Monday, September 27, 2010

WATUMIAJI WA VODACOM SASA KUCHATI BURE.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.
Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.
Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.
“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.
Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.
Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Moderm.

No comments:

Post a Comment