Monday, September 6, 2010

HALIMA MDEE ATEMA CHECHE JIMBO LA KAWE.

Kamama kawa kama dawa mtoto wa kitaa jumapili huwa nakuwa nimetulia tu kitaani kwangu. nikiwa katika misele ya hapa na pale kitaani kwangu si ndio nikasikia sauti kama za mziki hivi zikisikika si ndio nikasema ngoja nijisogeze nicheki kuna kitu gani kinaendelea kitaani kwangu kwa maana siku zote za wiki mtoto wa kitaa nipo na pilika za ujenzi wa hili taifa letu. Kusogea si ndio nikamgumia mdada makini kabisa ambae nkitaaluma ni mwanasheria na kutokana na uwezo wake wa kaza aliweza kulitingisha bunge lililopita akiwa katika vit maalum. Na sasa yupo kikazi zaidi akiwa ndio mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la kawe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHDEMA). Halima Mdee kwa sasa anaendelea na mikutano yake ya kampeni katika jimbo lake ila jana alikuwa kitaani kwetu katika kitongoji cha kawe mzimuni akizungumza na wananchi wa pande zile ambao ndio wapiga kura wake!
Mdee aliongea mambo mengi sana lakini cha misngi alikua anomba tu kura! kauli mbiu yake ni
VIJANA WA KAWE TUAMKE, TUSIDANGANYIKE!

Hapa Halima Mdee akiwa anamwaga sera zake jukwaani.
Hawa ndio baadhi ya wadau waliofika kwenye mkutano huo.
  
Ilifika hatua ya kumtambulisha mama yake mzazi kwa wapiga kura wakena Halima Mdee alifanya kama anavyoonekana
Huyu ndio mama mzazi wa Halima Mdee
Baada ya kuteremka jukwaani alikutana na mwandishi wa habari na aliulizwa maswali mawili matatu na aliyajibui kikamilifu!

No comments:

Post a Comment