Wednesday, July 27, 2011

Ezekiel Wenje(Mbunge wa Mwanza Mjini - Chadema) Atolewa Bungeni

  
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa upinzani baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.  
  
Pamoja na kusepa lakini Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) aliendelea kula nae sahani moja.   
  
Pamoja na kusepa lakini Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) aliendelea kula nae sahani moja.   
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge baada ya kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
 
Mbunge wa Ilemela kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ezekiel Wenje ametolewa nje ya Bunge katika leo Mjini Dodoma.Mheshimiwa Wenje ametolewa nje ya bunge na Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba ambaye ndiye anayeongoza kikao hicho, baada ya kuvuana huku akihoji kuwa mwenyekiti huyo anaongoza kwa kuwaburuza wabunge.
Wakati Wenje akiwasha kipaza sauti kuzungumza tayari kulikuwa na mabishano yakiendelea kati ya Mbunge Moses Machali (NCCR-Magezi Kasulu Mjini) aliyekuwa akihoji muda mfupi aliokuwa amepewa mbunge wa CHADEMA, Tindu Lisu kuthibitisha kauli yake ambayo alidai mmoja wa mawaziri wenye dhamana na kodi amelidanganya bunge katika majibu yake.
Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo ya Wenje baada ya kutolewa nje anasema mbali na mabishano hayo alitaka kutoa taarifa ya uwepo wa taarifa za kuingia kwa samaki wa sumu nchini jambo ambalo ni hatari kwa wananchi.
Kitendo cha kutolewa kwa Mbunge Wenje bungeni hakikuwapendeza wabunge wa CHADEMA hivyo nao kutoka nje ya Bunge na Kuzungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi huku bunge likiendelea bila ya wao kuwepo Bunge linaendela na Kikao Chake Jioni Hii

No comments:

Post a Comment