b..

B1

Wynem

animation

Friday, June 29, 2012

RAY AZINDUA FILAMU YA SOBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS

Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre   kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.Picha na Mpiga picha Wetu
Msanii wa Filamu Nchini Visent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps.Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya lei kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre vilivyotolewa na Kampuni ya Steps wakati wa Uzinduzi wa filamu yao Mpya ya Sobing Sound.Picha na Mpiga Picha Wetu
Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre   kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.Picha na Mpiga picha Wetu

Na Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu nchini  Visent Kigos 'Ray'  amezindua filam yake  mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.Filam hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filam hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5  kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaamAkizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba  watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha uku wengine wakiendelea kutahabika kitendo ambacho si kizuri.Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atakuwa kila filamu anayotoa atakikisha japo kidogo kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima kwana awajapenda.Alisema msaada uliotolewa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza amesema kampuni ya  Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kutushawishi tuwe tunawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingila magomu.Nae mmoja wa wakilishi wa Kampuni ya Steps Ignatus Kambarage amesema swala la watoto yatima ni letu sote na wala alichagui kwa kuwa tunawajibu na angalau kidogo tunachokipata kupitia filamu zetu tunarudisha kwa kutoa shukrani zetu.

No comments:

Post a Comment