Monday, November 26, 2012

MWIGIZAJI JOHN STEPHANO KUZIKWA JUMANNE MAKABURI YA KINONDONI


JOHN STEPHANO- Enzi ya uhai wake

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwao Mwananyamala 'A'  jirani na Kopakabana Bar  jijini Dar es Salaam.

Marehemu John anaetarajiwa kuzikwa kesho siku ya jumanne Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam, 
John alianza kujiingiza katika Sanaa ya Uigizaji mwaka 2001 chini ya wasanii wenzake, Thea na Deo Shija na ilipofika mwaka 2008 alianza kuigiza filamu na hadi mauti yanamfika alikuwa njiani kutoa Filamu yake.
Pia Mtanzania yeyote atakae guswa na Msiba huu anaweza kutuma Rambi Rambi zake kupitia Namba ya Tigo Pesa za 0715541714 au 0718951355

No comments:

Post a Comment