Monday, September 24, 2012

MCHEZO WA ATALANTA KUTIKISHA TAMASHA LA BAGAMOYO


Na Mwandishi Wetu
KUNDI la Das Letzte Kleinod (PICHANI) kutoka Ujerumani kesho (Jumanne) litafanya onyesho la mchezo ya kuigiza  wa ATALANTA unaozungumzia masuala ya Utekaji nyara na uharamia  wa utekaji wa meli katika Pwani ya Somalia.
Mchezo huo ambao umelenga kualezea masuala mbalimbali ikiwemo madhara yatokanayo na uharamia huo unaofanyika katika Pwani ya Somalia kwa zaidi ya Miaka 20, utaonyeshowa katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo na baadaye utaonyeshwa kwenye ukumbi wa Goethe Institute jijini Dar es Salaam ijumaa.
Kwa mujibuwa Mratibu wa Kikundi hicho Juliane Lenssen, mchezo huo  wa ATALANTA umeandaliwa kutokana na ripoti iliyotokana na utafiti uliofanywa na mwandishi na muongozaji wa mchezo huo Jens-Erwin Siemssen katika pwani ya Somalia, na pwani za Afrika Masharki.
Amesema kundi hicho kimepata mwaliko wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuja Tanzania kuonyesha mchezo huo ambapo pia umshirikisha wasanii wawili kutoka Tanzania, mmoja kutoka Kenya na wengine kutoka Ujerumani.
Huu ni mchezo wa pili kwa kikundi hiki kutengeneza kuhusisna na masuala mbalimbali ya Afrika ambapo mwaka 2007, kikundi hiki kiliandaa mchezo wa Mkono wa Damu ambao ulikuwa ukizungumzia masuala mbalimbali ya utumwa  ambao ulionyesha katika nchi mbalimbali na kwa hapa Tanzania ulionyesha katika miji ya Bagamoyo na Zanzibar.
mwisho.

No comments:

Post a Comment