Friday, September 18, 2015

"NEW AUDIO" UJANA - SKYWALKER FT WAKAZI, DAMIAN SOUL, OBI ELINAMI, P THE MC, ZAIID & KICHE LEGEND


Pata picha wanapokutanishwa rappers wakali watano na waimbaji wawili mashuhuri wa R&B kwenye wimbo mmoja! Matokeo yake utayafahamu zaidi pale utakapotenga dakika zaidi nne kuusikiliza wimbo huu ambao hauishi kuwa na ujumbe muhimu tu, bali wenye mdundo wa kuvutia, mashairi makali na style za kutofautiana za uchanaji pamoja na melody tamu za R&B.
Wimbo huu uliotayarishwa na Skywalker unazungumzia ndoto chanya za vijana wanaotumia nguvu, elimu na vipaji vya kujitengenezea maisha yao mazuri sasa na sio baadaye. Ujana ni wimbo unaowakumbusha vijana kuwa wakati wa kutafuta maisha mazuri ndio huu na kila mmoja anapaswa kuchangamka.

VERSE 1 BY P THE MC

P ni zao za Tamaduni Muzik na kwa wale mashabiki wanaohudhuria vilinge vya Msasani Club watakuwa wanajua uwezo wake. Hadi sasa ameshaachia zaidi ya nyimbo 30 ambazo zinapatikana kwenye akaunti yake ya Mkito. Kwa ushirikiana na Zaiid, waliachia mixtape yao iitwayo Mwenge Kiwalani. Hivi karibuni aliachia ngoma yake ‘Run DSM’ aliyowashirikisha Dully Sykes na Young Killer.

VERSE 2 BY OBI ELINAMI

Obi ni muimbaji wa R&B na producer ambaye kutokana na kazi zake za corporate zimemfanya asijulikane sana lakini uwezo wake si wa kuelezeka kirahisi. Pamoja na kuachia ngoma zake mwenyewe zikiwemo Lost, Right/Left, Far Away na Nilipokuona amekuwa akifanya cover za wasanii wa nje ukiwemo ‘I'm Not The Only One’ wa Sam Smith.

VERSE 3 BY WAKAZI

Wakazi ni miongoni mwa rappers wa Tanzania wenye mixtapes nyingi zaidi za hip hop zikiwemo tatu za MYU: The Trilogy, Abacus EP na Live From Stakishari. Anatarajia kuachia album yake mpya iitwayo Kisimani.

VERSE 4 BY ZAIID

Hili ni zao lingine la Tamaduni Muzik. Zaiid alijipatia sifa zaidi pale alipoachia cover ya wimbo wa J.Cole, Who Dat. Mwaka 2013 aliachia mixtape yake iitwayo KANDA MBOVU. Yeye na P The MC wana mixtape yao ya pamoja, Mwenge Kiwalani. Hivi karibuni aliachia cover ya wimbo wa Fetty Wap ‘Trap Queen’ aliyoipa jina ‘Madebe.’

VERSE 5 BY DAMIAN SOUL

Damian alianza kufahamika kutoka kwenye mashindano ya Tusker Project Fame kabla ya kuanzisha career yake kama solo artist. Amefanikiwa kutoa hits kadhaa zikiwemo Ni Penzi na Baraka alizomshirikisha Joh Makini na wimbo wake wa sasa ‘Tudumishe’ aliomshirikisha G-Nako. Mwaka jana alikuwa mmoja wa wasanii walioshiriki kwenye shindano la Maisha Superstar.

VERSE 6 BY SKYWALKER

Sky ni mtangazaji wa redio, mhariri wa tovuti ya burudani ya Bongo5.com na producer pia. Amewahi kutoa mixtape yake iitwayo Nimefunzwa.

VERSE 7 BY KICHE LEGEND

Kiche ni kiongozi wa kundi la vijana watano liitwalo 909 wenye nyimbo kama Angalia Juu, Sikubaliwa Kushindwa na Njoo Hapa.

UNAWEZA PIA KUDOWNLOAD WIMBO HUU KWENYE LINK HII: http://bit.ly/1KiDHKH 

No comments:

Post a Comment