b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, September 25, 2012

KIDEDEA  WATAKA SANAA YENYE UJUMBE KWA JAMII.

Wasanii kikundi cha Chemchem Arts wakiigiza mchezo mfupi kuonyesha nguvu ya sanaa za maonyesho katika kufikisha ujumbe, kwenye Jukwaa la sanaa Jumatatu iliyopita.
Wasanii wa kikundi cha Chemchem Arts maarufu kama Kidedea, wakiwa jukwaani wakati wakionyesha mchezo wao uliokuwa na lelo la kuonyesha jinsi sanaa za jukwaani zinavyoweza kufikisha ujumbe.
**********************
Na Mwandishi Wetu
KIKUDI cha Chemchem Arts Group, maarufu kwa jina la Kidedea kimelezea umuhimu kwa wasanii hapa nchini kuandaa michezo ya kuigiza itakayokuwa na ujumbe mahsusi utakaoisadia jamii ya Tanzania kutafakari juu ya muskabali wa masuala mbalimbali  yanayoendelea hapa nchini.
Akitoa wasilisho katika Jukwaa la Sanaa Katibu wa Kikundi hicho Christian Kauzeni amesema moja kati ya mapungufu makubwa ya sanaa za hapa Tanzania ni kushindwa kufikisha ujumbe utakaoifanya jamii kupata hisia, kuamka na kuchukua hatua juu ya masuala mbalimbali yanayowakabili wanajamii.
Marta baada ya wasilisho lake lililoeleza changamoto na mafanikio ya kikundi hicho katika ufanyaji wa sanaa, kikundi hicho kilionyesha mchezo mfupi wa kuigiza  uliojadili pamoja na mambo mengine tabaka lililopo kati ya tajiri na masikini.
Mchezo huo ulionyesha jinsi wananchi walivyo na hasira ya kuhukumu na kuwauwa vibaka  na wezi wa kuku huku wakiwaacha mafisadi wanaolihumu taifa wakiendela kutamba na magari ya kifahari. Mchezo ulilenga katika kuwapa tafakari watazamaji juu ya namna ya kuchukua hatua katika kukabiliana na masuala mbalimbali yanayojitokeza katika maisha ya kila siku  hapa nchini.
Wakichangia mara baada ya wasilisho na mchezo huo, baadhi ya wadau wa masuala ya sanaa wameeleza umuhimu wa jamii kuamka na kuchukua hatua stahili juu ya masuala muhimu badala ya kuacha mambo makubwa kupita na kuisha kirahisi na badala yake wahoji kwa kina kwa viongozi waliowachagua.
Akijibu hoja za washiriki, Kauzeni alisema ni muhimu sana kwa watu kushiriki michakato mbalimbali ya maamuziki ikiwa ni pamoja na kuhudhuria vikao vya serikali za mitaa kwani huko ndiyo wananchi wanaweza kuanza kuleta mapunduzi ya kweli kwa kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa.

No comments:

Post a Comment