Friday, November 16, 2012

MAISHA PLASS: WASHIRIKI KUMI KIKAANGONI


Na Julieth Kulangwa
BAADA ya wiki iliyopita kuhsuhudia washiriki wawili, Bereniki na Justin wakitolewa katika 'fake eviction', waliobaki walipendekezana na kujikuta kumi kati yao wakiingia kikaangoni.
Justin na Bereniki baada ya 'kula bata' walirejeshwa kijijini bila wenzao kuwa na taarifa hiyo, wengi walionekana machoni kuwafurahia wenzao waliporejea lakini mioyoni huenda walikuwa tofauti.
Kwani Bereniki ambaye alijiapiza kuwa atahakikisha mwaka huu mwanamke anachukua ushindi, hata baada ya kurejea aliendeleza maneno hayo huku akisisitiza kuwa harakati zinaendelea.
Haina ubishi kuwa Justin na Bereniki ni kati ya washiriki wenye nguvu kwa maana hiyo kurudi kwao kutakuwa kumewashtua wale ambao waliamini kuwa kikwazo kimeondoka.
Lakini kumbuka wiki hii pia itakuwa tofauti na wiki tatu za mwanzo ambapo washiriki wawili walikuwa wakiaga mashindano kwani safari hii watatu na wa mwisho wataondoka kijijini.
Washiriki waliongia kikaangoni ni pamoja na Rashid Ndunduke, Bahati Kisula, Dora Mhando, Swaumu Shaaban, Magret Msechu, Tatu Masoud, Saad Mohames, Gabriel Lwinga, Hidaya Abdallah na Jonathan Joachim.
Baada ya mtoano huu washiriki kumi nane watabaki na hakutakuwepo mwingine mpaka shindano hili litakapofikia tamati mwezi ujao.
Shindano lilianza likiwa na washiriki 26, mpaka sasa washiriki wanne walitolewa moja kwa moja na wengine wawili walitolewa na kurudishwa katika fake eviction wiki iliyopita.
Mshindi atakuwa mmoja tu ambaye atajishindia kitita cha shilingi za Tanzania milioni 20. Huyu atapatikana kwa kupigiwa kura nyingi na watazamaji.

Mashabiki kujishindia zawadi.......
'Fans'  wanaweza kujishindia zawadi nyingi zikiwemo fedha taslimu, kompyuta aina ya laptop na fursa adimu ya kutembelea kijiji cha Maisha Plus..
 Kushiriki, andika neno MAISHA kisha tuma kwenda namba 15678 na baada ya hapo yatakujia maswali rahisi kuhusu MAISHA PLUS, JIBU maswali yote. -- Unaweza kuwa mmoja kati ya washindi.

No comments:

Post a Comment