Friday, May 20, 2011

BREAKING NEWS….. SHEIKH YAHYA HUSSEIN HATUNAE TENA!!


 
Sheikhe Yahya Hussein Enzi za uhai wake

Mtabiri maarufu wa mambo ya Nyota afrika mashariki na Kati Sheikhe Yahya Hussein Amefariki dunia Leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. 
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Lugalo. kwa taarifa zaidi kuhusiana na Msiba wake na habari zaidi juu ya kifo hicho tutawaletea hapa hapa endelea kuwa nasi na utafahamu zaidi. 
Blog hii inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, wananchi wote wa Tanzania kutokana na msiba huu mkubwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na ujasiri wanafamilia yake katika kipindi hiki kugumu cha kuomboleza hadi kuzikwa kwa mwenzetu Sheikhe Yahya Hussein.
SULE'S INC. & ENTERTAINMENT na timu nzima ya blog ya mtoto wa kitaa inatoa pole kwa ndugu jamaa na waislamu wot kwa kuondokewa na ndugu yao kipenzi.
INNA LILLAHI WA INNA-ILAHI RAAJIUUN

No comments:

Post a Comment