu nyingine wateja wake kufurahia usiku kwa kuwapatia “Yatosha Nyts” ofa inayowawezesha kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo,pamoja na kifurushi cha internet cha MB 10 kwa kiwango cha shilingi 300 tu.

Ofa hii ya “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwenda mitandao yote kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi hadi siku za wikiendi.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema, “ Tunatambua wateja wetu wanamahitaji tofauti ya huduma za simu. “Yatosha Nyts” ni ofa kabambe na ya kipekee inayo kidhi mahitaji ya wateja wetu. Tumezindua “Yatosha Nyts” ofa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu ya kuwasiliana na kupanga shughuli za siku inayofuata bila hofu ya kupungukiwa na salio kwenye simu zao.

 “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja kuwasiliana na familia, marafiki , mpenzi na wafanya biashara wenzake wakati wa usiku kwa bei nafuu zaidi.

Aliongeza kwa kusema, “ikiwa ni mwendelezo wa kutoa huduma za mawasiliano bora zenye gharama nafuu, wateja wetu wanauwezo wa kununua kifurushi cha “Yatosha Nyts” wakati wowote na kuanza kufurahia kupiga simu, kutuma SMS bila kikomo na 10MB za kuperuzi.

Kwa shilingi 300 tu wateja wetu nchi nzima wanaweza kupiga simu bila kikomo Airtel kwenda Airtel , kutuma ujumbe mfupi (SMS) bila kikomo kwenda mitandao yote na 10 MB za kuperuzi katika mitandao ya jamii kila usiku. Kujiunga na “Yatosha Nyts” piga *149*99#, “Yatosha Nyt” ni offa mpya na moja kati ya ofa nyingi zenye ubora ambazo Airtel inawatapia wateja wake chini ya huduma ya kibunifu ya Airtel Yatosha.

Airtel Yatosha inawapatia wateja wetu uhuru wa kununua kifurushi kinachowafaa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kutembelea sehemu za kutoa huduma.

Yatosha pia inawawezesha wateja kutengeneza kifurushi wanachokipenda, huduma ya kibunifu na ya kwanza kutoka Airtel

Friday, September 18, 2015

"NEW AUDIO" UJANA - SKYWALKER FT WAKAZI, DAMIAN SOUL, OBI ELINAMI, P THE MC, ZAIID & KICHE LEGEND


Pata picha wanapokutanishwa rappers wakali watano na waimbaji wawili mashuhuri wa R&B kwenye wimbo mmoja! Matokeo yake utayafahamu zaidi pale utakapotenga dakika zaidi nne kuusikiliza wimbo huu ambao hauishi kuwa na ujumbe muhimu tu, bali wenye mdundo wa kuvutia, mashairi makali na style za kutofautiana za uchanaji pamoja na melody tamu za R&B.
Wimbo huu uliotayarishwa na Skywalker unazungumzia ndoto chanya za vijana wanaotumia nguvu, elimu na vipaji vya kujitengenezea maisha yao mazuri sasa na sio baadaye. Ujana ni wimbo unaowakumbusha vijana kuwa wakati wa kutafuta maisha mazuri ndio huu na kila mmoja anapaswa kuchangamka.

VERSE 1 BY P THE MC

P ni zao za Tamaduni Muzik na kwa wale mashabiki wanaohudhuria vilinge vya Msasani Club watakuwa wanajua uwezo wake. Hadi sasa ameshaachia zaidi ya nyimbo 30 ambazo zinapatikana kwenye akaunti yake ya Mkito. Kwa ushirikiana na Zaiid, waliachia mixtape yao iitwayo Mwenge Kiwalani. Hivi karibuni aliachia ngoma yake ‘Run DSM’ aliyowashirikisha Dully Sykes na Young Killer.

VERSE 2 BY OBI ELINAMI

Obi ni muimbaji wa R&B na producer ambaye kutokana na kazi zake za corporate zimemfanya asijulikane sana lakini uwezo wake si wa kuelezeka kirahisi. Pamoja na kuachia ngoma zake mwenyewe zikiwemo Lost, Right/Left, Far Away na Nilipokuona amekuwa akifanya cover za wasanii wa nje ukiwemo ‘I'm Not The Only One’ wa Sam Smith.

VERSE 3 BY WAKAZI

Wakazi ni miongoni mwa rappers wa Tanzania wenye mixtapes nyingi zaidi za hip hop zikiwemo tatu za MYU: The Trilogy, Abacus EP na Live From Stakishari. Anatarajia kuachia album yake mpya iitwayo Kisimani.

VERSE 4 BY ZAIID

Hili ni zao lingine la Tamaduni Muzik. Zaiid alijipatia sifa zaidi pale alipoachia cover ya wimbo wa J.Cole, Who Dat. Mwaka 2013 aliachia mixtape yake iitwayo KANDA MBOVU. Yeye na P The MC wana mixtape yao ya pamoja, Mwenge Kiwalani. Hivi karibuni aliachia cover ya wimbo wa Fetty Wap ‘Trap Queen’ aliyoipa jina ‘Madebe.’

VERSE 5 BY DAMIAN SOUL

Damian alianza kufahamika kutoka kwenye mashindano ya Tusker Project Fame kabla ya kuanzisha career yake kama solo artist. Amefanikiwa kutoa hits kadhaa zikiwemo Ni Penzi na Baraka alizomshirikisha Joh Makini na wimbo wake wa sasa ‘Tudumishe’ aliomshirikisha G-Nako. Mwaka jana alikuwa mmoja wa wasanii walioshiriki kwenye shindano la Maisha Superstar.

VERSE 6 BY SKYWALKER

Sky ni mtangazaji wa redio, mhariri wa tovuti ya burudani ya Bongo5.com na producer pia. Amewahi kutoa mixtape yake iitwayo Nimefunzwa.

VERSE 7 BY KICHE LEGEND

Kiche ni kiongozi wa kundi la vijana watano liitwalo 909 wenye nyimbo kama Angalia Juu, Sikubaliwa Kushindwa na Njoo Hapa.

UNAWEZA PIA KUDOWNLOAD WIMBO HUU KWENYE LINK HII: http://bit.ly/1KiDHKH 

Tuesday, September 8, 2015

FLAVIANA MATATA APEWA UBALOZI WA UTAALI

Mwanamitindo wa Kimataifa anaefanyia kazi zake za nchini Marekani Flaviana Matata amechagulia na Wizara ya Maliasili kuwa Balozi wa Hiyari 'Good Will Ambassador' kwa kipindi cha miaka mitatu kwa dhumuni la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.

 Dr Adelhelm James Meru akimkabidhi Flaviana Matata barua ya kuchaguliwa kwake huku kaimu Mkurugenzi Devota Mdachi akishuhudia, katika ofisi za wizara hiyo

Flaviana ambaye juzi alikuwa mmoja kati ya shuhuda wa kushuhudia wizara ya maliasili na utalii wakizindua rasmi tangazo litakalokuwa linatangaza vivutio vya Tanzania nje ya anchi alitawazwa leo hii na katibu mkuu Dr Adelhelm James Meru aliyemkabidhi kwa niaba ya Waziri , Mheshimiwa Lazaro Nyalandu huku Kaimu Mkurugenzi Madam Devota Mdachi akishuhudia.