Tuesday, May 24, 2011

MAJIBU YA EPPA YAANAZA KUTEMA


....FARIJALA HUSSEIN NA RAJAB MARANDA....

    Hukumu ya kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetolewa leo kwa
   Farijala Hussein na ndugu yake Rajabu   Maranda,wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela ambapo pia wametakiwa kurudisha fedha hizo kwa Serikali
     Jopo la majaji watatu likiongozwa na Mh Saul Kinemela,limewatia hatiani kwa mashitaka nane yanayowakabili shitaka la kwanza lilifutwa kwa kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha hilo,Kwa kosa la pili mshitakiwa wa kwanza pekee atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela,kosa la tatu na la nne 
    washitakiwa wote watatumikia adhabu ya miaka mitano,kosa la tano mshitakiwa wa pili pekee atatumikia adhabu ya miaka miwili jela huku Kosa la sita washitakiwa wote kwa pamoja watatumikia adhabu ya miaka miwili jela na kosa la saba na la nane wote watatumikia adhabu ya miaka mitatu jela," alifunguka Hakimu Mgeta

No comments:

Post a Comment