Saturday, September 25, 2010

TUWASAIDIE WATOTO HAWA WA MITAANI WA NEW HPOE FAMILY STREET CHILDREN.

KITUO cha kulea watoto waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu na Hatarishi cha ‘New Hope Family Street Children’ cha jijini Dar es Salaam kimewaomba wafadhili kujitokeza kwa wingi ilikuwasaidia misaada ya haraka ikiwemo chakula na mahitaji mengine ya muhimu ya kila siku.
Walisema hayo jana wakati wakipokea msaada huo wa vyombo vya ndani vilivyotolewa na Uongozi wa Vijana kupitia Pasta Freddie Kyara na 'Madam Nuru' wa Kanisa la St. Columbus la Upanga jijini Dar es Salaam, katika makazi ya watoto hao kilichopo Ungindoni Kigamboni.
Vitu hivyo vilikabidhiwa na Mratibu wa na Afisa uhusiano wa kituo hicho Andrew Chale kwa niaba ya uongozi huo wa vijana wa St.columbus Youth, kwa watoto hao, Andrew aliwashukuru wasamalia kwa kujitokeza na kutoa msaada wao ambao umeweza kuonyesha tija na faraja kwa watoto hao.
"Tunashukuru sana kwa msadaa wa vitu hivi ambavyo ni chachu kubwa sana kituo hichi tunaomba wadau wengine kujitokeza ilikufanikisha zoezi la kuwasaidia watoto hawa' alisema Andrew.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kituo hicho Omary Rajabu alisema kuwa watahakikisha wanavitunza na kuvitumia kwa matumizi sahihi yaliyokusudiwa na kituo hicho. “Tunafarijika kwa msaada wa vitu hivi tunahakika vitakuwa faraja kwetu na kuvitunza ilikufanikisha kazi shughuli za kituo” alisema Omary.
Kanisa hilo kupitia vijana wake (St. Columbus Youth) walichangia vyombo mbalimbali vya kupikia ikiwemo; taa za chemri,masufulia,vikombe,sahanai,jiko,na ndoo za maji na vifaa sabuni na miswaki.
Watoto hao kwa pamoja waliomba jamii iliyo na uwezo kujitokeza kuwasidia misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula na maswala ya elimu. “Tunaomba msaada wa chakula ilikitusaidie kwa miloo kamili tulivyokuwa navyo havitoshelezi” walisema watoto hao.
Kituo hicho kwa siku kinatumia chakula kilo 25, kiwango ambacho kwa hali ya kituo chao akikidhi hivyo waliomba wadau walio na uwezo kujitokeza na kuwasaidia vitu kama Mchele, Unga, Maharage ,mafuta na vyote vya kula.

No comments:

Post a Comment