Tuesday, June 19, 2012

MNYIKA ATIMULIWA BUNGENI LEO.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mhe. John Mnyika ametolewa nje ya bunge leo asubuhi na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake aliyosema kuwa Rais Kikwete ni dhaifu wakati alipotakiwa kufanya hivyo.
Mnyika alisema "Tumefika hapa kwa udhaifu wa raisi Kikwete, tumefika hapa kwa uzembe wa wabunge na upuuzi wa serikali ya CCM!!"
Mnyika ametolewa nje ya bunge wakati wabunge wakichangia mjadala wa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni. Mnyika atarudi bungeni kesho saa tatu asubuhi.

No comments:

Post a Comment