Sunday, November 25, 2012

PATA MASAHIRI (LYRICS) YA WIMBO WA SIHITAJI MARAFIKI KUTOKA KWA FID Q.


SIHITAJI MARAFIKI
VERSE 1

Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani/
haijalishi ulikua na wangapi bali wangapi uko nao..
washkaji ambao... 
kosa lako lao wakati hauna mafa
wanaokufikiria wewe muda ambao
wenzao walionao wanafikiria wengine ndo wanao
now kupata washkaji ukiwa na pesa... ni rahisi
kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi mie sikufichi sihitaji urafiki na usupastaa
ukihit ndo unang'aa.. 
upishwe useat kwenye bar
upewe beat na lamar kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground
sikuhizi mabinti wanaomiss ni walionidiss mie sio mdau
wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mmwanza
ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za kwanza
U-N-I-T na prof Ludi walionifunza kukaza...
kwetu mbali.. sijui lini nitarudi? (C) Lokua kanza
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea
aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

VERSE 2
Na usupastaa huwa ni feki.. utakung'arisha ukiwa na Market
utakupatia senti,utapita juu ya red carpet
utageuka young & restless, utakupa wanawake
utakupa mafake brethrenz.. kisha utaenda zake
kwahiyo power its not permanent.. huwa ipo kwa muda tu
respect ur own conglomorete... fikiri kikubwa tu
masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru
wanazusha najiskia.. so im my own best friend
sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man
naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention, lakini sio tajiri wakuafford kuua true friendship
tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga/na hizi falsafa double double ajabu sio kinywa cha mjomba
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

VERSE 3

Rafiki wa kweli yukoje.. ni mkimya au anayechonga
yule aliyekupa jina? au pengine anayekuponda? anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?
au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?/ hakuna adui mbaya ka rafiki yako mwenyewe ambaye hajui.. ka yupo nawe.. au yupo kinyume na wewe/bora adui.. kama hachachawi utaenda muomba akuelewe
ka buibui.. naweka tandu mtaenda kando mzingue?
kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo
Inabidi tu uwaache wakuwatch kwenye kideo/unakula nao happy leo.. kesho wanamtaka mkeo/urafiki sitaki.. hauletagi maendeleo..
nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama nature
wachache niliowafanya wakang'aa wanayaweka maisha yangu in danger
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

No comments:

Post a Comment